Sunday 6 February 2011
BUTIAMA NA MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA MWL.J.K. NYERERE
1.Hili ni jumba la Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere, Butiama mkoani Mara.
2.Picha mbali mbali za Mwalimu enzi za uhai wake.
3.Redio aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali alipenda pia kuitumia katika baadhi ya ziara zake za ndani na nje ya nchi. Redio hii alipewa zawadi huko Ujerumani mwaka 1969.
4.Hivi ni baadhi ya viatu alivyokuwa akivaa Hayati Mwalimu J.K.Nyerere. Mwalimu alipenda zaidi viatu vya kutumbukiza, pembeni kama mkoba ni redio yake. Itizame kwa uzuri katika picha inayofuata.
5.Urithi wa asili wab Tamaduni za kizanaki silaha za jadi, vifaa vya nyumbani, ala za muziki, mapambo ya asili, lugha, mila, desturi - nk. Vyte utavikuta kwenye nyumba hii ya makumbusho ya Mwalimu.
6.A gift of traditional stool given to Mwl. Nyerere by the residents of Dar-es-Salaam after the victory of Kagera war in 1978 - 1979.
7.Joho la Uhitimu.
8.Jiwe la kusagia nafaka huitwa 'Ombwe' na dogo huitwa Esyo, kwa kawaida kazi ya kusaga hufanywa na wanawake. Chakula kikuu cha wazanaki ni ugali, huliwa kwa nyama, samaki na mboga za majani. (Picha:Mdau Mwanza)
TUJIPANGE KUANZA VIZURI WIKI YA KAZI
Saturday 5 February 2011
Noti Mpya Zimechakachuliwa: Gavana Ndulu
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekiri kuwa noti mpya ilizozitoa kuanzia mwezi uliopita zimeanza ‘kuchakachuliwa’ na wahalifu kwa kutengeneza noti bandia.
Subscribe to:
Posts (Atom)