Saturday 28 February 2015

KAPTAIN KOMBA AFARIKI DUNIA

Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mkurugenzi wa TOT Band, Captain John Komba amefariki jioni hii katika Hospitali ya TMJ jijini Dar. Mipango zaidi mtajulishwa baadae. MUNGU AIPOKEE ROHO YAKE PEMA AMEN.

KAMATI KUU YA CCM WAKUTANA DAR LEO

Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM Ikulu Jijini Dar

ONYESHA UPENDO


KIVUKO CHA MV DAR ES SALAAM CHAFANYIWA UZINDUZI-MAJARIBIO

Kivuko hiki ambacho kiliingizwa nchini mwishoni mwaka jana kitakuwa kinafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo.
Mhe.Waziri wa Ujenzi John Magufuli akiwa katika kivuko hicho katika safari ya majaribio kwenda Bagamoyo

Friday 27 February 2015

KUMBUKUMBU YA VITA YA KAGERA

Amiri Jeshi Mkuu wakati huo Hayati Mwl.Julius K.Nyerere akijadiliana jambo na wakuu wa Jeshi kuhusu uvamizi wa Nduli Idd Amin katika sehemu ya Tanzania huko Bukoba. Vita hivyo vilianza rasmi tarehe 30-Oct-1978 na iliisha rasmi tarehe 11-Apr-1979 (miezi mi-5, wiki 1 na siku 5)

MAGAZETINI LEO

Milioni 10 kununua mboga, hii sasa ni dharau

HUU SASA NI UTUMWA

Hawa ni Tour Guides wakiwa wamewabeba watalii. Jamani hata kama ni kutafuta pesa si mtindo huu sasa tutarudi kule kule enzi ya utumwa. Haipendezi.
(Picha na maelezo kwa hisani ya DJ.SEK BLOG)

NDIO MAANA TUNASEMA SHULE MUHIMU

ASILI YAKE AFRIKA

Thursday 26 February 2015

Mhe.CHENGE NA SAKATA LA ESCROW

KWA WATUMIAJI WA USAFIRI WA TRENI YA JIJINI DAR........

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya treni ya Jiji kuanzia leo Jumatano jioni Februari 25 hadi Jumatatgu Machi 02, 2015 itakapoanza tena.

Kwa mujibu wa taarifa ya Uongozi wa TRL iliotolewa jioni leo Februari 25, 2015 uamuzi wa kusitisha huduma hiyo umesababishwa na vichwa viwili vya treni hiyo kuharibika na kuhitaji matengenezo makubwa katika Karakana Kuu ya Morogoro .

Taarifa imefafanua kuwa kwa vile kimebaki kichwa kimoja huduma hiyo haiwezi kuendelea hadi vichwa hivyo viwili vitakapo maliza kukarabatiwa siku ya Jumamosi huko Morogoro.

Kwa kawaida treni ya Jiji hutumia vichwa viwili wakati inapotoa huduma kati ya stesheni za Ubungo Maziwa na Stesheni kuu ya Dar, wakati kile cha tatu huwa cha akiba endapo dharura itakipata kichwa kimoja wapo wakati huduma inaendelea.

Aidha Uongozi wa TRL unawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa jumla hasa wa eneo la Jiji waliokuwa wamezoeya kupata huduma hiyo kila siku kwa usumbufu utakajiotekeza .

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Februari 25, 2015

*** (Picha na habari kwa hisani ya Michuzi Blog) ***

MAMBO YA JOTI

Joti (Lucas Mhuvile) kaamua kutoka kihivi leo.

KATUNI YA LEO

Wednesday 25 February 2015

MAISHA JAMANI MAISHA

Huwezi amini hata baada ya kupigana sana kupunguza hali ngumu kwa Watanzania ili waweze pata maisha bora kila mtanzania, bado kwa wengine huu ni msamiati. Hata wembe au mkasi tu wa kunyolea ni shidaaa. Ila tusikate tamaa tuendelee kujitahidi itawezekana.
Nae huyu naona ana ndoto nzuri ya kuwa mmiliki wa gari au labda dereva wa gari fulani. Kasome utimize ndogo yako sasa.

MKUU MPYA WA WILIYA YA KINONDONI AANZA KAZI

Mhe Paul Makonda,Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni ameanza kazi baada ya kuapishwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadiki. Amesisitiza kuwa atatimiza majukumu yake kwa kufuata alichokiita STK( Sheria, Taratibu na Kanuni) na kwamba anafanya kazi ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Wilaya alopangiwa.
Mhe. Makonda akitia sahihi kiapo tayari kuanza kazi kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Mhe.Rais Kikwete akisalimiana na Mhe.Paul Makonda huko katika Shule ya Msingi Kunduchi ambapo mhe Rais alikwenda kukagua Maabara pamoja na kugawa vitabu vya Sayansi vilivyochapishwa kwa Msaada wa Watu wa Marekani.

Tuesday 24 February 2015

MAPENZI NA SIMU: KAWIVU KIDOGO LAZIMA KAWEPO

"Sijui anachat na nani huyu tena, ngoja nipige chabo" Ni kama vile maneno hayo yapo moyoni kwa Diamond akitupia jicho simu ya mpenzi wake 'The Lady Boss' Zari

Monday 23 February 2015

KUMEKUCHA KILA MMOJA AKIJARIBU KUWAHI RIZIKI

Mwanzo wa juma ndo umeanza,likiwa ni juma la mwisho la mwezi Februari. Nawatakia nyote mafanikio katika kile unachoshughulika nacho kihalali wiki hii.

Sunday 22 February 2015

TULIPOTOKA NA TULIPO: USAFIRI WA NDEGE TANZANIA


Boeing 737-2R8C Iliyopewa jina Kilimanjaro ikiwa katika huduma mwaka 1978

Boeing 707-320 Iliyopewa jina la "Ngorongoro Crater" ikiwa katika uwanja wa ndege wa Zurich huko Uswisi katika moja ya safari zake mwaka 1980
Boeing 737-236 Baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na Shirika la ndege la Afrika ya Kusini na kuzindua ndege hii mwaka 2002
Airbus A320-214.Shirika hilo likaendelea tena kushirikiana na Afrika Kusini lakini kipindi hiki rangi ya ndege zake ikabadilishwa tena
The De Havilland Canada DHC-8Q-311 DASH 8 5H-MWG Baada ya kukumbwa na madeni na matatizo mengine ya ndani ya Shirika, ATCL ikajikuta inabakiwa na ndege hii ambayo iliingizwa Novemba 2012 kufanya safari za ndani kati ya Dar-Tabora-Kigoma.

Baada ya kufunguliwa kwa Uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya, shirika hili limekodisha ndege kutoka Shirika la ndege la Kenya kuhudumia.

NB>:Ila tunachojiuliza imekuwaje maana Shirika hili miaka ya 70 na 80 ilikuwa inatoa huduma nzuri sana za ndani na nje ikihudumia kutoka Dar es Salaam to Athens (707),
Antanarivo (737), Bombay (707) Bujumbura (737, Cairo (707), Frankfurt (707), Kigali (737), London-xx Gatwick (707), Mahe(737), Maputo (737), Mauritius (737), Moroni (FKF), Muscat (737) and Rome (707).
Nembo na rangi vimebadilika nadhani kwa mawazo yangu ya zamani iliwakilisha vizuri Tanzania kuliko sasa

LISEMAVYO MWANANCHI

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Ujumbe huu ungekuwa unamhusu binadamu ingefurahisha kuliko kuandikwa tu kwenye Daladala.Ni muhimu kusafisha maisha yetu kwa matendo mema ili Mungu azidi kutubariki na kufanya makazi pamoja nasi. Usidharau nafasi ya Mungu katika maisha yako mpendwa Mdau.

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wasikilize na kufuata
mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini ili Tanzania iwe nchi
yenye watu waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Februari 20, 2015) wakati
akizungumza na maelfu ya waumini na wananchi waliohudhuria ibada ya
mazishi ya Askofu Mstaafu Magnus Mwalunyungu kwenye kanisa la Moyo
Mtakatifu wa Yesu la Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa.
“Leo ni siku ya pekee ya kuwasikiliza viongozi wa dini wakituasa
tujiandae kwa maisha baada ya kifo. Tukio hili la leo litupe nguvu ya
kukubali kwamba kifo kipo licha ya kuwa hakizoeleki na kinapotokea
kinaleta simanzi kubwa,” alisema.

Saturday 21 February 2015

NASEMA KWA SAUTI........................................

WAKATI MWINGINE TUWAPIME AKILI MADREVA HAWA

Hata kama ni suala zima la kutafuta hela na kuboresha maisha, lakini busara na uhakika wa jambo unalofanya ni muhimu kuzingatiwa.

MAISHA

Wakati wengine wanakula na kusaza, wengine wanakufa kwa njaa. Think twice!

MHE.RAIS KIKWETE MWENYEKITI MPYA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Mhe Rais Jakaya Kikwete akipokea bendera ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutoka kwa Mhe. Raisi Uhuru Kenyatta wa Kenya kama ishara ya kuwa mwenyekiti mypa wa Jumuiya hiyo katika Mkutano wa 16 huko KICC Kenya.
Viongozi Maraisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika mazungumzo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha 16 cha Jumuiya hiyo