Tuesday 30 June 2015

WATANGAZA NIA CCM WALIORUDISHA FOMU LEO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati), akikabidhi fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Rajabu Luhavi alipozirejesha katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, baada ya kupata wadhamini wanaohitajika. Kulia ni Mkewe Mama Dorcas Membe
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein akionesha Fomu yake ya kugombea kwa Wanachama wake katika hafla ya kurejesha Fomu hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Afisi Kuu Kisiwandui. Picha na Makame Mshenga.
Nae waziri Mkuu Mizengo Pinda amerudisha fomu

IRENE UWOYA ATOKELEZEA KI-CCM

MHE LOWASSA AKAMILISHA ZOEZI LA KUTAFUTA WADHAMINI HUKO MOROGORO

Wakati huo huo inasemekana kuwa...Waziri Mkuu mstaafu, Monduli, Edward Lowassa ametajwa kuongoza katika kutaja vipaumbele vya maendeleo ikiwamo kupunguza tatizo la Ajira nchini na kuinua Elimu, miongoni mwa kundi la wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kadhalika, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa ndiye kiongozi wa siasa aliyeshuhudiwa na wananchi wengi katika hotuba zake kuliko wanasiasa wengine waliokwisha kutangaza nia.

Hayo yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Katerri, alisema ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka vijijini na mijini

Friday 26 June 2015

KUDUMISHA MILA

Mhe.Uhuru Kenyatta,Rais wa Jamhuri ya Kenya akila nyama choma. Hii ni alama ya kutumisha utamaduni wetu. Tusione aibu kudumisha mila njema tulizorithi kwa wazee wetu.
Wakati huo huo mtangaza nia ya Urais 2015 Mhe Edward Lowassa akipata nyama choma alipokuwa katika moja ya mizunguko yake kutafuta wadhamini.

MCHEPUKO SIO DILI

Tazama picha hii, ingekutokea wewe siku ya harusi yako ingekuwaje hapo? Sipati picha!!

Thursday 25 June 2015

MANDHARI SAFI: FAHARI YA BARA LA AFRIKA

WEMA SEPETU: "NAWEZA KUWA MBUNGE BORA"

Wema Sepetu ameeleza sababu 5 za yeye kuweza kuwa Mbunge bora kabisa baada ya kutangaza nia yake ya kutafuta nafasi hiyo ya uwakilishi kupitia CCM – Viti Maalum mkoani Singida. Zifuatazo ni sababu hizo 5:

1. Nina kipaji cha uongozi, kuanzia ngazi ya shule ya msingi, sekondari, chuoni, katika taji langu la Urembo na Majukumu kama Miss Tanzania na pia kama mfanyabiashara.

2. Niko karibu na wananchi wa rika zote, naelewa matatizo yao na nimekuwa tayari nikishiriki katika kuyatatua katika ngazi mbalimbali. Naweza kuwaleta watu pamoja.



3. Naamini katika dhana ya mwanamke anaweza, sio tu akiwezeshwa bali akiamua mwenyewe kwamba anaweza. Nia yangu ya kuwa Mbunge ni chachu kwa wasichana wengine kwamba wanaweza kufanya yale wanayotaka kwenye maisha na wakayafanya kwa ufanisi.



4. Mimi ni kijana na mbunifu pia. Shida nyingi za vijana kwa dunia ya leo zinahitaji ubunifu katika utatuzi. Mfano elimu ya ujasiriamali katika kupambana na ajira, afya ya uzazi katika kuweza kufanya shughuli zako vizuri, haki za wanawake ili waweze kushiriki katika kujenga nchi yetu, n.k. Nataka kupiga hatua zaidi katika kuchangia ubunifu wangu kutatua matatizo ya vijana katika uwanja mpana zaidi kwa kutumia ubunifu huo na exposure yangu ya ndani na nje ya nchi.



5. Naamini katika mabadiliko. Kwamba vijana lazima washiriki kujenga jamii wanayoitaka. Naona kuna mengi ambayo naweza kuchangia, mengi ambayo hayako sawa. Sioni sababu ya mimi kukaa pembeni na kusubiri mwingine abadili yale ninayotaka yabadilike wakati nina uwezo wa kufanya hivyo.

- See more at: http://patahabari.com/2015/06/24/wema-sepetu-sababu-5-kwa-nini-naweza-kuwa-mbunge-mzuri/#sthash.Hfb8rVIy.dpuf

Wednesday 24 June 2015

JE UNAONA TOFAUTI GANI KATIKA PICHA HIZI? tAZAMA UBEBAJI MABEGI/POCHI

Hapana chezea Diamond

AZAM MARINE WAINGIZA BOTI MPYA "KILIMANJARO V"

Baada ya kuingiza Boti ya Kilimanjaro IV ambayo imekuwa ni kivutio cha usafiri kati ya Zanzibar na Dar es Salaam, Kampuni ya Azam Marine ya mheshimiwa Bhakhresa sasa imeingiza Boti nyingine mpya KILIMANJARO V. Boti hiyo ya kisasa imeshushwa leo katika Bandari ya Zanzibar. Tazama picha nyingine hapa chini Boati hiyo ikiwa inashushwa ikitokea Australia. Tunapongeza Azam Marine kwa kuimarisha usafiri huu wa majini kati ya Tanzania Bara na Zanzibar
Imepewa kisifa :"Lady of Zanzibar"

Monday 22 June 2015

Sunday 21 June 2015

UKUMBI WA BUNGE DODOMA TUPU. KISA MBIO ZA URAIS

TASWIRA MBIO ZA URAIS 2015

TASWIRA YA TAZARA FLYOVER KATIKA VIDEO

Tazama hapa video ya namna Flyover ya Tazara itakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika/

HAPPY FATHER'S DAY

Siku hii itukumbushe kusaidiana majukumu pale inapowezekana sio kuachia malezi mtu mmoja katika familia. Hongereni kina baba wote mnaojitahidi katika hilo.

Mkazi wa Jiji la Dar es salaam, Saidi Mustafa.......akiendesha baiskeli huku akiwa amembeba mtoto wake Bakari, mgongoni mwake kama alivyokutwa na mpiga picha hii huko Kinondoni B, Jijini Dar es salaam. Baadhi ya akina Baba wanawajibika ipasavyo katika shughuli za Familia, tofauti na dhana iliyojengeka miongoni mwa Jamii (Picha hii hapa chini kwa hisani ya Fadhili Akida)

Saturday 20 June 2015

ACHA NICHEKE MIE....

Eti Gold digger teh teh

Friday 19 June 2015

MSHUKIWA WA MAUAJI YA WAUMINI 9 KANISANI HUKO MAREKANI APANDISHWA KIZIMBANI LEO

Mshukiwa wa mauaji ya kanisani nchini Marekani ameshtakiwa na mashtaka tisa ya mauaji
Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa la kihistoria la Kiafrika katika mji wa Charleston ameshtakiwa na mashtaka tisa ya mauaji pamoja na shtaka moja la kumiliki silaha, polisi wamesema.
Mshukiwa Dylan Roof mwenye umri wa miaka 21,anatarajiwa kufikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani baadaye hii leo kupitia teknolojia ya video.
Polisi wanayachukulia mauaji hayo katika kanisa la Emanuel AME siku ya jumatano usiku katika mji wa kusini mwa Carolina kama uhalifu wa chuki.
Alikamatwa siku iliofuata yapata maili 200 kutoka mji wa Carolina kazkazini kabla ya kusafirishwa na kurudishwa mjini Charleston.
Gavana wa jimbo la Carolina Kusini Nikki Haley amesema kuwa bwana Roof anapaswa kupewa adhabu ya kifo. CHANZO:BBC
Mtuhumiwa akionekana kwenye screen alipokuwa anasomewa mashtaka yake.
Baadhi ya waliouawa katika shambulizi hilo

RAIS KIKWETE ZIARANI INDIA

Mhe. Rais Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India mhe. Narendra Modi katika Ikulu ya India. Mhe Rais yupo India kwa ziara ya Kiserikali.

WEMA SEPETU HAKAMATIKI...MBIO ZA UBUNGE SINGIDA

MANENO KUNTUUUUUUUUUUU................................
Kama watu wanaogombea wako hivi kwanini Wema naye asigombee? Ukikubali kina fulani wagombee basi na kina fulani nao waachwe wagombee. Watanzania wakiwachagua wataishi na uchaguzi huo kwa miaka mitano. Kama ana mashabiki wake katika Bongo Movie na hata nje ya Bongo movie kwanini asigombee?

SIO RAHISI KIHIVYOOOOO.

Mambo ya copy and paste

NAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Kwa Wapendwa Waislamu wote, nawatakia mfungo mwema.

Thursday 18 June 2015

NMB YAZINDUA MASTERCARD

Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro.
Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam .

Wednesday 17 June 2015

WEMA SEPETU AJITOSHA KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA

Star wa Bongo Movie Wema sepetu amemamua kujitokeza adharani na kutangaza nia yake ya kutaka kugombea Ubunge viti maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM mkoani Singida ambapo ndio nyumbani kwao...
Wema amesema kwasasa anahitaji Dua zenu pamoja na nguvu yenu kwan yeye mara nyingi amekuwa akiwapa nguvu watu wanaohitaji msaada kutoka kwake sasa ni zamu yake kuwaomba watanzania wamuunge mkono kufikia malengo yake