Sunday 31 July 2016

USOMPENDA KAJA


MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kahama, James Lembeli, ameibukia katika mkutano wa Rais, Dk. John Magufuli, huku akimwomba kiongozi huyo kuhakikisha anakisafisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).Lembeli ambaye mwaka jana alijiengua ndani ya CCM na kujiunga na Chadema, alisema ikiwa Rais Magufuli atafanya hivyo, yuko tayari kurejea CCM.

Wednesday 27 July 2016

CHEKA KIDOGO NA MAMBO YA TANGA

TAZAMA HII KALI KUTOKA ZANZIBAR

Kwenye mnada wa samaki huko Pemba Bwana mmoja alifika 70,000/ kwa tenga. Akatokea mwakilishi (ccm) akatamka kutoa 140,000/- Cha ajabu yule mchuuzi akampa aliyefikia elfu 70,000/
Mwakilishi alipouliza jamaa akamwambia kwani nyie tukishinda mwatupa?
Chezea Zanzibar wewe!

Tuesday 26 July 2016

MAISHA YA UTOTO RAHA; NO STRESS

Kuwakuta watoto katika hali kama hizi hasa maeneo ya vijiji asilia ni jambo la kawaida na kama ulitokea sehemu kama hizo na hukupitia hatua hizi basi kuna kitu ulimiss.

Monday 25 July 2016

KUMBUKUMBU YA MASHUJAA YAFANYIKA DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao.
Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.
Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.
“Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.
“Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa” Amesema Rais Magufuli.
Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.
Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
25 Julai, 2016

Sunday 24 July 2016

ONLY IN TANZANIA ( INATOKEA TU TANZANIA)

Pikipiki ndani ya mabasi yaendayo kasi

KUMTOA OUT "BABY WAKO" SIO LAZIMA MWENDE BEACH

MWIGIZAJI WA BONGO MOVIES JACKLINE WOLPER ARUDI CCM

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper aliyekuwa akimuunga mkono Edward Lowassa katika uchaguzi Mkuu 2015, ametangaza kujiunga na CCM rasmi jana.Wolper alikaribishwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga na CCM.Kitendo hicho kilifanyika katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika jana Julai 23, mkoani Dodoma.

Saturday 23 July 2016

MHE DKT JOHN MAGUFULI ATANGAZWA RASMI MWENYEKITI MPYA WA CCM TAIFA

Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio ziapatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika.
Wakati huo huo, Mwenyekiti mpya wa CCM amemteua Mhe Kanali Abdulrhamani Kinana kuwa katibu Mkuu wa CCm licha ya kiongozi huyo kabla aliweka nia yake ya kujiuzulu

NCHI YA KITU KIDOGO: HAYA YATAISHA LINI?

"KIBEGA": NI MAPEMA SANA

Kutokana na hali ngumu ya maisha ya jamii nyingi nchini, watoto wengi wamejikuta wakilazimika kufanya kazi ambazo hawastahili katika umri huo. Ni jukumu la viongozi,wazazi na jamii kwa ujumla kuangalia hatua za kuchukua kutatua tatizo hili.

Friday 22 July 2016

SHAMBULIO ENEO LA MADUKA (SHOPPING CENTRE) HUKO MUNICH GERMANY

Habari zinazoendelea mpaka muda huu ni kuwa limetokea shambulio katika eneo la Olympia Shopping Centre huko Munich kusini mwa Ujerumani. Inasadikiwa watu wengi wameuawa na wengi kuumia. Tayari Polisi, zimamoto, Msalaba Mwekundu na wahusika wengine wapo eneo la tukio kuokoa. Treni zote za chini ya Ardhi (U-Bahn) zimeshimama kufanya kazi.
tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyopokea

SAFU YA MAKOCHA MAARUFU KUINOGESHA LIGI KUU YA UINGEREZA

Makocha hao ni pamoja na Klopp (Liverpool)-Guardiola (Man City)-Mourinho (Man United)-Wenger (Arsenal)-Conte (Chelsea)

CCM WAKUTANA DODOMA KWA AJILI YA KUMPATA MWENYEKITI MPYA HAPO KESHO

DALILI ZA KUANZA UJENZI WA RELI YA KATI KISASA WAANZA KUONEKANA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam.

Thursday 21 July 2016

KUDUMISHA MILA

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Hai, mhe Freeman Mbowe akipata kinywaji maarufu huko Kilimanjaro "Mbege" akiwa raia wenzake

Wednesday 20 July 2016

KATUNI: KUELEKEA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA CCM TAIFA

TUMSAIDIE DADA WAKONTA KAPUNDA KUPATA MATIBABU

Wakonta Kapunda : Msichana mwenye umri wa miaka (22) akitumia ulimi kuandika meseji kwenye simu yake ya Mkononi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Dada yake Bi. Judith Assenga.Binti huyo ameanza kutumia kiungo hicho katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Mkoani Tanga
Msichana mwenye umri wa miaka (22) Bi. Wakonta Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Binti huyo anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
Mratibu wa Masuala ya Habari katika Kampeni ya kumsaidia Wakonta Bw. Joseph Kithama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namba ambazo wadau wanaweza kutumia kumchangia Binti huyo anayehitaji msaada ili apatae matibabu na kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam

USHOGA TANZANIA HAUKUBALIKI ASEMA MHE RC MAKONDA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mhe Paul Makonda
DAR ES SALAAM: Watu tisa wanaodaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga), wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakituhumiwa kukusanyika kinyume cha sheria kwa lengo la kupinga amri ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ya kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsia moja jijini hapa.Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, watu hao walikamatwa baada ya polisi kuvamia kwenye Ukumbi wa baa ya Matema uliopo Kinondoni B ambako zaidi ya wanaume 200 wanaodaiwa kuwa mashoga, walikusanyika kwa lengo la kujadiliana kwa kina kuhusu amri ya Makonda ya kuwapiga marufuku ili kutoa tamko la pamoja.

Tuesday 19 July 2016

MASANJA MKANDAMIZAJI ANATUKARIBISHA Agosti 14,2016

NINA KADI YAKO RAFIKI YANGU,
KAMA UNADHANI UNAWEZA KUNIUNGA MKONO TAFADHARI NIWEKEE NAMBA NIKUUNGE KWENYE GROUP LA MARAFIKI WALIOTAYARI HUMO.
MCHANGO NI LAKI 1 TUU!!!
KARIBU SANA RAFIKI,
NAJUA KUNA MWINGINE HATA KUWA NA MCHANGO BASI NISAIDIE HATA MAOMBI🙏🏾
NAJUA KUNA MWINGINE HATA NIOMBEA BASI NISAIDIE KUNUNA😀.
NAJUA KUNA MWINGINE HATA NUNA ILA ATAVIMBA BASI NISAIDIE KUPASUKAA

TUNAAMBIWA TUPENDE VYA (NYUMBANI) KWETU LAKINI mmmmh....

Hivi ni viatu vya dhabatu wanavyopewa wachezaji wa Mpira wa Miguu (Football) kama tuzo, lakini mwenzangu hebu angalia hiyo Gold(dhahabu) ya kiatu chetu!....

Monday 18 July 2016

JE WAJUA HISTORIA YA KIJIJI CHA GEZAULOLE ("KIJIJI CHA WAZURURAJI")

Picha na maelezo kwa hisani ya Majjid Mjengwa
Ndugu zangu,
Nakumbuka utotoni katika jiji la Dar es Salaam, nilishuhudia kwa macho yangu msako wa wazururaji. Ni katikati ya miaka ya 70.
Niliona jinsi mgambo wa jiji walivyokuwa wakiwadhalilisha vijana na watu wazima kwa kuwakamata, kuwafunga mashati na kuwapandisha kwenye malori tayari kwa safari za kwenda Gezaulole. Kosa lao? Walikuwa wakizurura mijini bila kazi. Hivi, anayetafuta kazi atabaki nyumbani kuisubiri, si ni lazima apige mguu kuitafuta? Nakumbuka kama mtoto nilijisikia vibaya sana kuona udhalilishaji ule uliofanywa kwa watu wazima.
Na sijui leo ukifanyika msako wa wazururaji Dar yatahitajika malori mangapi?
Na miaka ile ya sabini tulipokuwa watoto tulisikia hata nyimbo za redioni kuhimiza ‘ wazururaji’ waende kwenye vijiji vipya vilivyoandaliwa na Serikali kama makazi ya ‘ Wazururaji’. Watoto wa enzi hizo huenda tunakumbuka wimbo huu;
“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”
Na Kigamboni ya enzi hizo ilikuwa shamba kweli. Wengi wa waliofikishwa huko Gezaulole na vijiji vingine kule Kigamboni wakayaanza maisha mapya ya vijijini.
Kuna waliokimbia Gezaulole wakarudi tena mjini au kwenye vijiji vyao vya asili. Kuna waliobaki huko Gezaulole, wakafyeka mapori yao. Wakaanza kilimo. Wakaizoea hali mpya. Wakajenga familia zao huko.
Ajabu, leo wenye fedha ndio wanaokwenda kuyanunua kwa bei ya hadaa, maeneo ya watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu. Kuna watoto na wajukuu wa ‘wazururaji’ waliobaki na vieneo vidogo. Miongoni mwao ndio hao wanaofanya shughuli za kusukuma mikokoteni na kuendesha maguta.
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa

BAADA YA MHE.RAIS MUSEVEN WA UGANDA KUSIMAMISHA MSAFARA ILI APOKEE SIMU; YAMEKUWA HAYA:::

Mhe Rais Museven alipoketi pembeni ya Barabara ili kuongea na simu
Masanja mkandamizaji nae yumo

Sunday 17 July 2016

ENZI ZA PEKOSI: ZAMANI RAHA

MHE AUGUSTINE MREMA ATEULIWA MWENYEKITI WA PAROLE

Mh Agustino Lyatonga Mrema Mwenyekiti wa Bodi ya Parole
……………………………………………………………………………………………………………..
Na; Lucas Mboje – Jeshi la Magereza,
PAROLE ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo Gerezani cha miaka minne na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum baada ya kukidhi vigezo vifuatavyo:-
i). Awe ametumikia theluthi (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwenendo wa kurekebika kurudi katika jamii kumalizia sehemu ya kifungo chake kwa masharti maalum. Masharti hayo ni kuwa chini ya uangalizi maalum kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka atakapomaliza kifungo chake, kuzingatia masharti ya Parole anayopewa kikamilifu pamoja na kuwa raia mwema na kuishi kwa kujipatia kipato halali katika jamii;
ii). Awe ameonesha kujutia kosa, kurekebika tabia na kuonesha mwenendo mzuri gerezani na;
iii). Mamlaka husika kujiridhisha kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.

Parole ni moja kati ya adhabu mbadala na imeonesha mafanikio makubwa katika nchi nyingi duniani. Utaratibu huu ni wa kipekee kwa kuwa unawagusa wafungwa wa vifungo virefu ambao ndio wengi waliopo magerezani. Aidha, ni utaratibu unaoshirikisha jamii katika urekebishaji kwa kuzingatia usalama wa jamii na dhana kwamba uhalifu ni zao katika jamii.
Madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu wa Parole nchini hayatofautiani na madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu huu kwenye nchi nyingine Duniani zikiwepo nchi za Afrika kama vile: Afrika kusini, Zambia na Namibia. Mfumo wa Parole ulioainishwa hapa nchini unatokana na uzoefu wa Parole unaotumika nchini Canada.

Saturday 16 July 2016

MATOKEO KIDATO CHA SITA


Baraza la mitihani Tanzania(NECTA) imetangaza matokeo ya kidato cha sita 2016, na Kuzitaja shule zilizo fanya vizuri zaidi Kitaifa na zile ambazo hazikufanya vizuri Kitaifa.

Ubora wa shule umepagwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average – GPA) ambapo A=1, B=2, C=3, D=4, E=5 na F=7.

Aidha, upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30 kama ifuatavyoa:


Shule 10 Bora Kitaifa
1. Kisimiri (Government)

2. Feza Boys (Private)

3. Mwanza Alliance Girls (Private)

4. Feza Girls (Private)

5. Tabora Boys (Government)

6. Marian Boys (Private)

7. Kibaha (Government)

8. Mzumbe (Government)

9. Ilboru (Government)

10. Tandahimba (Private)

Shule 10 za Mwisho Kitaifa
1.Mpendae (Unguja)

2.Ben bella ( Unguja)

3.Tumekuja (Unguja)

4.Green Bird Boys (Kilimanjaro)

5.Jang'ombe (Unguja )

6.Kiembesamaki (Unguja )

7.Tanzania Adventist ( Arusha )

8.Al-Ihsan Girls ( Unguja )

9.Azania (Dar es salaam )

10: Lumumba (Unguja)

Friday 15 July 2016

MHE ZITTO KABWE AUKACHA UKAPERA

Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe jana aliuacha rasmi ukapera baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake aliyemvisha pete ya uchumba miezi miwili iliyopita, ndoa na tafrija zote zilifanyika Zanzibar.

UBUNIFU

Thursday 14 July 2016

UMUHIMU WA LUGHA YA BIASHARA

WALIOSEMA HAWAIVI CHUNGU KIMOJA? (Mhe Msigwa na Mhe Naibu Spika Tulia)

Jana katika ugawaji wa Madawati, waheshimiwa hawa walijikuta wakikaa meza moja na hata kupiga picha ya pamoja. Siasa pembeni katika kuwatumikia Watanzania

Rais Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Iringa (Chadema), Peter Msigwa na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia, kwa kukaa pamoja katika meza kuu wakati wa hafla hiyo.

Wabunge kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walitangaza kususia vikao vya bunge vinavyoongozwa na Dk. Ackson au shughuli yoyote itakayoongozwa naye kwa madai amekuwa akiendesha vikao vya bunge kwa upendeleo na kutaka avuliwe wadhifa huo.

Rais Magufuli alisema inapofika masuala ya kuleta maendeleo ya taifa, viongozi wanapaswa kuweka kando masuala ya vyama.

Alisema hata yeye wakati akipiga kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, aliwaahidi Watanzania kuwa atawatumikia wote bila ya kuangalia vyama, kabila, dini wala rangi.

“Mmeacha vyama vyenu pembeni, mnaunga mkono maendeleo, leo unapomwona Msigwa na Tulia wapo jirani inatia moyo, ndicho tunachokitaka, nchi hii ni yetu sote, tukifanya hivyo nchi yetu itakuwa ya mfano,” alisema Rais Magufuli.

Alipoulizwa kwa kitendo chake cha kuhudhuria shughuli hiyo na kukaa meza moja na Dk, Ackson, Msigwa alisema wamefika katika hafla kama wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge.

Alisema pia walihudhuria hafla hiyo kwa sababu ni suala la maendeleo na walipaswa kushiriki ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kama zilivyopangwa.

“Hii shughuli haiendeshwi wala kuandaliwa na Tulia, ni shughuli iliyoendeshwa na tume yetu na ndiyo maana tupo hapa,” alisema Msigwa