Saturday 19 December 2009

MFULULIZO WA MARAHA KUELEKEA XMAS NA MWAKA MPYA


Ndafu wa nguvu

Kumbi zilizopambwa zikapambika

Mwanamama Tshalla Muana stejini

JB Mpiana na jopo zima

Saturday 19 September 2009

SAFARINI

Kumradhi wadau, nilipata safari ya ghafla kuelekea Kijijini kwa Bibi na Babu kuhani msiba wa Baba yangu mzazi, na mtandao huku hakuna kabisa. Muda mfupi ujao nitarudi na kuwaletea yaliyojiri.
Salaam kutoka Kijijini

Tuesday 1 September 2009

KOMOA UKOMOLEWE ! au BILA BILA!

KARIBU DAR ES SALAAM ZOO

Watanzania wenzangu,kumbe kuna fahari yetu imejisimika ndani ya DAR ES SALAAM ZOO, tujongee tukajionee wenyewe kama kwenda Serengeti au Ngorongoro ni Mbali, basi hapa patakidhi haja yako.
Taarifa hizi ni kwa hisani ya:
www.daressalaamzoo.com na Michuzi

Monday 31 August 2009

MASANJA WA ORIJINO KOMEDI KWENYE BLOG

Masanja nae kaibuka kwenye blog na amekuja na kitu kinaenda kwa jina la
www.mkandamizaji.blogspot.com
Karibuni wadau kwenye kiwanja kipya hicho.

MWISHO WA MWEZI

Mwisho wa mwezi umewadia, tunapoganga yaliyopita,pengine picha hii inaweza kukukumbusha mengi. Zingatia kusamehe waliochukizwa na mafanikio yako, na jitahidi kuimarisha mafanikio uliyopata mwezi mzima,na yawe kichocheo cha mwezi ujao. Jitahidi kupunguza wakuchukiao kwa kuwa "mtu wa watu", na pengine kwa kuweka mipaka.
Nawatakieni nyote Mwisho mwema wa mwezi na mwanzo mwema wa wiki.

Sunday 30 August 2009

WADAU NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA

"Bila msaada wa Bwana ,kazi zenu ni bure....." Tujitahidi kumweka Mungu mbele katika yote nae atatujalia yale tuyahitajio. Ni siku nyingine ya kumsifu yeye kwa namna ya pekee, tuitumie vema. Pia ni wakati wa mapumziko kwa wengine, basi mapumziko mema.

Punda afe,mzigo ufike!!

Saturday 29 August 2009

NOTI MPYA YA SHILINGI 2,000



BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa noti mpya za Sh2,000 ambazo zitatumika sanjari na zilizopo kwenye mzunguko kwa sasa.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba, lengo la kutoa noti hizo mpya ni kukidhi mahitaji yake kwenye mzunguko wa fedha nchini.
"Noti hizi mpya zinatofauti moja tu na zile ambazo zimo kwenye mzunguko kwa sasa nayo ni saini zilizopo.

Saini zilizopo kwenye noti mpya ni za Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania,” alisema.
Profesa Ndulu alisema kuwa noti hizo bado zina rangi ya kahawia, zikiwa na michoro inayoonyesha mandhari ya kitanzania kiuchumi, kiutamaduni pamoja na urithi wetu na mazingira.

"Mbele ya noti, bado kuna picha inayoonyesha utajiri wetu wa kuwa na mojawapo ya wanyama pori wakubwa yaani simba ,alama ya kificho ya twiga ambayo bado ipo kama ilivyo katika noti nyingine zinazozunguka sasa" lilifafanua tangazo hilo.
Alama nyingine zilizopo katika noti hiyo ambazo hazina tofauti na iliyopo kwenye mzunguko ni nyuma ya noti kuna picha inayoonyesha picha ya ngome kongwe illiyopo Forodhani jijini Zanzibar.

Vile vile, alisema zina picha ya kinyago cha kuchonga na alama ya usalama inayobadilika rangi ikigeuzwa.
”Benki kuu inawashauri wananchi kuwa hakuna haja ya kubadili noti hizo kwani thamani yake ni ileile na kwamba haina mpango wa kuzifuta zilizokuwepo katika mzunguko wa awali.

Habari imeandikwa na Burhani Yakub wa gazeti la Mwananchi.

ASILI YETU ZAMANI HIZO

LOH, KUMBE NA SISI TUNA VIFAA!!

Hivi na vingine vingi vilionyeshwa siku ya Maadhimisho ya Miaka 45 ya JWTZ


BARABARA ZETU NA ADHA YA USAFIRI

Friday 28 August 2009

USALAMA WA MABASI YA ABIRIA:Yote kufungwa mikanda




Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kombe alisema suala la kufunga mikanda katika mabasi sio jambo la hiari na halina mjadala ni wajibu wa kila mmiliki wa basi kuhakikisha anatekeleza agizo hilo kwani ni moja ya sheria za usalama barabarani nchini.
Alisema ifikapo Oktoba mosi basi ambalo litakuwa halijatekeleza agizo hilo litakamatwa na askari na kupelekwa mahakamani pamoja na kulizuia kuendelea kufanya kazi hiyo ya kusafirisha abiria.
Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na mabasi ambayo hayatatekeleza agizo hilo na watapewa adhabu kali kwa kudharau agizo hilo.

Amesema lengo la agizo hilo ni kukabiliana na ajali za barabarani zimalizike ama zitoweke kabisa na kila basi linatakiwa liwe na cheses nzuri, na mikanda ya kuvaa abiria wanapokaa kwenye siti kwa kuwa abiria wamekuwa wakijeruhiwa na kufa kwa kukosekana kwa mikanda hiyo

MUITE AKUPAMBIE NA KUIPENDEZESHA SHEREHE YAKO

Sherehe za kisasa na wataalamu wa kisasa. Mualike Mpendwa huyu akufanikishie shehere yako kwa mapambo ya kisasa kabisa. Mtembelee katika Blog yake ujionee mwenyewe
www.poshweddings-tz.blogspot.com

WEEKEND HODIIIIII

Hodi wenyewe, mpoooo?

Thursday 27 August 2009

UREMBO WAHITAJI UVUMILIVU SANA

Kinadada wanapenda sana urembo ikiwa ni mojawapo na kusuka nywele. Kuna mtindo wa ususi wa nywele unaopendwa sana, ila wasusi wake maarufu ni jamii ya Kimasai. Style hii ya ususi inawataka kinadada hawa wakae kitako muda mrefu na ili kazi hii iweze kuisha mapema kidogo inabidi wasusi wawe wawili. Hapa dada huyu anachoka kukaa,kuinamisha shingo na kuna mengine kama "kajismell" toka kwa hawa jamaa na pengine pia suala la "mfadhaiko". Hongera kinadada kwa uvumilivu wenu.

Wednesday 26 August 2009

UBUNIFU

NANI ALAUMIWE?

Wadau,leo ngoja niongelee tabia ya "KULALAMIKA" bila kuchunguza zaidi nani wa kulalamikiwa na nini sababu ya kulalamika.
Katika picha hizi mbili hapa chini:


Mama huyu mfanyabiashara wa khanga na vitenge,ameuchapa usingizi katika eneo la biashara yake. Si ajabu mwisho wa siku akifanya mahesabu ya mapato yake kwa siku ataanza kulalamika "oooh siku hizi wateja hakuna, biashara haichanganyi, Rais hatuangalii watu wake,viongozi wazembe, njaa sana,nchi ya tabu sana hii" na maneno mengine kama hayo. Lakini sidhani kama katika tathmini yake ya kufanya biashara alizingatia vigezo ya biashara. Kwa mfano,mazingira anapofanyia biashara pana mwelekeo wa kuvuta wateja?, kauli yake kwa wateja je?, bei za bidhaa?, aina za bidhaa na mengine kama hayo. Zaidi sasa tunapoangalia picha hii, ni ukweli kwamba sidhani kama wateja watavutwa kuja kununua kitu kwako wakati wewe umelala, muda utakaotumia kuamka, kujiweka sawa na kuanza kuhudumia mteje tayari atakuwa keshakereka. Tusibaki tunalaumu tu,tuangalie hayo.


Katika picha hii nayo tunamwona jamaa huyu,yaonekana nae ni mfanyabiashara au mfanyakazi katika gari. Yeye kaona sehemu ya kupumzikia ni chini ya gari, tena gari lenyewe laonekana halina break imara ndio maana wameweka jiwe karibu na tairi.Lakini kiutaalamu uzito/egemeo la gari na uzito/egemeo la hilo jiwe haviendani. Hapo atakuwa amelalamika weeeeee kwamba hali ya maisha ngumu hadi amepata usingizi. Kwa mfano kama ni gari la kubeba mchanga hata mteja akija na kukuta amelala hivyo ni vigumu sana kumwamsha maana mteja unapokuja unategemea upokelewe kwa shangwe na maneno ya mvuto,"Mteja ni Mfalme" Halafu pia kwa bahati mbaya likitokea la kutokea labda gari limebiringika,ndio kusema hapo lazima watu waandae nyimbo za maombolezo.

Haya na mengine mengi ni ya kuangalia badala ya kulalamika tu.
Picha kwa hisani ya www.samvande.blogspot.com

Tuesday 25 August 2009

TASWIRA NZURI ZA UWANJA WA TAIFA

Kwa taswira hizi, ni wazi na sisi twaweza kujivunia sasa.

HII KALI ZAIDI

"Mwili haujengwi kwa matofali"
Pengine na watoto hawa wanajiuliza kama nao wakikua watamfikia huyu ndugu teh teh teh

HODIIIIIIIIIIIIIIIIII

Karibuni katika kibaraza murua cha kupata taarifa cha www.saluya44.blogspot.com

Monday 24 August 2009

NAWATAKIENI WIKI NJEMA

Ni jumatatu tena,mwanzo wa pilikapilika za juma. Nae mwanamama huyu yupo katika pitapita za kutafuta maisha. Jua ni kali na maisha ndio hivyo tena.Kizuri ni kwamba anamjali sana mwanae hadi anatafuta namna ya kumkinga na jua. Hongereni kinamama kwa malezi na matunzo sahihi.Tuongeze bidii katika majukumu yetu,maisha yataboreka tu japo si kwa siku moja.
Wakati kila mmoja akiwa anajibiidisha kutafuta riziki, Mwombaji Maarufu Mzee Matonya ambaye aliondolewa jijini Dar,sasa kahamia katika mitaa ya Mji wa Morogoro akiendelea na mbinu yake ya kutafuta pesa ili kusukuma gurudumu la maisha.

Sunday 23 August 2009

MISS UNIVERSE 2009

Mrembo wa dunia kwa mwaka 2009 anatoka Venezuela kwa mara nyingine. Huyu ni Stefania Fernandez.Mwaka jana 2008 Mrembo wa Dunia alikuwa Dayana Mendoza nae pia kutoka Venezuela.Mrembo wetu Illuminata kwa bahati mbaya hata kwenye 15 bora hakuwepo lakini,labda bado wakati wa kuwapta warembo kutoka Tanzania japo ni warembo sana.
Miss Universe 2009 Stefania Fernandez

Miss Universe 2008 Dayana Mendoza

MOTO WATEKETEZA BWENI IRINGA


BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA IDODI YA MKOANI IRINGA, LIMETEKETEA KWA MOTO NA WANAFAUNZI WAPATAO 14 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA TUKIO HILO LILILOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO. KWA MUJIBU WA MWANDISHI WETU ALIYEFIKA ENEO LA TUKIO, AJALI HIYO ILISABABISHWA NA MSHUMAA AMBAO ULIWASHWA NA MWANAFUNZI MMOJA ALIYEKUWA AKIJISOMEA USIKI NA KWA BAHATI MBAYA ALIUSAHAU KUUZIMA HADI UKAWASHA GODORO. HABARI ZAIDI ZINASEMA HUENDA IDADI YA WALIOFARIKI IKAONGEZEKA, KWANI HADI SASA WANAFUNZI WAWILI HAWAJULIKANI WALIPO. NI AJALI NYINGINE MBAYA YA MOTO KUTOKEA SHULENI AMBAYO INAWAKUMBUSHA WATU ILE AJALI MBAYA KULIKO ZOTE YA 'MOTO WA SHAURITANGA'!

JUMAPILI NJEMA

Nawatakieni nyote Jumapili njema. Ni siku ya kuongea na Mungu kwa namna ya pekee zaidi.Tuitumie vema.

Picha kwa Hisani ya MAISHA

Saturday 22 August 2009

TUTAFIKA KWELI?

MAMBO YA "SUMMER TIME"

Mke wa rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama amezidi kuonyesha tofauti yake na wake wa marais waliopita wa Marekani. Michelle amekuwa mke wa kwanza wa rais kuvaa kikaptula na kupanda dege la rais Air Force One walipokuwa katika mapumziko na ziara fupi huko Arizona. Taswira hii imepewa maelezo tofautitofauti

MFUNGO MTUKUFU - RAMADHAN KAREEM


Nawatakia wadau wahusika wote Mfungo mwema wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Allah awawezeshe kuchuma matunda yatokanayo na mfungo huu.Kila mmoja anuie katika kutenda mema na matendo ya huruma zaidi.Ramadhan Mubaaraq

Sikutamanishi ila nakukumbusha tu mambo yahitajikayo kwa futari ndani ya mfungo huu.

Friday 21 August 2009

WATOTO KATIKA NCHI YA SHIBE

Pamoja na ukweli kuwa nchi yetu imebarikiwa katika mambo mengi, bado hali ya maisha ni ngumu kwa wengi.Chakula ni cha kubangaiza na hata wakati mwingine baadhi ya jamii zinalazimika kuokota chakula toka majalalani. Hali hii inapaswa kufikia tamati. Hata hivyo, hili ni jukumu la Taifa zima si viongozi peke yao.

Wednesday 19 August 2009

HASHEEM THABEET ALIPOKARIBISHWA IKULU

Jamaa kakwea hadi raha. Hii nayo ni Fahari ya Tanzania!

MSIBA JIMBO KUU KATOLIKI MWANZA-ASKOFU MKUU MAYALLA


ASKOFU mkuu wa jimbo kuu la Mwanza, Kanisa Katoliki Mhashamu Anthony Petro Mayalla (69) amefariki dunia leo mchana kutokana na maradhi ya moyo baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini kwake.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkurungenzi wa mawasiliano wa baraza la Maaskofu (TEC) kanisa katoliki, Padri Revocatus.Makonge Askofu huyo amefariki baada ya madaktari wa Hospitali ya rufaa ya Bugando kuhangaika kumpatia matibabu bila ya mafanikio.

Alisema kuwa marehemu aliamuka salama leo na kuendelea na shughuli zake za kila siku ofisini kwake mpaka majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando.Habari kutoka katika ofisi ya aksofu huyo, zimeeleza kuwa alipatwa na maradhi hayo wakati akiwa katika maandalizi ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Vatican ambaye alikuwa akitarajiwa kufanya ziara jimboni kwake Oktoba 5 mwaka huu kwa ajili ya kufungua ujenzi wa hospitali ya watoto.“Baada ya kufikisha hospitalini hapo madaktari waliahangaika kuokoa maisha yake lakini nahati mbaya lifariki dunia majira ya saa 8;30 mchana,” alieleza Padri Revocatus Makonge.

Askofu Mayalla alizaliwa Aprili 23 mwaka 1940 katika katika kijiji cha Nera wilayani Kwimba na kupata elimu yake ya msingi katika wilaya hiyo na masomo ya sekondari.Askofu Mayalla alikuwa amehitimu shahada ya kwanza ya elimu aliyopita katika chuo kikuu cha Loyola huko Chicago Marekani mwaka 1973 hadi 1975

BAADA YA "FAKE PASTOR", SASA NI "VILLAGE PASTOR"

Filamu hii murua itakuwa mitaani kuanzia mwisho wa mwezi huu. Mtunzi na mwigizaji mkuu ni Kanumba na inasemekana inatoa taswira ya tukio la kweli lililotukia. Karibu ununue filamu za Kitanzania kuijenga nchi yako na kuinua vipaji vya washiriki.


Picha kwa Hisani ya Michuzi