Sunday 31 May 2009

PATASHIKA YA WATOTO OMBAOMBA DAR

HIVI NDIVYO MELI YA MV FATIH ILIVYOZAMA KATIKA BANDALI YA MALINDI ZANZIBAR!!


Kama ilivyokuwa Mv.Bukoba

HAYA SASA !

Bongo kumekucha

YATIA HURUMA NA KUHAMASISHA VILEVILE

Kila mara nitazamapo picha kama hizi nakumbuka jinsi Tanzania tulivyobarikiwa na maliasili nyingi. Ufisadi umekuwa ni tatizo kubwa. Hali kama hii isingepaswa kuwepo kama Serikali yetu ingekuwa makini. Cheche za Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Hari mpya zahitajika sana kubadili hali hii. Angalia watoto wazuri wanavyojitahidi,japo katika hali mbaya hata viatu miguuni hakuna.Serikali inapaswa kuona hili na kuwapa shime kupunguza makali haya.

MISS UNIVERSE TZ 2009


Miss Universe Tz 2009 Illuminata James (kati) akipozi na mshindi wa pili Evelyn Almasi (kulia) na Hidaya Maeda ambaye ni mshindi wa tatu katika kinyang'anyiro hicho hicho huko Mlimani City-Dar

UJUMBE KATIKA KATUNI

Saturday 30 May 2009

KARIAKOO 1971

NYUMBA ZETU

Mfano wa nyumba ya kabila la Wabena

Mfano wa nyumba ya kabila la Wahaya

Friday 29 May 2009

Wednesday 27 May 2009

MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA

Hii ni picha inayoonyesha mwonekano wa jengo litakalojengwa kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za Baba wa Taifa Mwl.Nyerere. Jengo hili litajengwa Mtaa wa Shaaban Robert karibu na Makumbusho ya Taifa Dar-es-Salaam.

Tuesday 26 May 2009

SAFISHA MIKONO KABLA NA BAADA YA KULA

Katika kuimarisha afya ya jamii, kumekuwa na msisitizo wa kusafisha mikono kabla na baada ya kula. Lakini wakati mwingine tunajisahau kama kila mmoja wa familia au jamii anafuata maelekezo haya kisahihi. Picha hii ni changamoto tu.

Monday 25 May 2009

NDOTO YA KIGAMBONI

Hawa ni wenzetu huko China

MSOSI WA LEO

Baada ya kuhangaika labda usiku kucha kuvua samaki, leo jamaa huyu kapata kitoweo cha kutosha. Basi wototo ni furaha tu hapa.
Hawa nao wana lao

KERO YA MAJI - KITETO

Licha ya baraka ya mito na maziwa nchini, bado maji ni kero kwa wananchi wengi kama hii inayowakumba jamii ya kimasai huko Kiteto.

NYUMBANI:TUJIANDAE KATIZO LA UMEME Mei 31


JIJI la Dar es Salaam litaingia kwenye giza nene Mei 31 mwaka huu wakati Shirika la Umeme nchini (Tanesco), litakapozima mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya kampuni ya SONGAS.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imesema mitambo hiyo itazimwa kupisha matengenezo ya kawaida katika njia ya kupitishia gesi kwa siku nzima kuanzia saa 10:00 alfajiri hadi saa 12:00 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kuzimwa kwa mitambo hiyo kutasababisha upungufu wa nishati hiyo kwa megawatti 50 na kusababisha baadhi ya maeneo hayo ya jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.

Maeneo yaliyotajwa kwenye taarifa hiyo kuwa yatakosa umeme ni Wilaya ya Temeke maeneo ya Mwembe Yanga, Tandika Azimio, Tandika sokoni, Kichangani, Temeke Wailes, Temeke Hospital, Maeneo yote ya Yombo, Veternary, Jeje Industry, Petrolube, Tanzania Printers, Metal Product, Kilungule, Tazara flats, Boney M, Vituka, Dovya, Stereo

Wiyani Kinondoni maeneo yatakayoathiri ni Kinondoni Kaskazini maeneo ya M.M.I Steel Industries, Mikocheni B, Kawe Beach, Baadhi ya eneo la viwanda pamoja na kiwanda cha Bidco, Kunduchi Mtongani, Salasala, Baadhi ya maeneno ya barabara ya Africana na viwanda vya Raffia Bag na Family Soap.

Tatizo hilo pia litawakumba wakazi wa Kinondoni Kusini katika maeneo ya Sinza, Manzese, Tandale, Kijitonyama na Mwananyamala.
Taarifa imezidi kueleza kuwa wilayani Ilala umeme hautapatikana katika maeneo ya NSSF Water Front, Tanzania Tea Blenders, Polisi Makao Makuu, TRC, Makao Makuu ya DAWASCO, Keko Mwanga, Mtaa wa Lugoda, Baadhi ya maeneo ya Kariakoo kutokea mtaa wa Msimbazi mpaka Lumumba na Ilala Boma.

Maeneo mengine ni Ilala Sharif Shamba, Ilala Bungoni, Buguruni Malapa, Buguruni Rozana, Buguruni Sokoni, Sehemu ya barabara ya Mandela kuanzia Buguruni mpaka Tabata Dampo, Tabata Liwiti, Tabata Bima, Tabata Mawenzi, Tabata Kimanga na Tabata Kisukuru.

Maeneo hayo ni na Makoka, Kiwalani kwa Gude, Jet Club, Kipawa, Mtaa wa Azikiwe, Mtaa wa Kisutu, Hospitali ya Hindu Mandal, Jengo la Haidery Plaza, Mnazi Mmoja sehemu ya barabara ya Morogoro kuanzia Mtaa wa Kisutu mpaka mtaa wa Samora yatakosa umeme kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 6:00 mchana.

Tanesco imesema umeme utakatika kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 jionii katika Mtaa wa Muheza, Mtaa wa Msimbazi, Mtaa wa Nkrumah mpaka Mtaa wa Samora, Upanga Mashariki, Sea View, Kituo cha Polisi cha Salender Bridge, Mitaa ya Uhuru, Magila, Lumumba, Mahiwa na Livingstone.

Imesema pia umeme utakatika sehemu ya barabara ya Bibi Titi kuanzia barabara ya Morogoro, Ally Hassan Mwinyi, DIT, Business College, Hospitali ya Regency, Viwanda vya Zenufa, Mukwano, Bakhresa, Murzah Oil, Vingunguti, sehemu ya Kiwalani, baadhi ya maeneo ya barabara ya Nyerere kuanzia TAZARA mpaka Metrol Steel Kiwalani, Segerea, Kinyerezi na Bunyokwa.

Hali ya umeme itarejea kama kawaida mara baada ya matengenzo hayo kukamilika," imesema taarifa hiyo na kuwaomba radhi wateja

Sunday 24 May 2009

NJOO TWENDE NYUMBANI

Haya ndo mambo ya usafiri wa nyumbani. Wasafiri wamekaa raha mustarehe.Kweli nyumbani raha!

Saturday 23 May 2009

TRC/TRL BADO TUNAJIKONGOJA

Mojawapo ya treni za mwendo kasi zinazotumia umeme huko UingerezaHii ni treni ya Shirika la Reli Tanzania, hapa ikiwa Morogoro.

MATOKEO YA MLIPUKO WA MABOMU MBAGALA

Wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Maendeleo huko Mbagala Kuu karibu na eneo la mlipuko wa mabomu wakifanya mtihani wa Utamirifu (Mock) hivi majuzi kwa staili hii.Kwakweli hali inatisha maana wanafunzi wanapata elimu kwa taabu sana.Tuendelee kuiomba serikali itupilie macho tatizo hili.

Friday 22 May 2009

Mhe.RAIS KIKWETE(TZ) AKUTANA NA Mhe. RAIS OBAMA (USA)

JK akipokewa na mwenyeji wake Rais Obama wa Marekani katika Ikulu ya White House.JK ni kiongozi wa kwanza wa Afrika kuingia humo tangu Mhe.Obama achukue nchi mwezi Februari mwaka huu.


Picha kwa hisani ya MichuziJr/Jiachie

Dr. HARRISON MWAKYEMBE APATA AJALI YA GARI

Huyu ni Mbunge wa Kyela.Ajali hii imetokea huko Iringa. Tumwombee apate nafuu mapema.Waweza kucheki video yake; nenda kwenye youtube hapo kulia, kwenye search box andika "ajali ya Mwakyembe" ,search waweza kuona.


Wednesday 20 May 2009

OHOOOOOOOOOOOOOO!!!!!

"Sasa nimeingia duniani ,lakini yaelekea maisha ni 'tafu' kweli kweli sijui nitayaweza!"

SPIKA WA BUNGE LA UINGEREZA ATANGAZA KUJIUZULU


Spika wa Bunge la Uingereza Michael Martin ametangaza jana kuwa atajiuzulu tarahe 21 mwezi ujao kutokana na kulaumiwa kwa kushindwa kufanya mageuzi ambayo yangeliwezesha kuepusha kashfa ya gharama za wabunge.

Hii ni mara ya pili kwa Spika wa Bunge la Uingereza House of Commons kujiuzulu katika historia ya nchi hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa miaka 300 iliyopita.
Spika Michael Martin atang'atuka kutokana na lawama kali zilizotolewa baada ya Spika huyo kushindwa kuchukua hatua za kuepusha kashfa ya gharama za wabunge.

Baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo walidai kurudishiwa fedha za gharama zao hata kama walinunua mahitaji kama shuka za nyumbani. Wabunge wengine walidai kurududishiwa fedha mara kadhaa.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph pana wabunge waliodai kurudishiwa fedha za gharama za mabwawa ya kuogelea na gharama zilizotokana na matengenezo ya viwanja vya tennis
Akitangaza kujizulu,Spika Michael Martin amesema ameamua kujiuzulu wadhifa wa Uspika Jumapili ya tarehe 21 mwezi Juni

Wabunge 23 kutoka vyama vyote hawakuwa na imani na Spika huyo.
Kiongozi wa chama cha upinzani David Cameron ambae kwa sasa anaongoza katika kura maoni amesema wananchi wa Uingereza waliokasirishwa sana wanataka zaidi kupatiwa fursa ya kupiga kura kuliko kuondolowa kwa Spika.Uchaguzi wa bunge nchini Uingereza utafanyika mwezi juni mwaka ujao.
Mwandishi/Mtullya Abdu.
Mhariri/ Mohammed Abdul- Rahman

Tuesday 19 May 2009

KARIBU BINTI MACHOZI

Wanablog, karibuni kwenye blog mpya na murua ya Lady Jaydee muone kazi nzuri ya mwanadada mrembo wa nyumbani TZ. Mtembelee hapa www.ladyjaydee.blogspot.com

Monday 18 May 2009

UTAFUTAJI WA ELIMU

Wakati wanafunzi wanajitahidi kutafuta elimu popote ipatikanapo, bado kwa baadhi yao mazingira ya kupata elimu yapo duni sana. Hapa chini yaonyesha bweni la wanafunzi shule moja ya sekondari huko Tanga, ambapo Waziri Mwantumu Mahiza alitoa machozi alipotembelea eneo hilo kujionea hali halisi. Tuwasaidie!
_
Haya ni mabweni mapya na mazuri ya Sekondari ya Baobab ambapo kwa hali hii hata utulivu katika kupata elimu unakuwepo. Tunawapongeza!.

Sunday 17 May 2009

VYOMBO VYA USAFIRI DAR

Vyombo vingine vya usafiri Dar kama matani vile teh teh teh

WAREMBO / MAMISS WETU

Tunapowapongeza warembo wetu kwa namna wanavyojitahidi katika suala la urembo, sio vibaya pia tukijikumbusha uhalisia wa sura zetu za kiafrika. Wanablog hebu tazameni wenyewe tofauti kubwa ionekanayo kati ya mwonekano wa uso na mikonoHawa pia ni Mamiss wetu lakini katika sura zao halisia, nadhani wanapendeza pia, tena zaidi hahahahhaaa

TANZANIA ASSOCIATION - READING


Tanzania Association Reading
Ndugu Watanzania,

Uongozi wa muda wa Umoja wa Watanzania Reading (Tanzania Association Reading) Unapenda kuwatangazia mkutano wa Watanzania wote wa Reading, Berkshire UK, utakaofanyika tarehe 24th May 2009, Community center, Colley Park,140 Winsley road , RG1 6DW, Reading; kuanzia saa tisa mchana hadi saa mbili jioni (3pm – 8pm), vivywaji na vitafunwa vitakuwepo.

Mkutano huu ni muhimu sana kwetu sisi watanzania wa Reading kwa maana utazungumzia yafuatayo:-

a) Uongozi kutoa taarifa ya maendeleo ya ukamilishwaji wa uundaji wa Umoja huu, na taratibu zake hapa Reading.

b) Kupata taaarifa ya ukamilishwaji wa usajili wa Umoja huu, katika vyombo vya dola hapa Reading.

c) Kuiainisha na kuipitisha katiba, na viambatanisho vyake vya Umoja wa Watanzania Reading.

d) Kuelezea umuhimu wa Umoja wa Watanzania Reading na shughuli zake katika kuboresha maisha ya Watanzania hapa Reading na vitongoji vyake.

e) Kupata maoni, marekebisho na ushauri kuhusiana na vipengele a,b,c) hapo juu.

f) Kutoa mapendekezo na kupanga tarehe ya uchaguzi na utaratibu mzima wa uchaguzi wa viongozi wa kwanza wa kudumu wa Umoja huu hapa Reading vitongoji vyake.

g) Kelezea umuhimu wa kujiunga kuwa mwanajumuia hai wa Umoja huu na faida za kuwa mwanajumuiya hai, na maana yake ni nini.

h) Mengineyo

i) Kuweka action plan na majukumu

j)Email ya jumuiya kwa mawasiliano zaidi ni hii tzra2009@googlemail.com

Kufika kwako ndio kufanikisha mkutano huu na maendeleo yetu hapa Reading.

Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na

Mwenyekiti wa muda (H.Chang’a) 07954563709

Makamu mwenyekiti (B. Chisumo) 07876126862

Katibu wa muda (S. K. Buraganya) 07894547323

Katibu(Msaidizi) (PeteR Michael) 07888841971Asante

TA reading

MAN UTD MABINGWA TENA

Timu ya Man Utd imenyakua tena ubingwa wa Premier League huko Uingereza baada ya kutoka sare ya 0-0 na timu ya Arsenal. Timu hii imeukwaa ubingwa huo kwa mara ya 17 sasa. Hongereni mashabiki wa Man Utd.