Wednesday 16 August 2017

BODABODA MARUFUKU KUBEBA WATOTO NA WANAFUNZI CHINI ZA MIAKA 10

Jeshi la Polisi August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au vyote viwili.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Theopista Malya, amesema kuwa watoto wamekuwa kwenye hatari kubwa wakipandishwa kwenye Bodaboda na wakati mwingine waendesha bodaboda hubeba watoto zaidi ya mmoja jambo ambalo ni lazima likemewe.

Aidha, alisema kuwa Jeshi hilo limeandaa kipindi maalumu cha Radio kitakachorushwa na Clouds FM kila siku ya Jumatano saa 2:00 Usiku kikiwa na lengo la kuongeza elimu kwa waendesha Bodaboda katika kuzingatia Usalama Barabarani pindi wanapofanya shughuli zao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani (TSA), John Seka alisema kipindi hicho kitalenga kuwapa elimu waendeshaji wa bodaboda.

Pia, alitumia nafasi hiyo kuwataka wafuate sheria zilizowekwa na Sumatra ili waepukane na mkono wa sheria.

Paulina Shayo ambaye ni mwakilishi kutoka WAT Saccos alisema kuwa wanatoa mikopo kwa bodaboda na kwamba mikopo hiyo itawasaidia kuwa wamiliki halali wa vyombo hivyo.

Sunday 30 July 2017

Sunday 23 July 2017

HABARI NJEMA. CCM KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI YATIMA VYUO VIKUU

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wake, Humphrey Polepole kimetangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambao wamekosa mikopo ya kuendelea na masomo na wanafunzi ambao ni yatima.

Taarifa iliyotolewa na Polepole inasema kuwa wanafunzi hao wanapswa kufika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kusaidiwa shida zao hizo za mikopo, jambo ambalo limepokewa tofauti na baadhi ya watu wakidai kuwa suala la kutoa mikopo kwa wanafunzi ni jukumu la bodi ya mikopo.

Kutokana na mitazamo ya watu kuwa tofauti katika jambo hili, Humphery Polepole aliibuka na kusema kuwa upinzani wa Tanzania ni mtihani mkubwa kwani wanapojaribu kutatua matatizo ya watu wanakujua juu na wasipotatua matatizo pia wanakuja juu.

"Tukikaa kimya kwa shida za watu inakuwa tatizo, tukishughulika na shida za watu inakuwa tatizo kubwa. Huu upinzani mtihani" alisema Polepole

POLENI KWA BLOG YENU KUTOKUWA HEWANI MUDA

Wapendwa wanablog ya Karibu Nyumbani, kwa takribani wiki 4 hivi Blog yenu haikuwa hewani kutokana na Safari ya Kikazi sehemu ambapo upatikanaji wa Internet ulikuwa mgumu. Karibuni tena.

Monday 26 June 2017

EID MUBARAK

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) pampja na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika Ikulu Mjini Unguja leo kumtakia Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wakiitikia Dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibae Sheikh Saleh Omar Kabi,(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi akiongoza Swala ya Eid kuadhimisha sikukuu ya Eid el Fitr
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakichukua Chakula wakati wa hafla fupi ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania na kufanyika ofisi za Bakwata mkoa wa Kilimanjaro

Sunday 25 June 2017

HONGERA RAYVANNY WA WCB

Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) ameshinda tuzo ya BET (Black Entertainment Television) kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’.

Kufuatia ushindi huo msanii Diamond Platnumz ambaye anaiongoza WCB amepongeza ushindi huo wa Rayvanny, amesema kuwa zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu tena kufuatia ushindi huo.

“Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale”

Saturday 24 June 2017

TAARIFA YA SIKUKUU YA EID EL FITR


Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo

Thursday 22 June 2017

SHOPPING ZA EID IMEPAMBA MOTO

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Mfungo wa Ramadhani kuisha, maeneo mengi ya masoko yamejaa wateja wakifanya manunuzi kwa ajili ya kupendeza wakati wa Sikukuu ya Eid.
Nawatakia wote maandalizi mema

WATAKAOPATA MIMBA SHULENI KUKIONA CHA MOTO

Rais John Magufuli amesema wakati wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi) wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.

“Azae halafu aende kuwahubiria wenzake, unajua ilikuwa hivi, halafu nilifanya hivi,”amesema.

Amesema waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya ufundi stadi (Veta) na kilimo badala ya kurudi shule na kuanza kuwafundisha wenzao yale waliyoyafanya.

“Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.

Amesema; “Ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili lakini sekondari, darasa la kwanza kupeleka walio na watoto, tunapoteza maadili yetu, watazaa mno.”

“Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. Hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema

Mhe RAIS MAGUFULI AFUTARISHA KIBAHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kunawa na kisha kuchukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017 katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima mkoani humo

MHE RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA ZA BAGAMOYO/MSATA 64KM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
Daraja la Ruvu Chini katika Barabara hizo za Bagamoyo/Msata

Wednesday 21 June 2017

MHE.RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MATREKTA CHA TAMCO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua kiwanda cha kuunganisha matrekta cha Ursus na kiwanda cha Nondo cha Kiluwa ambapo amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi kwani Serikali iko nao bega kwa bega. "Kiwanda ni kikubwa na kinatoa nondo ambazo zinaweza kujenga daraja lolote Tanzania au Ulaya.Tanzania tuna chuma, kwa nini tuagize chuma kutoka Brazil au China.

Saturday 17 June 2017

BIASHARA YA MKAA BADO IMESHAMIRI

Pamoja na tatizo kubwa la uharibu wa misitu na mazingira, biashara ya mkaa imeendelea kushamiri hasa maeneo ya Mijini.
Hapa chini ni Biashara ya mkaa maeneo ya Kigogo Fresh nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

Thursday 15 June 2017

MAAKULI HAYA YANAKUKUMBUSHA WAPI?

PRECISION AIR KUANZA SAFARI ZA HADI MBUGANI SERENGETI

Shirika la Ndege la Precision Air linatarajiwa kuazia Oktoba 1, 2017 kuanza kutua katika kiwanja cha Seronera ,katika Mbuga kubwa ya Serengeti

Wednesday 14 June 2017

MHE RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA BARRICK

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kulia ni balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles

Tuesday 13 June 2017

MHE RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA ZOTE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na wakuu wa mikoa wote katika kikao kilichohudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 13, 2017

CHEKA KIDOGO

Sunday 11 June 2017

ZANZIBAR YATANGAZWA KWA KUPITIA MABASI HUKO LONDON UINGEREZA

Kwa siku mbili mfululizo sasa mabasi ya jiji la London yamekuwa yakibeba tangazo ya shirika la ndege la Uturuki ambalo linapigia debe kituo chake kipya cha safari ya ndege zake “Zanzibar*.

GOOD NEWS WANAFUNYI MAJERUHI WA LUCKZ VICENT WARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI HUKO U.S.A

BASI LA BATCO LATEKETEA KWA MOTO HUKO MKOANI MARA

Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW likiteketea kwa moto hii leo katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama Mkoani Mara, gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.

MHE MAGUFULI NI RAIS WA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI ITIKADI

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mgwira, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “mkosoaji mwenye faida” na kwamba Rais John Magufuli bado ana nafasi kwa wote wanaomkosoa kwa hoja na si vinginevyo.

Hatua hiyo inatajwa kumweka Magufuli katika taswira ya kukanganya zaidi kwa kuwa tayari amepata kutoa kauli zinazokandamiza siasa za upinzani nchini, ikizingatia kuwa Juni, mwaka jana, alitangaza kusitisha mikutano ya kisiasa akitoa ruksa kwa wabunge pekee hali iliyozua malumbano kati yake na viongozi wa vyama vya upinzani.

Vile vile akiwa Zanzibar, katika mikutano ya hadhara, mwaka jana, alimshangaa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na wapinzani ambao anaamini hawakustahili kuwamo kwenye serikali hiyo.

Lakini kwa sasa Raia Mwema limeambiwa na mmoja wa wandani ya Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam kwamba uteuzi huo si wa mwisho na kwamba Rais Magufuli haamini kwamba kuna watu wameumbwa kuwa wapinzani maisha yao wote.

Hii ni mara ya kwanza kwa mmoja wa wandani wa Rais Magufuli kueleza kinagaubaga kuhusu uteuzi huo wa Mghwira ambaye alikuwa mshindani wa mgombea huyo wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

“Nenda kawaambie Watanzania kwamba Mghwira amechaguliwa kwa sababu ya constructive criticism (ukosoaji wenye hoja) yake. Rais hana shida na wakosoaji wa namna hiyo na siku zote wana nafasi kwa serikali yake.

“Hata Profesa Kitila Mkumbo naye alikuwa anamkosoa Rais Magufuli mara kwa mara lakini bado alimteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Hii ni kwa sababu siku zote Kitila alikuwa akimkosoa kwa haki na kwa hoja.

“Sasa kuna wakosoaji wengine kila siku wanakosoa tu na wakati mwingine wanaweka matusi na kashfa humohumo. Watu kama hawa Rais Magufuli hawezi kufanya nao kazi.

“Na naomba wewe mwenyewe nikupe home work ya kujiuliza nini maana ya mwanasiasa wa upinzani. Je, maana yake ni kupinga kila kinachofanywa na serikali iliyo madarakani?

“Kwa tafsiri ya Rais Magufuli, hakuna mpinzani wa kudumu. Yeye anaamini vyama visivyo madarakani ni vyama mbadala tu kwa CCM na haimaanishi kazi yao ni kupinga tu bila hoja. Ujumbe kwa wanasiasa wote ni kwamba yeye hana ubaguzi na yuko tayari kufanya kazi na wote wenye hoja, Raia Mwema limeambiwa na chanzo chake hicho cha uhakika kutoka Ikulu.

Polepole azungumza

Kwa upande wake, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisisitiza kwamba rais amefanya uteuzi huo kwa kuzingatia kigezi kikuu cha Utanzania wa mteuliwa.

“Ni rais wa Watanzania wote anapofanya uamuzi huzingatia katiba na sheria za nchi. Amepewa mamlaka kikatiba kuteua wasaidizi wake wakiwamo wakuu wa mikoa na wilaya, msingi wa kwanza katika uteuzi ni Utanzania wa watu hao anaowateua na mengine kama uadilifu.

Hizi ni zama za CCM mpya tunatazama uadilifu na kuzingatia watu wenye fikra na mwelekeo sawa na ule wa rais wetu, kuendeleza mapambano ya kuelekea uchumi wa kati ambao kimsingi ndio uchumi wa viwanda.

Rais anapofanya uamuzi hafungwi, kuna maeneo anaelekezwa na kuna maeneo anaachwa afanye kutokana na imani ya wananchi juu yake. Rais anapoteua Watanzania wanaweza kutoka popote kwenye vyama vya siasa au hata vyombo vya ulinzi, kuna askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania amewateua kuwa wakuu wa wilaya kwenye wilaya za pembezoni mwa nchi, hawa bado ni askari walioko kwenye utumishi wa jeshi,” alisema Polepole.

Friday 9 June 2017

ORODHA ZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA SITA NA VYUO VYA UFUNDI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.

Kuangalia majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa
http://tamisemi.go.tz/form_five_selection_or/

FURAHI NA PICHA HII LEO

Thursday 8 June 2017

BAJETI YA SERIKALI 2017/2018 YASOMWA LEO BUNGENI

Wakati Bajeti za Mwaka 2017/18 ikisomwa, tujikumbushe picha za Waziri wa Fedha miaka za 90 Luteni Kanali Jakaya Kikwete akisoma Bajeti
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari. Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli. Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.
Serikali imetangaza kufuta ushuru wa huduma kwenye nyumba za kulala wageni. Hayo yameelezwa leo (Alhamisi) bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango wakati akiwasilisha bajeti kuu ya mwaka 2017/18. Pamoja na ushuru huo, pia Serikali imefuta ushuru wa mabango yanayoelekeza mahali zinapopatikana huduma za kijamii kama vile shule na hospitali.

Tuesday 6 June 2017

MHE MAMA ANNA MGHWIRA AAPISHWA KUWA MKUU WA MKOA WA KNJARO LEO


Leo hii mara baada ya kuapishwa Ikulu ,Mhe Anna Mghwira alikabidhiwa Ilani ya CCM na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ,mbele ya Rais Magufuli na Viongozi Wengine waandamizi wa Serikali na kuagiywa akachape kazi bila kusikiliza maneno ya watu wanaoongea dhidi ya uteuzi wake

Monday 5 June 2017

TUANZE MWANZO WA JUMA KWA UJUMBE HUU

KIVUKO CHA MV.KAZI CHAANZA KUTOA HUDUMA RASMI FERRY- KIGAMBONI


TANZIA: R.I.P Dr.Phillemon Ndesamburo

Alokuwa Mbunge wa Moshi Mjini (CHADEMA)Mhe.Phillemon Ndesamburo amefariki wiki ilopita na mazishi yake kufanyika huko KDC Moshi. Alikuwa mmoja wa waasisi wa Chama cha Upinzani CHADEMA

REAL MADRID WALIVYORUDI NYUMBANI KWA SHANGWE BAADA YA KUTWAA KOMBE LA UEFA

Usiku wa June 3 2017 katika uwanja wa Millenium jiji la Cardiff nchini Wales Real Madrid waliandika historia mpya katika uwanja huo baada ya kufanikiwa kutwaa taji lao la 12 la UEFA Champions League katika historia ya club yao.

Sunday 4 June 2017

KATUNI YA LEO

MHE MAMA ANNA MGHWIRA (ACT) ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

IKULU: Rais Magufuli amemteua Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, mama Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akijaza nafasi ya Said Meck Sadick aliyejiuzulu

Saturday 3 June 2017

WABUNGE WA UPINZANI WASUSIA BUNGE NA KUTOKA NJE

MHE MBUNGE LIVINGSTONE LUSINDE ALICHOONGEA NA KISHA KUZUSHA MJADALA

Mbunge Mhe.John Mnyika atolewa nje ya Bunge kwa amri ya Spika Job Ndugai na kuamriwa kutohudhuria vikao kwa siku 7 baada ya kutokea malumbano leo. Baada ya tukio hilo na wabunge wa upinzani wakaamua kutoka nje

Tuesday 30 May 2017

ALIYEBUNI NA KUCHORA NEMBO ZA TAIFA AFARIKI DUNIA


Mzee Francis Maige Kanyasu maarufu kama "Ngosha" aliyedai kuwa yeye ndiye mchoraji wa nembo ya Taifa amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, leo akiwa na umri wa miaka 86.!

Monday 29 May 2017

UTEUZI WA IGP

Aliyekuwa Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2017 amemteua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa polisi (IGP).