Sunday 28 September 2014

UIWAZAPO KESHO

Kesho ni jumatatu, k2wa wanafunzi hawa wanaosomea sakafuni unadhani watakuwa wanajisikia vizuri kwenda shuleni? Shule ambapo ni sehemu ya kupata elimu ukiwa na utulivu na furaha, kwa hawa ni tofauti kabisa. Serikali na vyombo husika, tupieni jicho jambo hili

KUWAZA KWINGINE UUUH

Wednesday 24 September 2014

UPENDO KWA VITENDO

Pamoja na mafuriko hayo mama huyu amesukumwa na moyo wake kuona afanye hili ambalo mbele ya Mungu ni baraka tele na mbele ya watu ni funzo kubwa.

HABARI NJEMA KWA WASAFIRI WA ANGA

Shirika la ndege la Etihad Airways (http://www.etihad.com) ni shirika la ndege la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu, ambalo linatarajia kuongeza safari zake barani Afrika kwa kuzindua safari mpya ya kila siku Mjini Dar es Salaam, mji mkubwa zaidi Tanzania.
Safari hizi za ndege kati ya Abu Dhabi na Dar es Salaam, zitaanza tarehe 1 mwezi Desemba 2015, zikiendeshwa kwa kutumia ndege ya Airbus A320 yenye viti 16 vya kitengo cha Biashara na 120 vya kitengo cha Uchumi.
Dar es Salaam itakuwa kituo cha 110 cha Etihad Airways duniani kote, na kituo cha 11 barani Afrika na Bahari ya Hindi. Ratiba hii ya kila siku itatoa njia mbili za uunganishwaji katika kitovu cha Etihad Airways mjini Abu Dhabi, pamoja na uunganishaji rahisi wa safari zingine za vituo 45 maarufu katika Mashariki ya Kati, Ulaya, Bara Dogo la India, Asia Kaskazini na Kusini-Mashariki, na Australia

MOVIE MPYA KALI SOKONI. WAHI NAKALA YAKO

Imeshirikisha wakali wa Bongo Movie. Itakuwa sokoni kuanzia kesho 25.09.2014. Usikose nakala yako kama wewe ni mpenzi wa Bongo Movies.

Tuesday 23 September 2014

KWA WAKWE HESHIMA TELE, CHEO PEMBENI

Mhe Mama Tunu Pinda akipiga goti kusalimia wakwe zake alipowasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda huko Kibaoni Katavi.

DALADALA ZA BONGO DAR ES SALAAM

Ukitoka nyumbani inabidi uwe umeshiba vizuri maana pilika za kupata usafiri wa daladala katika baadhi ya maeneo ya Jiji ni tabu sana. Hakuna cha mwanaume wala mwanamke, hapa ni"MWENYE NGUVU MPISHE"
Mambo ya Tandika huko Wilayani Temeke

Monday 22 September 2014

ENZI ZA MWALIMU

Kiongozi mnyenyekevu na wa mfano. baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere
Kilimo kama uti wa mgongo wa maisha ya mtanzania

UGOMVI MWINGINE AIBU TUPU

MAZAO YA NYUMBANI

Kinamama wakiuza mikungu ya ndizi katika moja ya masoko huko Kilimanjaro

Sunday 21 September 2014

UBUNIFU WA KWELI

Pengine tatizo letu ni kipato, uongozi bora na tekinolojia, lakini vichwa vimejaa mawazo mazuri na endelevu

PICHA HII ITUFUNDISHE UPENDO WA KWELI

Ila huu hapa ni urafiki na upendo wa mashaka

KUDUMISHA MILA

Wazee wa Kimasai wakila nyama mara baada ya kupata semina kuhusu LISHE
Hapa mtoa mada akiongea na wanasemina

SHULE ZETU

Kesho ni Jumatatu wanafunzi wanarudi shuleni kupambana na kitabu.Lakini kwa watoto kama hawa wa shule ya Awali huko Songea wanaenda shule ila mazingira ya usomaji hayaridhishi kabisa. Serikali tupieni macho haya mapungufu. Marekebisho yanawezekana na juhudi tu na kutilia mkazo uwajibikaji stahili.

KURUKA STEJI NDO MATATIZO YAKE HAYA

UAFRIKA RAHA....

Friday 19 September 2014

UTALII MWINGINE WATAKA MOYO

Hapa watalii wamejifungia kwenye gari kuwatazama simba. Kawaida tungetegemea simba hao ndo wawe kwenye uzio huo.

SCOTLAND KUENDELEA KUWA SEHEMU YA UNITED KINGDOM/UINGEREZA

Jana ilipigwa kura kwa wanaotaka Scotland kuwa Nchi yenye mamlaka kamili na sio kuwa mshirika wa UK pamoja na England na Wales. Hata hivyo 45% walitaka nchi hiyo ijitenge ila 55% wakataba ibaki sehemu ya UNITED KINGDOM. Kufuatia matokea hayo wengine wamelia na wengine wamefurahi huku Waziri Mkuu wa Scotland Mhe Alex Salmond kuamua kujiuzulu.
Chini ni Waziri Mkuu Mhe.Alex Salmond

UJASIRIAMALI: UWAJIBIKAJI NA KUJITUMA KUTABORESHA MAISHA

Moja ya maduka madogo ya maeneo ya vijijini na mtaani ambayo raia hujipatia mahitaji yao ya kila siku. Kuendelea kuwajibika,kutunza mtaji, kuboresha mauzo kutampelekea mjasiriamali huyu baadae kuwa na duka duka na hata Supermarket. KUMBUKA hata Mbuyu ulianza kama mchicha.

CHADEMA DUH

Thursday 18 September 2014

MAGAZETINI LEO

KUKOBOA MAHINDI KINYUMBANI NYUMBANI.

Raha ya nyumbani kila kitu kinapoandaliwa kiasilia
(Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog)

KWA HUYU PESA INA MATUMIZI MENGINEEEE

Maisha jamani kila mtu alivyoumbwa tu. Huyu mwenzetu pengine alipewa hizi dola ili akanunua mahitaji yake ila kwakuwa kwake hela sio kitu cha msingi basi anaitafutia matumizi katika ya mahitaji ya maisha yao ya kila siku.

KATIKA KUDHIBITI MAANDAMANO YA CHADEMA, ULINZI WA KUTOSHA

Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa Dodoma leo
Nako Jijini Dar hali ilikuwa Tete pale Kiongozi wa Juu CHADEMA alipokuwa anaingia Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mahojiano

USITUPE TAKA HOVYO