Sunday 30 March 2014

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA.

Kwakweli wetu Tz tuna shida ya usafiri lakini wenzetu huko wamezidi

UKIWAULIZA???......."Tunatazama mpira"

Saturday 29 March 2014

MALEZI NI HATUA

Katika ukuaji kuna hatua ambazo mtu hupitia hadi ukuaji wake mtimilifu. Hatua kama hii wanayopitia hao japo kwao ni kama kucheza tu lakini yawajenga na hapo baadae kuishi vizuri kifamilia kama mke na mume. Tujitahidi watoto wetu wasiruke Stage wasijefanya hayo ya kitoto wakiwa wakubwa.

Thursday 27 March 2014

RAIS OBAMA AMTEMBELEA PAPA FRANCIS 1 HUKO VATICAN

"Wonderful meeting you. I'm a great admirer," the president said.
"I bring greetings from my family," Obama added. "The last time I came here to meet your predecessor I was able to bring my wife and children."

TASWIRA. FAHARI YA TANZANIA

Wednesday 26 March 2014

YATAKA MOYO NA INATIA HURUMA

Mtoto huyu nae anatamani anywe maji safi na salama lakini ndo hivyo katika mazingira alipo hakuna huduma hiyo. Hapa msaidizi wake ni mungu tu maana wanyama wanatumia maji hayo hayo na yeye pia, ni mungu tu kumnusuru na magonjwa. Serikali inatakiwa kuangalia haya. Hiki ndicho kizazi kinachokua na kuiona serikali kama imewatupa na hivyo kuwa na chuki nayo.

TUKUMBUKE KWETU

Maneno ya khanga lakini yanasema kitu. Basi nami nimeonelea niwape wadau zawadi ya taswira hii ya kwetu.

Tuesday 25 March 2014

KITUO CHA MABASI MOSHI

Madreva na wamiliki wa mabasi yaendayo Arusha na sehemu nyingine ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro yakianzia Kituo hiki cha Moshi, wameweka mgomo wa kutopeleka magari yao stendi leo kutoa huduma, na hatimae kuamua kucheka mpira wa mguu kati ya madreva na makondakta.

Stendi yageuka kiwanja cha kandanda
(Picha kwa hisani ya Dj.Seki)

Monday 24 March 2014

TASWIRA YA UWAJIBIKAJI

Tukiangalia taswira hii tunapata mengi ya kujifunza. Miongoni mwa hayo ni:-
"Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" Mtoto huyu japo katika udogo wake kashaanza kuiga wanachokifanya wazazi au ndugu zake. Yaelekea atakuwa mama mzuri katika mapishi. Ila pia yawezekana akawa mchuuzi mzuri wa biashara ya samaki. Yaelekea pia atakuwa mwajibikaji mwenye kujituma hata katika mazingira magumu kama aonekanavyo hapo bila nguo juu na joto kali la moto.

Ila pengine ni vizuri pia tukaangalia madhara anayowezapata huyu mtoto. Kwanza yaonesha kuna dalili fulani za mzazi au mlezi kuzembea kidogo maana mtoto wa umri huu si vyema kuwa katika mazingira hayo,tena bila uangalizi. Na pili kiafya joto hilo linaweza kuidhuru ngozi ya mtoto huyo ambaye hajajisitiri vizuri. Tuwe waangalifu.

Sunday 23 March 2014

MIAKA 5 TANGU KUONDOKEWA NA BABA MZAZI

Mwandishi wa Blog hii leo anaungana na wanafamilia, Ukoo wa Mwangoka na Swai kufanya kumbukumbu ya miaka 5 tangu kuondokewa na baba yao kipenzi Mzee Amedeus Mwangoka Huko Sanya Juu-Kilimanjaro. Anaomba sala zenu. "Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe"
Baba mzazi enzi za uhai wake.
Mwandishi wa Blog hii akiwa katika majonzi siku ya mazishi ya Baba yake mzazi

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Hii ni namna mpya ya kusalimiana. Ni kama vile wanasema "tunafanya hivi ili kuendelea kuifanya Jumapili kuwa siku takatifu".

Friday 21 March 2014

KUNA LEO NA KESHO

Ndege anapokuwa hai huwa anakula sana funza, lakini anapokufa funza humla yeye.......Maisha yanabadilika kila wakati, hivyo basi usimdharau wala kumuumiza mtu yoyote yule katika haya maisha........Kwani unaweza ukawa imara sana leo, ila kumbuka maisha ni imara kuliko wewe........na elewa kuwa mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima.........Hivyo kuwa mwema kwa kila mtu! kwasababu huwezi jua.
Uliyenae ni rafiki/mume/mke/ndugu wa kweli au wa mashaka tu? Jiulize

KAZI NYINGINE ZATAKA MOYO NA UBUNIFU

Hapa mwalimu anajitahidi kuwapa wanafunzi elimu bila kujali mazingira duni ya kazi yake.
Ubunifu ni muhimu katika kufanya kazi na kujiongezea kipato japo ni katika mazingira magumu.

Tuesday 18 March 2014

MWANAUMEEEEEEEEEE

Mwanaume ni kupiga kazi kwa kwenda mbele. Haijalishi ipi, watasema nini... mradi fedha baba maana ukirudi nyumbani unakutana na mwanao kakaa hivi......
maana kachoka kula hivi......

Monday 17 March 2014

Saturday 15 March 2014

Teh Teh ACHA NICHEKE MIE

Vipi,Shwari?

MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO

Picha hii imepigwa mahali fulani kati ya mikoa yetu ya Tanzania (Jina limehifadhiwa) lakini yatuonyesha namna ambavyo tunapuuzia malezi ya watoto wetu. Mtoto huyu ambae leo anafundishwa na kuruhusiwa kucheza hivyo mbele ya kadamnasi atazuiwa vipi au atajizuia vipi akiwa mkubwa kwenda kucheza vilabuni au katika kadamnasi. Na je hayo ndo maadili ya Mtanzania?. Wazazi tuwe makini na malezi ya watoto.

Friday 14 March 2014

P SQUARE WANATISHA

Pesaa huweza kufanya mengi. Mojawapo ni kupata maisha ya hadhi unayotaka. Pichani ni mazingira nadhifu ya wanamuziki PSQUARE.
Hii ni sehemu ya kupata maakuli

TASWIRA: MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta,Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh.Samia Suluhu, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Sefu Iddi, Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt.Thomas Kashilila na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la katiba aliyemaliza muda wake Mh.Pandu Ameir Kificho(picha na Freddy Maro).

Thursday 13 March 2014

KAZI HALALI NI........

Kwa mtu yeyote,
Wa aina au jinsia yoyote,
Mahali popote,
Ya aina yoyote,
Kwa wakati wowote,
Kwa manufaa yoyote,
ILI MRADI HAVINJI SHERIA
Pichani ni mtu anayeonekana kuwa ana asili ya China, akiwa katika biashara yake ya mahindi_choma katika viunga fulani Jijini.

MDAU WA MUDA MREFU UNAKUMBUKA HII?

Wednesday 12 March 2014

KIJANA MREFU WA KITANZANIA ZAIDI YA HASHEEM THABEET

Huyu ni Baraka kijana mrefu kitanzania

Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam. Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu moja Tsh. 1000.
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. Inasemekana kuna watu wanamfuatilia kumsaidia umaarufu.(Kwa hisani za Xdeejayy blog)
Hapa ni Baraka alipokutana na Hasheem

Monday 10 March 2014

UBUNIFU

Hapa watoto hawa wameamua kubuni njia rahisi za usafiri wao.
Katika kujitahidi kujifunza kwa bidii, huyu nae kabuni njia ya kuzuia usingizi akiwa katika kujifunza. Lakini hapa naona kazidiwa na kaupchapa usingizi hapo hapo. Chezea chemli wewe!

FOLENI JAMANI FOLENI

Wakati kukiwa na ongezeko kubwa la ununuzi wa magari na kusababisha idadi kubwa ya vyombo hivyo vya usafiri, foleni za magari nchini, hasa jijini Dar es Salaam, imefikia hatua ya kutisha huku ikisababisha madhara makubwa kiuchumi, kijamii na kiafya, ikiwamo magonjwa ya akili.

Sunday 9 March 2014

NDEGE YA MALAYSIA YAPOTEA IKIWA NA ABIRIA 239

Ndege aina ya Boeing 777-200ER ya Shirika la Ndege la Malaysia inasadikiwa kuanguka kusini mwa bahari ya China. Ndege hiyo ilikuwa na abiria 227 na wafanyakazi wa ndege 12 ilikuwa ikitokea Kuala Lumpur kuelekea Beijing China. Masaa 2 baada ya kuruka, ndege hiyo haikuonekana katika vyombo vya kuongozea ndege. Mpaka sasa juhudi zinafanyika kujua ilipoangukia na hali za abiria. Hata hivyo vyombo vya habari vya nchi inayohusika vimewatahadharisha ndugu na jamaa kuwa wajiandae kupokea habari ambazo zinasadikiwa zitakuwa si njema.

JUMAPILI NJEMA WADAU

Karibuni upepo mwanana wa Bagamoyo

Friday 7 March 2014

AIR TANZANIA YAPATA NDEGE MPYA

Ndege 5Y-WWA aina ya CRJ200 iliyowasili
Usiku wa kuamkia Ijumaa, Ndege hii mali ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Hongera kwa Shirika hilo kwa kuboresha huduma maana ni hatua nzuri sasa.
Mwonekano wa ndani ya ndege.
(Picha zote kwa hisani ya Dj.Seki Blog)

MVUA JIJINI DAR ZALETA ADHA KUBWA

Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini hasa Jijini Dar zinasababisha kero nyingi ikiwemo hii ya usafiri kama inavyoonekana pichana.
(Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)