Tuesday 31 March 2009

MICHEZO YA WATOTO

Huu sijui unaitwaje

Mdako

Bao

Michezo hii inawajengea watoto tunu njema nyingi kama umakini, utulivu, furaha, urafiki, ubunifu, kuchemsha bongo, kutulia nyumbani na mengine mengi. Yafaa kuendelezwa

Picha kwa hisani ya Baraka Chibiriti

HII NI BILA BILA



Tatizo la usafiri linalopelekea kujazana kwenye vyombo rasmi na visivyo rasmi vya usafiri kimakosa na hivyo kuhatarisha maisha. Hii si kwetu tu,hata kwa wenzetu, ila si kwamba tunahalalisha hili!

Aaaaah ndio! BABA NA MWANA


Hii inafundisha na kurekebisha hali ya kutegeana katika malezi na makuzi ya mtoto ambapo zamani ilikuwa "Mama na Mwana" tu

Monday 30 March 2009

AJALI YA TRENI


Imetokea ajali ya Treni huko Dodoma na kuua Abiria 13 papo hapo na wengine kujeruhiwa. Hii ni baada ya treni ya Abiria kugongana na Treni ya Mizigo.

Saturday 28 March 2009

SHUKRANI KATIKA HUZUNI





MwanaBlog anatoa shukrani za pekee kwa wote wanaoendelea kumfariji katika kipindi hiki kigumu akiwa nchi za mbali na hivyo kushindwa kuhudhuria mazishi ya baba mpendwa.Asanteni sana na Mungu awakarimu.

HUZUNI



Mpendwa Mzee Amedeus Mwangoka,Baba mzazi wa mwenye Blog hii ametutoka ghafla Kibosho Hospital-Moshi, usiku wa Jumatatu 23/03/2009. Mazishi yanafanyika leo Jumamosi 28/03/2009 nyumbani Kilingi-Sanya Juu Kilimanjaro. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. Apumzike kwa Amani.Amina.

Monday 23 March 2009

MOTO MOTO MOTO



Paradise Holiday Resort pamoja na Ocenic Bay zote zikiwa Bagamoyo zachomeka na moto mkubwa. Kwa mujibu wa shuhuda wetu moto huo ulianza eneo la Bistro Alakat Restaurant ambapo cheche za moto ziliwaka hadi kwenye makuti. Moto ukaenea kwenye Main Restaurant iliyo karibu na store ya chakula. Moto huo ulienea hoteli nzima na ikawa vigumu kuuzima. Magari ya zima moto yalichelewa kufika eneo la tukio kwa sababu yanatokea Dar es salaam. Hoteli hii ya kifahari imeteketea kabisa kilichobakia ni vibanda vitatu vya makuti katika eneo la bahari, Paradise Holiday Resort ilikuwa na vyumba tisini na tano. Moto huwo huo pia umeathiri Hoteli ya jirani ya Oceanic Bay, kiasi cha hasara hakijajulikana mpaka sasa.

Tuesday 17 March 2009

MAMBO YA KITOWEO



Kuku wa VINGUNGUTI, na SAMAKI WA FERRY

Monday 16 March 2009

"HOME SWEET HOME" Iwapo umebobea maeneo ya anga za mbali,unapowaza kwenda kusalimu makazi asilia kwa Babu na Bibi,yawezekana ukapitia mpangilio huu.

Unaondokea katika Jiji maarufu kama hili
Unachukua usafiri wa basi hapa kuelekea Airport

Unapita Barabara hii kuelekea Airport

Unaingia katika kiwanja hiki au hiki cha ndege


Unachukua usafiri wa Ndege kama hii

Unapokaribia Nyumbani Tanzania, unaona mandhari safi ya Jiji la Dar-es-Salaam

Unashukia katika kiwanja chetu cha ndege

Unachukua usafiri huu kuelekea katikati ya Jiji kujipumzisha kwa muda kabla ya kuelekea kijijini kwa Babu na Bibi

Unajipumzisha katika moja ya sehemu kama hii

Unatembelea sehemu kama hizi kabla ya kuondoka, huku ukituma usafiri kama huu





Halafu unaondoka kuelekea Ubungo Bus Terminal kwa usafiri huu au huu


Safari ya kuelekea Kijijini toka Jijini inaanza hapa

Vijijini unapokelewa na usafiri kama huu kuelekea makazi asilia


UNAPOTEMBEA KUELEKEA NYUMBANI UNAPISHANA NA WANAKIJIJI WENZIO WANAOTESA KWA RAHA ZAO KIVYAOVYAO




Hatimaye kwa BABU,BIBI na wengineo



Sunday 15 March 2009

NYAMA CHOMA


Raha ya nyumbani ni pamoja na kupata Nyama choma ya "meeeeeeeeee"

HEBU LEO TUCHEKE NA KUFURAHI KUPITIA KATUNI, ILA LAKINI TUBEBE NA UJUMBE ULIOPO















Katuni hizi ni kwa hisani ya Global Publishers