Friday 28 August 2009

USALAMA WA MABASI YA ABIRIA:Yote kufungwa mikanda




Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kombe alisema suala la kufunga mikanda katika mabasi sio jambo la hiari na halina mjadala ni wajibu wa kila mmiliki wa basi kuhakikisha anatekeleza agizo hilo kwani ni moja ya sheria za usalama barabarani nchini.
Alisema ifikapo Oktoba mosi basi ambalo litakuwa halijatekeleza agizo hilo litakamatwa na askari na kupelekwa mahakamani pamoja na kulizuia kuendelea kufanya kazi hiyo ya kusafirisha abiria.
Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na mabasi ambayo hayatatekeleza agizo hilo na watapewa adhabu kali kwa kudharau agizo hilo.

Amesema lengo la agizo hilo ni kukabiliana na ajali za barabarani zimalizike ama zitoweke kabisa na kila basi linatakiwa liwe na cheses nzuri, na mikanda ya kuvaa abiria wanapokaa kwenye siti kwa kuwa abiria wamekuwa wakijeruhiwa na kufa kwa kukosekana kwa mikanda hiyo

3 comments:

  1. Afadhali wasisitize mikanda pengine itasaidia kupunguza idadi ya vifo punde ajali inapotokea. Vile vile mikanda itasaidia kupunguza idadi ya watu wanaosimama safari njia nzima!

    ReplyDelete
  2. ila inategemea na ajali kimetokea nini coz inaweza kuwa moto then naturally binadamu ata-panic then mkanda ataona umekwama...good idea ila ndio hivyo tena

    ReplyDelete
  3. Labda watageukia UBORA WA MABODI YA MABASI HAYO kwani kama ndio ambayo serikali ilikiri yako ktk kiwango cha chini, basi wakiwa na mikanda ndio watasagwa nayo. Na pia kama walivyosema Dada Zangu hapo juu, kuna SHAKA na utekelezaji. Ukisoma sheria zetu hazina tofauti na nchi nyingi. Tatizo huwa ni utekelezaji wake.
    Wasipokomesha Rushwa, hata wakiweka CCTV kwenye mabasi, watu wataendelea kufa kwa yasiyotakiwa.
    Blessings

    ReplyDelete

Maoni yako