Sunday 16 August 2009

HII SASA AIBU NYUMBANI ,KISA "UFISADI"

Wadau vita vyetu dhidi ya ufisadi lazima viendelee, hebu someni hii barua hapa chini. Mzungu analia kweli kweli
Subject: FW: RE: MY NIGHTMARE IN TANZANIA
Date: Tue, 4 Aug 2009 15:04:53 -0400
From: Ray Bergen
To: Lisana Koliskowski
Hello Lisa
I am glad to be back in America after such a disastrous trip to Tanzania. The most important thing was getting back home safely and seeing my family. The only thing I can assure you is that, I will never set my foot in that country, and will advice anybody planning to visit Tanzania to refrain from doing so. The nightmare started at the airport, when my luggage checked in from Amsterdam disappeared mysteriously in Dar es Salaam. And my inquiry with the airport authorities was forwarded to the police. At the police station (Central) I was told that I could not get help unless I bribe them $500, because they needed the money for fuel and other necessary needs to investigate the theft. Supposedly the police officer did not open the case and turned me to be the criminal, constantly coming to my Hotel room, asking me for money. In short all my four year work was lost with the laptop at the Airport.

Came clearing the vehicle we were supposed to use in the research, from the agents to the customs authorities, the vehicle exceeded the actual cost. I would have paid $38,000 for a $16,000 vehicle. I could not bear being in such a corrupt country and decided to terminate my research, and left the vehicle uncleared after one month of struggle with the customs, who needed money after money and bogus letters. Supposedly these exuberant fees were not supposed to be there in the first place, because all registered NGO’s are supposed to be exempted from paying these taxes and fees, but then the deal had been cooked to rip Muzungu off. Being a Muzungu is being a cash cow in Tanzania.. They don’t even fucken know that we are trying to help them. I pity the African continent and her people, I am glad they did not confuse me with Albino

Please advise any potential traveler to Tanzania to look for alternative country to visit, and if possible pass the message to the State Department as a warning to other Americans intending to visit this poor and corrupt country. I visited Botswana with my family in 2006. I tell you, could not be more satisfied with their politeness and straightforwardness , the same was in Mozambique where we received utmost hospitality.
Please, be careful and only travel to Tanzania when there is need and not to visit and do not carry any valuable. As soon as you arrive, register with the American Embassy

Sincerely,

Ray Bergen.

Kwa Kiswahili


Nafurahi kurudi nyumbani Marekani baada ya safari yangu ya mkosi ya kwenda Tanzania. Kitu cha muhimu ni kwamba nimerudi nyumbani salama kujumuika na familia yangu .Kwa kweli sitakaa nikanyage tena ardhi ya Tanzania na nitamshauri mtu yeyote yule ambaye anataka kwenda Tanzania afikirie mara kadhaa uamuzi wake huo wa kwenda Tanzania.

Kizaazaa kilianzia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere pale begi langu lililofanyiwa ukaguzi wa kina Amsterdam, Uholanzi kutoweka kimiugiza. Nilijaribu kufuatilia kwa utawala husika wa pale Uwanjani lakini walinielekeza kwenda Kituo cha polisi cha Kati ambapo nao walihitaji niwape hongo ya dola za kimarekani 500 ili waweze kunipa msaada.
Hizo dola 500 waliniambia ni kwa ajili ya kununulia mafuta ya gari na nyingine ni za kununulia vitu muhimu vya kufanyia upelelezi. Cha kushangaza ni kwamba ofisa wa polisi hakufungua kesi ya wizi bali alianza kunifanya mimi kama mhalifu kwa kuja hotelini kutaka nimpe pesa. Kwa kifupi nilipoteza laptop yangu ambayo ilikuwa na kazi ambazo nilizifanya kwa miaka takribani minne.

Tuje kwa upande wa kufanyia usajili gari la Asasi isiyo ya kiserekali (NGO), walitaka nitoe dola 38000 kwa gari lenye thamani ya dola 16000 tu. Sikuta ka kuhatarisha gharama zangu za kufanya utafiti kwa sababu ya umaskini na ufisadi wao ilibidi niache usajili wa gari baada ya usumbufu wa mwezi mmoja kwa sababu kila ulipoenda walikuwa wanataka rushwa kwa sababu mimi ni Mzungu na bila ya kujua kuwa nilikuwa pale kufanya utafiti wa kuwasaidia wao. Yaani kuwa mzungu niligeuka kuwa mtaji na namshukuru Mungu kwa sababu hawakunifananisha na albino.

Tafadhali watahadharishe watu wote wenye kipaumbele wenye mpango wa kwenda Tanzania tena ikiwezekana fikisha ujumbe huu kwa idara zote za Umma wa Marekani kama kuwaonya Wamerekani wote wenye mpango wa kwenda nchi hiyo maskini naya kifisadi.

Nilitembelea Botswana mwaka 2006 na nilifurahishwa na ukarimu pamoja na uwezo wao wa kufanya mambo kwa uwazi kabisa. Vilevile nilitembelea Msumbiji ambao pia walinitunza vizuri. Nawasihi mwende Tanzania wakati kukiwa na ulazima tu na usiende na vitu vya thamani na ukifika tafadhali jiandikishe kwenye ubalozi wa Marekani.

Wako mwaminifu, Ray Bergen

Imetafisiriwa na Godlisten N. Shao

1 comment:

  1. Hii nimeisoma kuleeee kwingine na kuona MAONI ya wadau. Wengi wametofautiana kuhusu hili. Wapo wanaoona kuwa huyu asemaye anasema ukweli na wengine wanamponda wakisema hafanyi la maana. Lakini kwangu haijalishi kama hii hadithi imetungwa ama la. Mimi nilikuwa mmoja wa wahanga wa tukio lililofanana na hili.
    Na tumesoma malalamiko meengi kuhusu suala kama hili. Ninashangaa kuona serikali inaweza kumpeleka naibu waziri kumpokea msanii ama mchezaji maarufu lakini ikashindwa kutuma japo mwakilishi kuangalia malalamiko ya namna hii ambayo TUMEYAWAKILISHA SAAAAAANA.
    Siku yaja na tutapata suluhisho KAMA TUTAAMUA
    Blessings

    ReplyDelete

Maoni yako