Tuesday 31 March 2015

UCHAGUZI WA RAIS NIGERIA: Muhammadu Buhari AONYESHA KUONGOZA KURA

Wananchi wa nchi ya Nigeria wamepiga kura jumamosi na jpili wiki ilopita kumchagua raisi wa nchi yao. Waliokuwa na uvutano mgumu ni Rais wa sasa Goodluck Jonathan na mpinzani wake Muhammadu Buhari. Mpaka sasa matokeo ya awali yanaonyesha Mhe. Muhammadu Buhari "ex soldier" anaongoza.
Mhe. Muhammadu Buhari anayechukua nafasi kubwa kushinda uchaguzi wa Uraisi Nigeria

MICHEZO YA WATOTO INAYOKUZA UMOJA NA UPENDO

Michezo kama hii ya watoto katika baadhi ya jamii zetu hasa waliotawaliwa na utandawazi wanaiona kama upuuzi. Lakini Michezo hii inakuza akili, inaburudisha, inaleta umoja na upendo kutokana na wanavyoshirikiana katika kucheza. Tujitahidi kuwapa moyo watoto wetu wapende michezo sio kutwa kukaa wakiangalia TV.

MHE. RAIS KIKWETE SAFARINI MAREKANI

Mhe. Rais Kikwete amewasili nchini Marekani kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Mwonekano wa Jengo hilo

Monday 30 March 2015

KUFUATIA SAKATA LA ASKOFU GWAJIMA....

Mhashamu Polycarp Kardinal Pengo atoa msamaha

Sunday 29 March 2015

WIKI YA MWISHO WA MWEZI

Ikiwa ni jumatatu ya mwisho kwa mwezi huu wa Machi, pilika zimeanza. Wengi wiki hii wakijiandaa kwa manunuzi kabla ya sikukuu ya Pasaka. Nawatakia utafutaji mwema. Hakuna kukata tamaa katika kutafuta riziki hata iwe unakumbana na adha kiasi gani.

NAWATAKIA JUMAPILI YA MATAWI NJEMA

Kwa wale Wakristo, jumapili ya leo ni adhimisho la Jumapili ya Matawi kukumbuka Yesu alipoingia Jerusalem kwa shangwe kabla ya kuteswa kufa na kufufuka. Ni wiki ya maadhimisho makuu kuelekea Pasaka.

Friday 27 March 2015

UTOTO RAHA

UMUHIMU WA KUWA MAKINI UNAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO

Ina maana madreva hawa hawapo makini katika makutani ya reli na Barabara au ni dharau???
Lori la Mizigo lilipoiginga Treni karibu na Machinga Compelex Jijini Dar leo.

KWA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU (FOOTBALL)

HIZI LIFT JAMANI....

Unapompa mtu lift kwenye gari lako ni kitendo cha huruma na kawaida ukarimu wa kitanzania, lakini uwe makini kuangali kama abiria wako uliyempa lift amefunga mkanda vizuri, wengine hawajui na hivyo unapomwambia "Funga mkanda" unaeza shangaa mtu amejinyonga ukapata "murder case bure"

KIBONZO CHA LEO: HAPO ABIRIA ROHO MKONONI

HAPO VIPI....?

Taswira hii imechukuliwa kwa jirani zetu Uganda.

MHE. RAIS KIKWETE ATEUA WABUNGE WAWILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.
Rais amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.
Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
- Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
- Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
- Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
- Mhe. Janet Zebedayo Mbene
- Mhe. Saada Salum Mkuya
- Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
- Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
- Mhe. James Fransis Mbatia
Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi, 2015.

Thursday 26 March 2015

UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO NA YA JAMII

Pamoja na kwamba baadhi ya watu wamejiingiza katika uvutaji wa sigara kama mojawapo ya starehe zao, lakini utafiti wa kitaalamu unaonyesha kuwa Uvutaji wa sigari ni hatari kwa afya yako (Huaribu mapafu) pia ni hatari kwa jamii inayokuzunguka. Ni muhimu kuchukua hatua za kuacha. Serikali inaongeza juhudi za kuzuia uvutaji wa sigara katika mikusanyiko ya watu/hadharani (Public areas)

Wednesday 25 March 2015

AJALI MBAYA YA NDEGE YA UJERUMANI


Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Dusseldorf-Ujerumani.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.
Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.

KUSAKA MAISHA

amoja na kujitahidi kusaka maisha, ila pia tunapotumia vifaa hivi tutazamame na usalama wa maisha yetu.

HAPA HAKUNA LELE MAMA

Hiyo ndo inayoitwa...Heshimaaaaaa TOA!


KATIKA HATUA NYINGINE........
Rais Jakaya Kikwete amelikata Jeshi la Polisi nchini kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wapigakura, upigaji Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.
Akifunga mafunzo ya maofisa warakibu wasaidizi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema dalili zinaonyesha kwamba kuna watu wenye nia ya kuhatarisha amani katika matukio hayo.
"Tunayoyasikia na tunayoyaona yanaashiria kuwapo kwa dalili za wenzetu kukwamisha shughuli hizi za kitaifa kwa kufanya vurugu, Jeshi la Polisi jiandaeni na vitendo vyote vitakavyofanywa kwa lengo la kuhatarisha amani," alisema akijibu maombi ya kupatiwa vifaa yaliyowasilishwa kwake na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride maalumu wakati wa hafla ya kuwatunukia vyeo maofisa 289 wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam

Tuesday 24 March 2015

KIBONZO CHA LEO

KERO YA MVUA ZAINAZONYESHA JIJINI DAR NA KWINGINEKO NCHINI

(Picha ya juu kwa hisani ya Global Publishers)
HALI ni tete katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na mvua ya masika iliyonyeshwa kwa siku tatu na kusababisha vifo vya watu watano, huku nyumba nyingi zikiwa zimezingirwa na maji. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Buguruni kwa Mnyamani na eneo la Jangwani katika Manispaa ya Ilala, ambako nyumba nyingi na barabara zimeathirika.
Sehemu nyingi na barabara nyingi zinapitika kwa taabu
Mto msimbazi nao umefurika
Maeneo mengi utata mtupu

Monday 23 March 2015

KUMBUKUMBU

Mmiliki wa Blog hii anaungana na familia na Ukoo wa Mwangoka kumkumbuka Baba Mzazi Mzee Amedeus Mwangoka aliyetutoka tar.23.03.2009 siku ya Jumatatu kama leo katika Hospitali ya Kibosho-Moshi. Tulikupenda sana Baba na kamwe hatutasahau busara zako na uchapakazi wako makini kutuwezesha wanao kuishi,kusoma na kukua kiroho na kimwili. Pengo lako kamwe halitazibika. Tunakuahidi kukuenzi kwa kuishi tunu zako. Tunakuombea Mungu akupumzishe palipo pema mbinguni. Tutakukumbuka daima Baba yetu. "Bwana alitoa na Bwana ametwaa,Jina la Bwana lihimidiwe" Amen.
Mzee Amedeus Mwangoka enzi za uhai wake huko nyumbani kwake Sanya Juu-Kilimanjaro
Taswira ya Mwana Karibu Nyumbani (Mtoto wa tatu wa marehemu) siku ya mazishi

Sunday 22 March 2015

MGOGORO WA MAGARI YA KITALII NA SAFARI ZA NDEGE KATI YA KENYA NA TANZANIA WATATULIWA

Imekubaliwa sasa kuwa ni ruksa magari ya kubeba watalii kutoka Tanzania kuingia katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta, ambapo hapo awali walizuiwa. Pia safari za Ndege la Shirika la ndege la Kenya Airways zimerudishwa kama mwanzo 42 kwa wiki. Makubaliano haya yamefikiwa na Maraisi wa nchi hizi mbili katika kikao cha dharura walichofanya huko Windhoek Namibia walipoenda kuhudhuria sherehe za miaka 25 ya Uhuru na pia kuapishwa Rais mpya wa 3 wa nchi hiyo.
Maraisi Mhe Uhuru Kenyatta (Kenya) na Mhe.Jakaya Kikwete (Tanzania) wakiwa katika kikao cha dharura kutatua mgogoro huu huko katika Hotel ya Safari Court jijini Windhoek,Namibia.

ZITTO HUYOOOOOOO....ACT

Baada ya kujiengua rasmi kutoka CHADEMA wiki ilopita, mhe.Zitto aonekana kuingia rasmi ACT.

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA WADAU WANGU

Saturday 21 March 2015

ASEMAVYO KINGWENDU

TAHADHARI MVUA UKANDA WA PWANI YA NCHI

DAR MVUA KIDOGO TU SHEEEEDAH

Eneo la Magomeni Mikumi karibu na Hotel Travetine, mvua hii ya muda mfupi maji yamejaa barabarani
Nako mitaani hali ndo mbaya zaidi
Na usiombe Ukosane na Mama mwenye nyumba kipindi kama hiki akutolee vitu nje kama hivi na mvua ikukute nje

KUTOKA MAGAZETINI

Habari kubwa zilizotawala ni kuhusu Mhe Zitto Kabwe
Mengine

MAENDELEO SEKTA YA BARABARA.

Mfano wa barabara zitakayokuwa katika makutano ya TAZARA jijini Dar. Mradi huu wa ujenzi unatarajiwa kuanza Mei 2015
Picha na mradi huu ni kwa hisani ya watu wa Japan kupitia shirika lao la JICA

Friday 20 March 2015

MHE ZITO KABWE AAGA RASMI BUNGENI


Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe usiku huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba anategemea kuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo inaandaliwa. Kaa chonjo...
Mhe Zito Kabwe akisoma barua aliyomwandikia Mhe.Spika wa Bunge kuhusu kung'atuka kwake Ubunge.

MAELEZO BINAFSI YA MHE.docx