Friday 31 January 2014

MWANAMKE MFUPI SANA NA MREFU SANA KTK REKODI YA DUNIA KWASASA

At just under 25 inches tall, Jyoti Amge of Nagpur, India, is the world’s shortest woman. She’s a college-bound student, with dreams of making it as an actress. Still, she weighs just 12 pounds — only nine pounds more than she did at birth.

Huyu nae ndio mwanamke mwenye urefu wa futi 7 huko huko Bara Hindi. Hapo kainama kidogo kupata taswira akiwa na wazazi wake

Thursday 30 January 2014

BABU WA LOLIONDO

Makazi ya Babu wa Loliondo kabla hajagawa kikombe. Makazi mapya na ya kisasa ya Babu wa Loliondo baada ya shughuli-tiba ya kugawa kikombe

Wednesday 29 January 2014

TASWIRA ZA USAFIRI WA TIMU MBALIMBALI ZA DUNIA

AZAM-Tanzania La mbele SIMBA la nyuma YANGA-Tanzania AC MILAN-Italy MANCHESTER UNITED-UK FC BARCELONA-Spain BUYERN MUNCHEN-Germany REAL MADRID-Spain

KIFAA CHA KUWEKEA TAKA.

Kifaa hiki kipo katika moja ya masoko ya manispaa hapa Tanzania. Sikosoi ila kwakweli hatuna matumizi mazuri ya kifaa hicho kiasi cha kukifanya hata chenyewe kionekane ni takataka. Tazama hapa chini kifaa kama hicho katika nchi za wenzetu. Hii ni mahali fulani nchini Ujerumani

DUNIANI KUNA MAMBO

Wakati mwanadada huyu kaamua kujikoleza mkorogo ili awe mweupe........ ......mzungu huyu nae katafuta mkorogo wake awe mweusi. Ila Blog hii inashauri kwa kusema "Natural is beutiful"

Sunday 26 January 2014

Friday 24 January 2014

VIONGOZI WA MFANO TANZANIA

Waziri wa Ujenzi Mhe. john Magufuli akikagua na kuhimiza ukarabati wa daraja la Dumila huko Kilosa. Mhe Waziri Magufuli akiruhusu lori la kwanza kupita baada ya ukarabati kufikia kiwango cha kuridhisha.

Thursday 23 January 2014

SERIKALI MNALIONA HILI?

Pengine watoto hawa wangetakiwa kuwa darasani wanasoma au nyumbani wamepumzika. Kwa mtazamo wangu, ni mapema sana kuhusishwa katika kazi kama hizi. Elimu ya kujitegemea ni suala zuri lakini kwa kiwango gani? Ugumu wa maisha,huduma duni,migawanyo isiyo sawa ya rasilimali,kumomonyoka kwa maadili na mengine km hayo yanapelekea vijana wadogo kujiingiza katika biashara za utotoni kukidhi maisha Hapa ni uwanja mkubwa wa mpira ambapo watoto hawa wanafanyishwa kazi. Inawezekana kabisa kuna fungu lilotengwa kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huu, sasa kwanini wanatumika watoto?

Tuesday 21 January 2014

MAENDELEO DARAJA LA KIGAMBONI

Huu ndio mwonekano mpya wa daraja la kigamboni kwa sasa

Hivi karibuni waziri wa ujenzi Mheshimiwa John Magufuli alifanya ukaguzi wa maendeleo ya daraja la kigamboni. Na hivi ndio linavyoonekana kwa sasa likiwa limeshaunganisha nchi kavu mbili

Monday 20 January 2014

KULA KIAPO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wake Dk Ghalib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na mawaziri katika sherehe ya kuapishwa kwa baadhi ya mawaziri wapya iliyofanyika Ikulu jioni ya leo

Sunday 19 January 2014

TUMALIZIE WIKI KWA KUPEANA MOYO NA CHANGAMOTO

Japokuwa ni mwanzo tu wa mwaka, kwa wengine tayari maisha yashaanza kuwachosha kiasi cha kukata tamaa. Lakini ni muhimu kuamini kuwa ambalo halijawezekana leo unaweza kujaribu kesho likawezekana. Tusikate tamaa.

Kwa tafsiri ya haraka ni kama vile mtu huyu amekata tamaa. Hiyo ni njia ya treni. Inamaana akiishia usingizini na treni ikipita hapo. Ni kifo tu. Hapo sio sehemu sahihi ya kupumzikia. Bila shaka huyu anataka kufupisha maisha yake kwa kifo hicho. Hapana. Tusikate tamaa. ((SAMAHANI WADAU KWA PICHA HII INAYOFUATA MAANA INAHUZUNISHA SANA.)) Katika picha hiyo ya ajali inayodaiwa kutokea huko Nigeria, dada huyu alipatwa na umauti baada ya kuamua kujilaza relini baada ya ugomvi wa kimapenzi. Jamani hasira hasara. Ni kweli inaumiza kupata na mtafaruko wa kimapenzi lakini isiwe ndo sababu ya kusitisha maisha.

MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,leo amefanya uteuzi wa Mawaziri na Manaibu wapya. Pia hii imehusisha kuteua wapya,kuhamisha na pia kupandisha au kushusha wengine.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mbele ya jopo la Waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam. Baraza Jipya la Mawaziri ni kama ifuatavyo: Mabadiliko na uteuzi huo kamili ni kama ifuatavyo:- OFISI YA RAIS Hakuna mabadiliko. OFISI YA MAKAMU WA RAIS Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb) Waziri wa Nchi (Mazingira). Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb) Naibu Waziri OFISI YA WAZIRI MKUU Hakuna mabadiliko WIZARA: WIZARA YA FEDHA Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) – Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) – Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)- Naibu Waziri wa Fedha WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA Hakuna mabadiliko WIZARA YA KATIBA NA SHERIA Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)-Waziri wa Katiba na Sheria Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI Hakuna mabadiliko WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA Waziri – Hakuna mabadiliko Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) – Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa WIZARA YA UJENZI Hakuna mabadiliko WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)- Waziri wa Mambo ya Ndani Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)- Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)- Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI Waziri: Hakuna mabadiliko Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO Waziri: Hakuna mabadiliko Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) – Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)- Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi WIZARA YA KAZI NA AJIRA Hakuna mabadiliko WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Hakuna mabadiliko WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI Waziri – Hakuna mabadiliko Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) – Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WIZARA YA MAJI Waziri – Hakuna mabadiliko Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)- Naibu Waziri wa Maji WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA Waziri – Hakuna mabadiliko Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) – Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika WIZARA YA UCHUKUZI Hakuna mabadiliko WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO Waziri – Hakuna mabadiliko Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) – Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo WIZARA YA MALIASILI NA UTALII Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)-Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii WIZARA YA NISHATI NA MADINI Waziri – Hakuna mabadiliko Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb) Naibu Waziri (Nishati) Ikulu DAR ES SALAAM 19 Januari, 2014 

Saturday 18 January 2014

Friday 17 January 2014

WACHINA KUTENGENEZA TENA MELI YA TITANIC.

PENGINE TUJIKUMBUSHE KIDOGO KUHUSU MELI YA TITANIC. *Titanic* ilikuwa meli  kutoka Uingereza iliyojengwa kati ya 1909 na 1912 huko Belfast . Wakati ule ilikuwa meli kubwa duniani pamoja na mwenzake "Olympic". Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki  kati ya Uingereza na Marekani . Kwenye safari yake ya kwanza iligongana nasiwa barafu  tar. 14 Aprili 1912 mnamo saa sita kasorobo usiku ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 katika usiku wa tar. 15. Aprili 1912. Watu 2200 walikuwepo kwenye meli. Katika maji baridi takriban 1500 walikufa ni 700 waliookolewa na meli zilizokimbia kuokoa watu. Hapa inaonekana "Titanic" ilipotoka bandari ya Belfast  kwa safari za kwanza za majaribio 2 Aprili  1912. Kampuni kutoka China ya Star Investment Group katika mkoa wa Sichuan imesema itatumia dola za kimarekani milioni 165 katika kuijenga upya mpaka kuikamilisha meli hiyo yenye mfano wa Titanic. Katika meli hii ya Replica ni ishara ya uvumbuzi uliopita kikomo kutoka kwa wachina.

Thursday 16 January 2014

"FRESH" KUTOKA SHAMBANI/BUSTANINI

Haya ni maboga huko Nangulukulu kusini mwa Tanzania. Hapa wafanyabiashara wanaonekana wakiuza mazao haya mazuri ya shamba,lakini pembeni kuna lundo la uchafu kitu kinachochangia matatizo mengi ya kiafya. Tukumbuke kuweka mazingira yetu kwa usalama wa afya zetu.

Wednesday 15 January 2014

GAZETI LA NEW YORK TIMES LALIPANDISHA JINA JIJI LA DAR-ES-SALAAM

The New York Times has named Dar es Salaam among 52 places in the world to go in 2014.
The American daily newspaper, which founded and continuously published in New York City since September 18, 1851, writes:

Tanzania may be best known for the snow-capped peaks of Mount Kilimanjaro and the game-packed plains of the Serengeti, but the real pulse of the country is found in its largest city, Dar es Salaam. An eclectic mix of music echoes through the beach clubs, open-air bars and nightclubs of this Indian Ocean coastal city. Old-school dance music competes with Swahili hip-hop and traditional drumming, all drawing from the city’s African, Indian and Arab influences. Add in the street food, the beaches and the fact that the year-old African low-cost carrier Fastjet uses Dar as its hub, and it’s easy to see that this commercial capital is more than a stopover on the way to Tanzania’s natural splendor. It is an African metropolis coming into its own.

Tuesday 14 January 2014

CHRISTIANO RONALDO:MWANASOKA BORA WA DUNIA

Usiku wa kuamkia leo, FIFA imemtangaza mchezaji wa Real Madrid kuwa mwanasoka bora wa dunia. Nafasi hii ilikuwa inashikwa na mchezaji bora wa Argentina na klabu ya Barcelona; Lionel Messi.

MATUMIZI MAZURI KWA TULICHOPEWA NA MUNGU

Mungu ametuumba alivyotaka mwenyewe. Pia kagawa riziki kwa kila mmoja kwa namna alivyotaka. Ila busara ya kawaida inatukumbusha kuwa na matumizi mazuri kwa tulichopewa na mungu. Hapa nakupa mifano michache;

Unapokula mpaka kusaza na kuamua kumwaga jalalani, kumbuka pia kuna binadamu anakufa njaa mahali fulani. Hivyo:Tumia kwa busara Unapowaza kuchoma nguo yako moto eti kwasababu tu dobi au mfanyakazi wako hakuinyoosha vizuri........ .....Kumbuka kuna binadamu mahali fulani anatembea uchi au na nguo zilizotatuka. Hivyo: Tumia kwa busara. Au hivi na anamtukuza muumba wake. Unapowaza kutupa jalalani kiatu chako eti kwa kuwa mpiga rangi hakukingarisha vizuri...... Kumbuka kuna binadamu mwenzio anaridhika na hiki alichovaa. Au hivi tangu utotoni. Unapowaza kukataa kwenda shule kisa wazazi hawajakununulia baiskeli kama ya John..... Kumbuka kuna wanafunzi wenzio hutembea umbali mrefu kwa miguu kwenda na kurudi shule Na tena kama hiyo hatoshi,wanawasili kwenye shule yao hii hapa

Monday 13 January 2014

KUMEKUCHA

Ni jumatatu mwanzo wa juma ambapo kila mtu anaianza siku yake kivyake. Kwa baadhi ya wafanyakazi,wafanya biashara na hata wanafunzi;huianza siku kwa vurugu hii ya usafiri. Kwa wanafunzi wa Shule za Awali na Msingi ambapo wengi wanaanza masomo leo,kila mmoja anawaza yake. Wengine wawaza watafikaje shuleni,wengine wanawaza namna ya kukabiliana na mazingira ya shule na changamoto km hizo Wengine wao mambo si mabaya Wengine mpaka huduma za kompyuta wanazo