Sunday 29 June 2014

MFUNGO MWEMA KWA WAISLAMU WOTE

NAWATAKIA JPILI NJEMA

Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu mahali fulani hapa nchini. Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole. Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia kanisani kusali. Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?
Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,
“Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”
Mwanaume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada
“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, Asante kwa ujumbe wa leo kutoka kwa mtumishi wako Mchungaji, Asante kwa miujiza ya uponyaji. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika, Kanisa woote tuseme Amen”
Baada ya kumaliza sala tu, alijikuta kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu kwani ibada ndo tu ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya kufunga ibada!
hii kali.
Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la.


Saturday 28 June 2014

BRAZIL WATINGA ROBO FAINALI

Timu ya Taifa ya Brazili imefuzu kuingia robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuitoa Chile kwa Penalt 3-2. Bao la ushindi la penalt lilifungwa na mchezaji maarufu wa Brazili Neymar Jr.
Wachezaji wakifurahia ushindi wao
Mlinda mlango wa Brazil Julio Cesar akiokoa moja ya hatari langoni mwake. Kipa huyu pia amezuia penalt 2 za Chile leo.

16 BORA KOMBE LA DUNIA KUANZA RAUNDI LEO

LIKE FATHER ,LIKE SON

Ukweli huu unamhusu Raisi wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyata. Kweli uraisi upo kwenye damu kwakuwa waswahili wanasema "Ukiona vyaelea,vimeundwa"

Mzee Jomo Kenyatta akiwa na mtoto wake ambae ni Uhuru Kenyatta enzi hizo za utoto, unaweza kushea hii picha na wenzako waone... (picha kutoka Nation Media)

NAWATAKIA WAISLAMU WOTE MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

KUANGUKA KWA ELIMU NCHINI HUANZA HIVI

Japo si lazima kuwa hivyo, lakini kwa kiasi fulani upanishaji wa ada vyuoni husababisha wale wenye uwezo kifedha kumudu masomo na wale wasio na uwezo kifedha hata kama wana uwezo mkubwa kiakili na ki-tunu kuwa waalimu bora baadae hushindwa. Hii inapelekea kujikuta mashuleni kunazidi kuwa na upungufu wa walimu na kutofaulu vizuri kwa wanafunzi kunaendelea. Ni vyema Wizara husika iliangalie hili.

Friday 27 June 2014

UZALENDO WA KWELI

Jana Timu ya Taifa ua USA ilicheza na Ujerumani katika kufuzu 16 bora za Kombe la Dunia huko Brazili. Raisi wa Marekani Mhe. Barack Obama akiwa safarini ndani ya ndege yake AIR FORCE ONE nae alifuatilia pambano hilo ambapo Marekani na Ujerumani zote zilifanikiwa kuingia 16 bora
Mhe.Raisi Barack Obama na cabinet yake ndani ya AIR FORCE ONE wakitazama kabumbu
Kocha wa Timu ya Taifa ya Marekani aliamua kuandika barua hii kuwaomba viongozi mbalimbali waipe support timu hiyo
Gavana wa New York alijibu kwa kumhakikishia kocha huyo kwamba atawaongezea wafanyakazi wake muda wa ziada wa pumziko mchana ili waweze kuishangilia timu yao

HII HAIKUBALIKI

Imekuwa tabia inayozoeleka kwa Matrafiki kujificha sehemu na kisha kutokea barabarani ghafla na kusimamisha gari kwa lengo la kukagua makosa. Ni sawa kwamba ukaguzi wa magari kuhakikisha usalama ni muhimu, lakini kwa staili hii ni mbaya maana wakati mwingine dreva anapata mshtuko na yaweza kusababisha ajali. Ni vema Maafisa hawa wakawa wanatumia utaratibu unaoeleweka. Hata hivyo ni muhimu pia kwa madreva na wamiliki wa vyombo vya moto kujitahidi kufuata sheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vyombo vyao ni salama kwa usafiri wa abiria na mali zao.

WEEKEND NJEMA WADAU

Mwisho wa juma umewadia, nawapa pole kwa majukumu mbalimbali ya kujenga Taifa,familia na pilika zote za kutafuta maisha bora. Ila ni muhimu kuwa makini namna tunavyotumia weekend zetu hasa ukizingatia hii imekuja mwishoni mwa mwezi pia.
Kwa staili hii ya unywaji, tutafika kweli???

"SIJUI CHUMVI IMEKOLEA VIZURI????"


TBC 1 WAPEWA GARI LA KISASA LA KURUSHIA MATANGAZO KUTOKA CHINA


Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam
Sehemu ya ndani ya gari hilo ambapo kuna stesheni nzima ya urushaji wa matangazo  moja kwa moja kama vile kutoka TBC1 Mikocheni.

Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China jana jijini Dar es Salaam.

Thursday 26 June 2014

USIVUKE MSTARI

Hii ndio staili mpya ya kuchora mstari kwa chaki yakupuliza ambayo huyeyuka baada ya muda mfupi inayotumiwa huko Brazil kuonyesha mstari wa kujipanga wakati wa kupiga mpira wa adhabu. Maendeleo...


MARCIO MAXIMO AJA TANZANIA KUIFUNDISHA YANGA

Aliyekuwa kocha wa timu ya Tanzania,Marcio Maximo amerudi tena Tanzania baada ya kuhitajiwa na timu ya Yanga kuifundisha.

Wednesday 25 June 2014

MWL.NYERERE FOUNDATION SQUARE KUJENGWA

Serikali ya China ikishirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua jiwe la Msingi la jengo jipya litakalojengwa kwa gharama ya zaidi ya dola milioni 77. Jengo hilo litakalojulikana kama Mwl.Nyerere Foundation Square litaleta mandhari nzuri jijini Dar na kuwa kivutio kwa mengi ikiwemo Utalii.
Mwonekano wa Jengo hilo litakapokamilika
Makamu wa Raisi wa China,Mheshimiwa Li Yuanchao na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe,Mizengo Pinda wakimwaga mchana kuashiria kianza rasmi kwa ujenzi wa jengo hilo
Mama Maria Nyerere akiwasili katika sherehe za uzinduzi wa jengo hilo

NIGERIA WAINGIA 16 BORA KOMBE LA DUNIA

Timu ya kwanza kutoka Afrika kutinga 16 bora ya Kombe ya Dunia mwaka huu,Nigeria imepata nafasi hiyo katika mechi ilomalizika hivi punde dhidi ya Argentina japo wamefungwa mabao 3-2
Wachezaji wa Nigeria wakishangilia baada ya kufunga moja ya magoli yao leo

Tuesday 24 June 2014

UMEME LEO KIZAAZAA


Sehemu kubwa ya nchi leo imekuwa na katizo la umeme kufuatia hitilafu katika Gridi kuu ya Taifa. Tanesco na Serikali angalie jambo hili maana maendeleo ya nchi yanazidi kudorora kwa kukosa vinavyochangia kuleta maendeleo kama matumizi ya umeme.
Wakuu nao wapatwa na adha hii hadi kuamua kutumua tochi  ya simu,loh. 

NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI


Monday 23 June 2014

UTAFUTAJI USIO SAHIHI

Wiki ya pilikapilika imeanza kila mmoja akijaribu kujitafutia riziki. Ila kwa wengine wanazitafuta kwa njia isiyo sahihi. Tuwe macho nao

Sunday 22 June 2014

MCHANGO WA MHE. GODBLESS LEMA KWA BUNGE LA BAJETI 2014

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ni miongoni mwa waliowasha vipaza sauti kwenye bunge la bajeti linaloendelea Dodoma ambapo sehemu ya alichochangia ni hiki kinachofata hapa chini. 
‘Dola bilioni moja miaka kumi nyuma ilikua ni Trilioni 11 lakini sasa unaongelea Trilioni 17 kwa hiyo shilingi imeshuka thamani lakini unashangaa kwanini tunaendelea kuongeza ushuru kwenye pombe na sigara kama chanzo cha mapato ya taifa letu, nchi nyingi duniani zinazoongeza ushuru kwenye pombe na sigara lengo lake ni kuona idadi ya wanaokunywa na kuvuta inapungua tofauti na Tanzania ambako lengo limekua ni kukusanya mapato, hiki ni kitu cha kusikitisha sana’

‘Nimekwenda Singida hivi karibuni kwenye ziara ya chama chetu na Mh. Tundu Lissu, ukiwa Singida na Dodoma unaona kuna jua kali… Singida Same serikali imeweka vikao barabarani >> NENDA POLEPOLE HAPA KUNA UPEPO MKALI UNAUA << ingekua ni taifa kama Israel, upepo mkali hauwekewi vibao vya kuua bali upepo mkali unachukuliwa kuwa umeme’

‘Sehemu kubwa ya Singida na Dodoma ni semi desert, serikali ingeweza kabisakabisa kutengeneza solar village maeneo haya ikatengeneza umeme mkubwa kupitia nguvu za jua ukaingiza kwenye gridi ya taifa na mngeweza kupunguza bili za umeme ambazo Wananchi kwa sasa wanapigwa huko mitaani’

‘Hata kama kutakua na mpango wa aina gani, unapokua na serikali ambayo haifikirii kwa upana… serikali ambayo inasema bado inakopesheka, bado tunaweza kukopesheka…. mimi ningekua ni nyinyi, ningekwenda kukopa barabara zote nchi nzima zijengwe, ningeenda kukopa reli ijengwe, ningekwenda kukopa Airport ziboreshwe na ningekwenda kukopa serikali yenu ihamie hapa Dodoma’

‘Watu wengi wamesema kuhusu serikali kuhamia hapa Dodoma, ukiondoa serikali Dar es salaam ukaileta Dodoma utaipa nguvu hii Ruaha ambayo hakuna watalii, watalii wataanza kwenda kwa sababu wakuu wote wa nchi watakuwa wanakuja Dodoma kufanya mikakati yao kwa hiyo centre ya mapumziko itakua ni Iringa, Mbeya na Singida hapa’
‘Mimi ningekua nyinyi ningefanya maamuzi magumu, ningechukua Mawaziri wote na makatibu wakuu wote waje hapa wakae gesti na wengine wakae kwenye matent kwa sababu msipochukua maamuzi serious hamuwezi kuibadili hii nchi, hii nchi haitobadilishwa kwa Kinana kuzunguka kutafuta kura za Urais huko kote anakokwenda’

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Nimeipenda picha hii iwe mwangaza wetu kwa siku ya leo. Katika maisha ni muhimu sana kujali utu wa mtu kwanza kabla ya makandomando ya nje. Nimewapenda maharusi hawa maana wameweka utu na upendo wa kweli mbele bila kujali mapungufu yao. Hakika maisha yao ni ya baraka maana kilichopo moyoni ndo kinasimamia maisha yao. Hongereni sana na Mungu awabariki.

WAJERUMANI NGUVU SAWA NA GHANA

Katika mechi iliyomalizika hivi punde, timu za Ujerumani na Ghana zimetoka droo kwa kufungana goli 2.
Mechi hiyo ya kusisimua ambayo kila moja ilikuwa na wachezaji ndugu Kevin Prince Boateng wa Ghana na Jerome Boateng wa Ujerumani, ilipata mabao yote katika kipindi cha pili.

Saturday 21 June 2014

FIFA UJERUMANI NA GHANA LEO


AJALI MAKONGO

Kuna ajali imetokea eneo la Makongo nje kidogo ya Mwenge Dar likihusisha Daladala ya abiria (Makumbusho-Kunduchi) na lorry.Inasemekana watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha. 


**Picha za magari yalohusika na ajali hiyo kwa hisani ya Dj Sek Blog**


AHADI YA KIZALENDO YA MHE.RAIS JAKAYA KIKWETE

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete amesema atajitolea kurudi kufundisha katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi baada ya kumaliza awamu yake ya Uongozi katika nchi kama Raisi. Ameyasema hayo jana katika mdahalo wa Wahadhiri na wanafunzi wa Chuo hicho huko Kunduchi Dar es Salaam. Itakumbukwa mhe Raisi alikuwa akifundisha katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania huko Monduli kipindi fulani.

Friday 20 June 2014

KWA MTINDO HUU, BRAZIL SI YETU


ENGLAND BYE BYE FIFA

Katika mechi ya jana, England imechapwa bao 2 kwa 1 na Uruguay. Kwa maana hiyo Uingereza haina point hata moja na hivyo kuzaaga mashindani baada ya mechi moja itakayofuata.
Suarez akiifungia Uruguay moja ya magoli yao

Thursday 19 June 2014

AJALI YA LORI KINYEREZI/UKONGA

Sheria za barabarani ikiwa ni pamoja na kuzingatia vigezo ya uzito unaokubalika ni muhimu


TAARIFA MUHIMU KUTOKA DART SEHEMU YA BARABARA MATAA UBUNGO KUFUNGWA KESHO KUPISHA UJENZI


Sehemu ya Barabara katika makutano ya Mandela na Morogoro sehemu ya Ubungo Mataa, itakufungwa kuanzia kesho usiku hadi Jumamosi asubuhi kupisha ujenzi wa barabara ya Mabasi yaendayo haraka. Wananchi waombwa kufuatilia maelekezo na wanaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

Najua huu ni msemo unaotumiwa san ana viongozi wetu, na bahati mbaya ni pale wanapoomba kura. Lakini tunawakumbusha kuwa wajitahidi kutekeleze ahadi zao maana kwakweli hali za walio wengi zinatisha. 
Hatukatai viongozi kutembelea Land Cruiser V8 za mamilioni ya fedha, lakini mwaona hawa waliowapigia kura wana makazi gani na huo usafiri wao hapo nje???

Tungefurahi huduma za afya kusogezwa karibu na wananchi na sio kuwaza kupeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi. Katika mazingira haya kweli huyu mgonjwa ataona ahueni yoyote?

Haya nayo ni makazi, mvua zikinyesha je?

Mzalendo wa kweli.

HISPANIA YABANWA VIBAYA FIFA HII

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Timu ya Hispania, leo tena imechapwa na CHILE magoli 2 bila katika mechi iliyomalizika hivi punde
Hii ndiyo timu ya Chile iliyowaangamiza Hispania
Golikipa wa Hispania Casilas akiwa amejishika kuno kutokujua afanye nini baada ya mchezaji wa Chile kufunga goli.
Shabiki akionyesha maandishi yenye maana "Kwaheri Hispania" maana matumaini ya timu hiyo kuendelea ni madogo. Mpaka sasa timu hiyo imefungwa mechi zote na haina pointi hata moja