Monday 24 August 2009

NAWATAKIENI WIKI NJEMA

Ni jumatatu tena,mwanzo wa pilikapilika za juma. Nae mwanamama huyu yupo katika pitapita za kutafuta maisha. Jua ni kali na maisha ndio hivyo tena.Kizuri ni kwamba anamjali sana mwanae hadi anatafuta namna ya kumkinga na jua. Hongereni kinamama kwa malezi na matunzo sahihi.Tuongeze bidii katika majukumu yetu,maisha yataboreka tu japo si kwa siku moja.
Wakati kila mmoja akiwa anajibiidisha kutafuta riziki, Mwombaji Maarufu Mzee Matonya ambaye aliondolewa jijini Dar,sasa kahamia katika mitaa ya Mji wa Morogoro akiendelea na mbinu yake ya kutafuta pesa ili kusukuma gurudumu la maisha.

1 comment:

  1. Ahsante kwa kutupa hongera akina mama kwa malezi bora, na ahsante kwa kututakia kuwa tuwe na wiki njema. Nami nasema uwe na wiki njema pia.

    ReplyDelete

Maoni yako