Wednesday 30 November 2016

KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE CHASITISHA UZALISHAJI KWA MUDA

UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umesimama kwa muda kutokana na hitilafu za kiufundi zilizojitokeza katika mitambo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Harpreet Duggal alisema jana kwamba mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea katika siku chache zijazo.

Alisema kiwanda kinachomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote wa Nigeria kilianza uzalishaji wa kibiashara mwaka huu na kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho, jambo lolote linaweza kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo.


Alisisitiza, “hitilafu hizi ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho.”

Akizungumzia gharama za uzalishaji, Duggal alisema uendeshaji nchini uko juu huku miongoni mwa sababu ikiwa ni matumizi ya jenereta za dizeli katika kuendesha kiwanda.

Hata hivyo, alisema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kuwapunguzia mzigo.

MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ

Hakuna ubishi kuwa Princess Tiffah ndiye mtoto maarufu zaidi Afrika kwa sasa.
Umaarufu wake unazidi kuongozeka kiasi ambacho wiki hii amefikishafollowers milioni 1 kwenye mtandao wa Instagram.


Ila katika nchi hii hii wapo watoto wengine wanaishi hivi

Tuesday 29 November 2016

NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA BRAZIL YAPATA AJALI

Habari za kusikitisha katika ulimwegu wa soka ni kwamba, klabu ya Chapecoense ya Brazil imepata ajali baada ya ndege iliyokuwa imebeba wachezaji pamoja na viongozi kuanguka kwenye mji wa Medellin, Colombia.Chapecoense ilikuwa imefika hatua ya fainali ya Copa Sudamericana, ambayo ni sawa na Europa League kwa Ulaya na walikuwa wanaelekea Medellin kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa fainali dhidi ya Atletico Nacional siku ya Jumatano.
Habari za hivi punde zaeleza kuwa abiria 71 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki ila kuna wachache wanaosadikiwa 6 walionusurika kifo

MARAIS WA TANZANIA NA ZAMBIA WAAZIMIA KUBORESHA ZAIDI TAZARA NA TAZAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu tarehe 28 Novemba, 2016 wamekubaliana kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuboresha utendaji kazi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA ili miradi hiyo miwili ilete manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi Tanzania na Zambia.

Monday 28 November 2016

MBEYA YA PILI AFRIKA KWA WINGI WA MADHEHEBU

Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.

Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.

Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.

“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo

UGENI WA MARAISI WAWILI NCHINI TANZANIA WIKI HII

Rais Magufuli leo amepokea Marais wa Mataifa mawili ya Tchad na Zambia kwa mialiko ya ziara za kikazi.Rais wa Chad Idriss Deby atakuwepo nchini kwa siku mbili katika ziara ya Kikazi; wakati rais wa Zambia mhe. Edgar Lungu atakuwepo kwa siku 3

Sunday 27 November 2016

KAMPUNI YA MURO KUUZA MABASI NA MALI ZAKE NYINGINE

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la nyumba kipigwa mnada, viwanja, magari, hoteli na mali mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni baadhi wa wakopaji kushindwa kurejesha fedha za mikopo walizochukua kutoka katika taasisi za kifedha.

Mbali na kupigwa mnada, baadhi ya hoteli na kumbi nyingine zimebadilishwa matumizi ambapo nyingi zimefanywa hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo huku nyingine zikibadilishwa na kuwa shule na vyuo wakati wamiliki wengine wakiamua kuzifunga au kupunguza idadi ya wafanyakazi.

Kampuni ya Muro Investiment Co. Ltd inayomiliki mabasi ya safari za mikoani na vituo vya kuwekea mafuta imetangaza kuuza mali hizo. Kampuni hiyo haikueleza sababu za kuuza mali hizo.

Hili hapa chini ndilo tangazo la kampuni hiyo likielezea mali zinazouzwa.

Saturday 26 November 2016

RAIS WA ZAMANI WA CUBA; FIDEL CASTRO AFARIKI DUNIA

Rais wa zamani wa Cuba na kiongozi wa mapinduzi ya kikomunisti, Fidel Castro amefariki akiwa na umri wa miaka 90, mdogo wake Raul ametangaza.

Amefariki usiku wa saa nne na dakika 22, kwa mujibu wa Rais Raul Castro.

Fidel Castro aliiongoza Cuba kama nchi ya chama kimoja kwa takriban miaka 50 kabla ya Raul kushika madaraka mwaka 2008.

Mazishi yake yanafanyika Jumamosi hii kwa mwili wake kuchomwa moto. Kutakuwepo na siku kadhaa za maombolezo ya nchi nzima.
Siku chache zilizopita akiwa anaongea na waandishi wa habari walofika kumsalimu aliwatabiria kwamba atakufa siku si nyingi na yawezekana hiyo ndo hotuba yake ya mwisho

WATOTO HAWA WAMEIGA AU KUJIFUNZA WAPI HAYA?

Tuwaonyeshe watoto mifano mema ili kuwajengea kesho nzuri

AUDIO: MHE RAIS MAGUFULI AKIONGEA NA SIMU NA RC WA DAR MHE PAUL MAKONDA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. Rais Magufuli ambaye alimpigia mkuu huyo wa mkoa wakati alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi katika Kata ya Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili ambako aliweza kumsisitiza kuwa aendelee kutumbua watu huko huko aliko.

Friday 25 November 2016

TANZANIA YA VIWANDA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alianzia ziara yake kwa kukagua uendeshaji wa Kiwanda wa cha tambi cha TanzaniaPasta, kilichopo eneo la Viwanda, Vingunguti wilayani Ilala. akizungungumza alipongeza hatua ya kuanzishwa kiwanda hicho akisema kinachangia lengo la Rais John Magufuli la kutaka Tanzania ijayo kuwa ya viwanda kwa lengo la kukuza nakuimarisha uchumi wa Taifa.
Hata hivyo aliutaka uongozi wa Kiwanda hicho kuhakikisha kinatimiza masharti ya utunzaji mazingira ikiwa ni pamoja na kutotiririsha maji hovyo, na pia kuhakikisha wananchi waliokusudiwa kulipwa ili kuondoka karibu na kiwanda wanafanyiwa hivyo mapema.
Pia aliwaasa wananchi kusisitiza watoto wao kusoma masomo ya sayansi kwa kuwa kazi nyingi za viwandani zinafanywa na masomi wa somo hilo, na kwamba vinginevyo atakaoajiriwa bila kuwa na elimu ya sayansi watabaki kuwa waokota maboksi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akigangua viwanda vya Paper Kraft kilichopo na cha Tanzania Tooku vilivyopo Mabibo Extenal leo jijini Dar es Salaam

Tuesday 22 November 2016

Monday 21 November 2016

MBUNGE WA ZAMANI WA NCCR MAGEUZI HUKO KIGOMA AHAMIA CCM

Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake


Saturday 19 November 2016

MHE MAALIM SEIF AAZIMIA KUFUTA NYAYO ZA LIPUMBA KUSINI MWA TANZANIA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kuzuru mikoa ya Kusini mwa Tanzania katika kipindi ambacho bado kuna sintofahamu kuhusu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho.

Mwanasiasa huyo ambaye ataongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya chama hicho, Julius Mtatiro pamoja na Wajumbe wa Baraza Kuu watazuru Mtwara na Lindi ikiwa ni miezi michache baada ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kuzuru eneo hilo la kusini.

Akizungumzia ziara hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma wa chama hicho, Mbarala Maharagande alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli za chama na kupokea maoni ya pamoja ya namna ya kuboresha utendaji wa chama hicho kwa ngazi za chini.

Maalim Seif anatua katika eneo hilo wakati ambapo kukiwa na mvutano baada ya baraza la madiwani kufanya jaribio lililoshindikana la kumng’oa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Geofrey Mwanchisye.

Jaribio hilo liligonga mwamba baada ya Mwanasheria wa Halmashauri hiyo, Sifaeli Kulanga kueleza kuwa hoja zao hazina msingi kwani tuhuma zao kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma yanakinzana na ripoti ya kamati maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Kesi kuhusu Uenyekiti wa chama hicho inaendelea Mahakamani ambapo Baraza Kuu la chama hicho linapinga barua ya Msajili inayomtambua Lipumba kama Mwenyekiti wa chama hicho wakati ambapo Baraza hilo lilikuwa limetangaza kumfuta uanachama.

Thursday 17 November 2016

MALEZI KWA VITENDO YANA MATOKEO MAZURI ZAIDI

Sijui ni kwa kiasi gani umeweza kuwapa picha na mtazamo bora wa maisha hao watoto wako. Usisahau kwamba wao wanajifunza kwa asilimia 70 kutoka yale wanayokuona ukiyafanya na asilimia 30 tu kwenye yale unayoongea. Ukiongea na kufoka sana pasipo kuwaonyesha matendo watatoka kapa:
Tuwaonyeshe watoto mifano bora.
Mhe Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama na watoto wake Malia na Sasha

Monday 14 November 2016

VYOO 100 KUJENGWA KWA AJILI YA WASAFIRI BARABARA YA MWANZA/SHINYANGA/DAR

Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD& CF), inatarajia kujenga vyoo 100 katika Barabara Kuu ya Mwanza-Shinyanga-Dar es Salaam unaokadiriwa kutumia Sh. milioni 500.

Mwenyekiti wa TD & CF, Alhaji Sibtain Meghjee alisema hivi karibuni mjini Mwanza kwamba mradi huo ni sehemu ya miradi mitatu mikubwa ambayo taasisi yake inatekeleza nchini.

Alisema baada ya kukamilisha mradi mkubwa wa jengo la kupumzikia wananchi wanaokwenda kutibiwa na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure wanatarajia kujenga vyoo 100 kwenye barabara ya kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kwa basi.

Meghjee alieleza kuwa maandalizi ya awali ya mradi huo yameshaanza na kwamba watashirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ili kupata taarifa sahihi kabla ya mradi kuanza.

“Penye nia pana njia, baada ya kukamilisha ndoto yetu, leo ya mradi huu mkubwa wa ujenzi wa jengo la kupumzikia hapa Sekou Toure, tunatarajiwa kutekeleza miradi mitatu mikubwa ukiwemo wa vyoo kwa ajili ya abiria wanaosafiri kati ya Mwanza na Dar es Salaam:

“Tunataka msamiati wa kuchimba dawa wakati wa safari ubaki kuwa historia kwa hiyo tunatarajia kufanya jaribio moja la kujenga matundu 100 ya vyoo katika njia na barabara kuu ya Mwanza hadi Dar es salaam ambavyo vitagharimu shilingi milioni 500.Tutashirikiana na mamlaka husika, ofisi yako na idara ya afya,”alisema Meghjee.

Meghjee alieleza kuwa taasisi hiyo pia ina mpango wa kutekeleza mradi wa kutengeneza viungo bandia kwa kushirikiana na kitengo cha Jairpur Foot/Knee and Limb Project cha India ambao unahitaji Dola 200,000 za Marekani (sh. milioni 44), zitakazowezesha kuanzisha huduma ya viungo hivyo bandia vya miguu, mikono, fimbo na baiskeli.

Alisema wanaendelea kuwasiliana na wafadhili watakaoshirikiana nao kwenye mradi huo na kuwahakikishia walengwa kuwa viungo hivyo vitapatikana kwa gharama nafuu mara utakapokamilika mradi huo.

Meghjee aliongeza kuwa wakati wakiendesha ujenzi wa jengo la mapumziko katika Hospitali ya Sekou Toure,walipata wazo la kujenga mabanda yatakayotumiwa na madereva wa pikipiki (boda boda) kuegesha vyombo vyao kivulini na kupata huduma ya vyoo na mabafu.

Mwenyekiti huyo wa TD & CF aliongeza zaidi kuwa endapo Halmashauri ya Jiji itaridhia na kuwapa eneo maalumu na mahususi la ujenzi wa huduma hiyo watafanya jaribio hilo moja ili kuweza kuona matunda yake.

MHE RAIS TRUMP WA MAREKANI NA FAMILIA KATIKA UBORA WAO

Saturday 12 November 2016

VIDEO: THE BEST OF OBAMA'S PHOTOS

Katika kipindi cha miaka 8 ya urais wake nchini marekani, Mhe Barack Obama alipiga picha zaidi ya milioni 2, hapa nakuwekea clip ya picha zake zilizovutia wengi kwa namna alivyokuwa mtu wa watu wote.

MCHAGUA JIKO SIO MPISHI

Hii nadhani wengi wetu tumepitia na bado tunaendelea kutumia hasa uwapo sehemu kama vile mstuni kwa matembezi. Vyombo kama hivi ni muhimu sana kuwa navyo vipo vingi sana SIDO tena ni imara zaidi kuliko plastiki.
((Picha na maelezo kwa hisani ya ruhuwiko.blogspot.com))

Friday 11 November 2016

MAREKANI BAADA YA UCHAGUZI WA RAIS

HOSPITALI YA "THE JAKAYAKI KWETE CARDIAC INSTITUTE" YAUNGANISHIWA INTERNET WIFI YA BURE NA TTCL

MAREHEMU SAMWEL SITTA AAGWA DAR NA DODOMA,KISHA KUSAFIRISHWA URAMBO TABORA KWA MAZISHI

Mhe Rais Magufuli akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Samwel Sitta katika viwanja vya Karimjee Jijini dar leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Novemba 11, 2016.
Mwili wa marehemu Samwel Sitta ukiwa Bungeni Dodoma kuagwa

Wednesday 9 November 2016

MHE DONALD TRUMP RAIS MPYA WA MAREKANI

Mgombea wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda uchaguzi mkuu wa Marekani baada ya kufikisha kura 276 huku Hillary Clinton akiwa na kura 218.

Hillary Clinton amempigia simu Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump na kumpongeza kufuatia ushindia huo alioupata.

Akizungumza na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Trump amewataka raia wote wa Marekani, waliomchagua na ambao hawakumchagua kuungana na kuanza kuijenga nchi yao kwani muda wa kampeni na siasa za kugawanyika umekwisha.

HOT NEWS; WAMAREKANI WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS MPYA

Donald Trump na Hillary Clinton wagombea katika uchaguzi wa urais Marekani, Novemba 8, 2016.
Wananchi wa Marekani watapiga kura leo Jumanne kumchagua rais wao, ambaye atamrithi Rais Barack Obama. Wagombea katika uchaguzi huo ni Donald Trump wa chama cha Republicana na Hillary Clinton wa chama cha Democratic.
Uchaguzi huu umekua na ushindani mkubwa tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mpaka siku ya leo ya uchaguzi watu wameendelea kutoa tathmini zao kuhusu nani ataibuka mshindi.
Awali wagombea hawa wawili walionekana katika mijadala kwenye runinga wakitupia vijembe na kila mmoja kumshutumu mwengine kwa makosa aliyofanya kwamba hana hadhi ya kuliongoza taifa la Marekani.

TANZIA TENA: ALIYEWAHI KUWA WAZIRI WA ELIMU JOSEPH MUNGAI AMEFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa waziri wa Elimu Tanzania Joseph Mungai amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Monday 7 November 2016

SIMANZI: SPIKA WA BUNGE MSTAAFU MHE SAMWEL SITTA AFARIKI DUNIA

Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.

Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo.

‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima."

Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye.

Sitta alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na pia mbunge wa Urambo Mashariki.

Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.

Alikuwa miongoni mwa wanachama zaidi ya 42 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana.
Mhe Rais Magufuli alipoenda kumjulia hali Mzee Sitta alipokuwa anaumwa

Sunday 6 November 2016

UDAKU WA LEO

Pale unapoanza shule upya baada ya vyeti kuthibitishwa ni feki

Saturday 5 November 2016

MHE DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATIMIZA MWAKA MMOJA WA URAIS

Leo na mimi nipaze sauti yangu imfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa Mafanikio Makubwa aliyoyapata ktk kipindi cha Mwaka mmoja wa utawala wake tangu aingie madarakani mnano Novemba 05, 2015.

Rais Magufuli kwa kiasi kikubwa amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma. Leo ofisi nyingi za utumishi wa umma zina nidhamu ya hali ya juu sana, watu wanatambua vizuri nini wanapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya ktk Utumishi wao. Huduma zenye kukidhi matakwa ya wananchi zimerejea.

Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali kwa kuzuia na kufuta matumizi yasiyokuwa ya lazima kama safari za nje ambapo ktk kila safari kwa sasa ni lazima Ikulu ibariki kwa kutoa Kibali na kuruhusu idadi ndogo tu ya watu na mara nyingine mabalozi kuiwakilisha Tanzania, kuondoa posho zisizo za lazima n.k

Rais Magufuli alielekeza fedha mbalimbali ambazo zilitengwa kwa matumizi Maalum Mfano Fedha kwa ajili ya Semina kwa Baraza la Mawaziri, Fedha kwa ajili Sherehe ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Uhuru - 09 Desemba 2015 n.k Mh. Rais alielekeza zikafanye Shughuli za Kimaendeleo ikiwemo kununua Vitanda vya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutengeneza Madawati kwa ajili ya Shule za msingi ili kuboresha Elimu.

Rais Magufuli alituahidi endapo atachaguliwa Elimu ya msingi na Sekondari itakuwa ni BURE ambapo ametimiza sasa Elimu kwa Shule za Msingi na Sekondari ni BURE kabisa.

Rais Magufuli aliahidi atafufua Shirika la Serikali la Ndege la ATCL kwa kununua Ndege Mpya ambapo tayari Mheshimiwa Rais ametimiza Ahadi yake kwa Kununua Ndege Mbili Mpya na leo ameahidi kutuletea Ndege Kubwa aina ya Boeing yenye uwezo wa Kubeba abiria zaidi ya 240 ili kukuza uchumi wa Nchi kupitia Sekta ya Utalii.

Rais Magufuli amefanikiwa kusimamia ipasavyo Ukusanyaji wa Mapato ya serikali na Kudhibiti Matumizi yake. Hongera pia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais ktk hili.

Rais Magufuli alituahidi kupambana na Ufisadi na Kuendeleza Vita dhidi ya Wala Rushwa kwa Kuanzisha Mahakama ya Kushughulikia Ufisadi na Rushwa na tayari mahakama ya Kushughulikia Ufisadi & Rushwa inaishi na leo naamini imesikiliza Kesi moja.

Rais Magufuli ameendelea kuboresha barabara kwa Kukijenga kwa Kiwango cha lami mfano kama ile ya Mwenge Dar es Salaam & Mwanza.

Mheshimiwa Rais aliahidi kuhamishia Serikali yake Makao Makuu ya Tanzania Mjini Dodoma na tayari amekwisha anza kutekeleza kwa kuhamisha Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara mbalimbali.

Rais Magufuli aliahidi kukuza Uchumi wa Nchi yetu kwa kuifanya Tanzania ya Viwanda na wote tumeshuhudia Juhudi za Mheshimiwa Rais za Kutafuta wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili yawekeze nchini.

Ndugu zangu yako Mengi sana aliyofanya Rais Magufuli mwenye macho haambiwi tazama ila naomba niishie hapo. Ijapokuwa Bado Changamoto ni nyingi na watu wataona Maisha yamekuwa magumu lakini tutambue na kuelewa hali hiyo haina budi kuja kwani Nchi iko katika kipindi cha Mabadiriko ya kiuchumi kitaalamu tunaita " TRANSITION PERIOD " ambapo kutokana na Juhudi za Mheshimiwa Rais kuujenga uchumi wa Nchi yetu ni lazima mwanzoni tutaona Mabadiriko fulani fulani hivyo Watanzania wenzangu tuvute subira kwa maisha Mazuri yaja. Tumpe nafasi Mh. Rais apambane kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yetu na sisi kwa nafasi zetu tumpe ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa Bidii sana.

Ama Kwa Hakika Rais wetu anastahili pongezi nyingi sana na Mimi Robert PJN Kaseko Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha nichukue nafasi hii kukupongeza Rais wangu na Mwenyekiti wangu CCM Taifa Mh. DKT. John Pombe Magufuli kwa kutuletea Maendeleo makubwa na Mabadiriko ya kweli kwa kipindi cha Mwaka mmoja tunashirikiana toka tukuchague utuongoze, Mabadiriko ambayo kiukweli sisi Wananchi wa Tanzania tulisubiri kwa Muda mrefu sana na nizidi kukutia moyo Mh. Rais usirudi nyuma endelea mbele tunatambua vikwazo ni vingi na Kazi ni ngumu lakini namuomba Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu, akupe afya njema na ulinzi wake ili uendelee vyema kuwaletea Maendeleo Wananchi wako maana wewe ni Mchapa Kazi Kwelikweli tunakufahamu vizuri. HAPA KAZI TU. CCM Hoyeeeeeee.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
November 04, 2016.