Sunday 31 May 2015

CHUO KIKUU KISHIRIKI MARIAN BAGAMOYO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, kwa pamoja wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, baada ya uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian mjini Bagamoyo,leo Mei 31, 2015

WANACCM WALOTANGAZA NIA YA KWENDA IKULU

Mhe. Steven Wasira
Waziri-wa-Nchi-Ofsi-ya-Rais-Steven-Wasira-akihutubia-kwenye-Uwanja-wa-Community-Cetre-Mwanga-Kigoma
Mhe.Lowassa huko Arusha jana
Mhe. Lameck Mwigulu Nchemba kutangaza nia leo huko Chuo cha Mipango Dodoma

HOTUBA YA MHE. LOWASSA HUKO ARUSHA

EL


MHE.LOWASSA ATANGAZA NIA AKIWA ARUSHA

Gari lililombeba Mhe. Edward Lowassa likiingia katika uwanja wa Shekh Abeid Karume huko Arusha
Mtangaza nia akiwapungia wananchi mkono wakati akiwasili katika Uwanja wa Karume huko Arusha
Mtangaza nia akiwahutubia wananchi

Friday 29 May 2015

SERIKALI YAMKOMALIA MWANAMUZIKI SHILOLE

Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Akizungumza bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
“Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia

FIFA: JOSEPH SEPP BLATTER ACHAGULIWA TENA RAIS

FIFA imemchagua tena Mhe.Sepp Blatter kuwa Rais wa FIFA baada ya mpinzani wake Prince Ali kujiengua dakika za mwisho. Blatter anaishika nafasi hiyo kwa mara ya Tano mfululizo tangu aingie katika ngazi hiyo ya Uongozi mwaka 1998.

Sepp Blatter ametangazwa mshindi wa kiti cha urais wa Shirikisho la Soka Duniaani FIFA kwa mara ya 5 mfululizo baada ya kupata kura 133 dhidi ya 73 za mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa msindi, Blatter amesema anajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo kuanzishwa kwa mchezo wa soka la ufukweni (Beach Soccer).

“Tumefanikiwa kuanzisha Beach Soccer na sasa mchezo huo unachezwa kote duniani”
Akizungumzia umri wake, Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesema kuwa umri mkubwa hauwezi kumzuia mtu kutimiza majukumu yake, na hivyo kwake umri siyo tatizo.
Tanzania imewakilishwa na Rais wa TFF Jamal Malinzi ambaye tayari alikwisha tangaza msimamo wa Tanzania kuwa ina muunga mkono Sepp Blatter, kwa maana hiyo bila shaka kura yake ni miongoni mwa kura 133 alizopata Blatter.

Kwa upande wa mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein amekubali matokeo na kutangaza kujitoa baada ya awamu ya kwanza ya upigaji kura

RAIS MPYA WA NIGERIA MUHHAMADU BUHARI AAPISHWA LEO

Nchi ya Nigeria leo imemwapicha Rais mpya wa kwanza kutoka Chama cha Upinzani kuingoza Nchi hiyo
Mhe Rais aliyemaliza muda wake Goodluck Jonanathan akimpongeza mhe Rais Buhari mara baada ya kuapishwa leo.
Makamu wa Rais Wa Tanzania mhe. M. Bilal akiwasil nchini Nigeria kugusdhuria sherehe za kumuapisha Rais Buhari.
Rais alomaliza muda wake Goodluck Jonathan akimwonyesha Rais mpya Buari mazingira ya Ikulu

KWA WAPENZI WA SOKA LA UINGEREZA

KUTANGAZA NIA ZA KUGOMBEA URAIS 2015

KUTOKA "TEAM LOWASSA"

Maandalizi ya eneo hilo atakalohutubia Mhe.Lowassa hapo kesho

WATU ZAIDI YA 1000 WAFARIKI KWA JOTO NCHINI INDIA

Watu zaidi ya 1000 wamepoteza maisha mpaka sasa nchini India kufuatia hali ya joto kupanda mpaka nyuzijoto 50.

Thursday 28 May 2015

ORIJINO KOMEDI WAKABIDHIWA MATREKTA

Mwigizaji wa Orijino Komedi Mjuni Silvery (Mpoki) akikabidhiwa Trekta na Fundi Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Bw.Yunusu Nsekela Jijini Dar es Salaam leo

MAGAZETI HABARI ZA URAIS TUPU

MAISHA NI KUSAIDIANA,VINGINEVYO NAMNA HII HATUFIKI MBALI

Wednesday 27 May 2015

NAMNA HII TUTAFIKA KWELI?

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU: MAJIMBO YA MBEYA MJINI NA VIJIJINI KUGAWANYWA

KIKAO cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya ya Mbeya, jana kilikaa na kupitia mapendekezo ya kuyagawa majimbo mawili ya Mbeya na kuwa majimbo manne ya uchaguzi kwa mwaka 2015.

Kikao hicho kiliwahusisha madiwani, wanasiasa, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na vyombo vya habari.

Katika kikao hicho, wajumbe walikubaliana kuyagawa majimbo hayo ambayo ni Jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Joseph Mbilinyi (Chadema). Kwa mujibu wa mapendekezo, jimbo hilo litagawanywa na kuwa na majimbo ya Iyunga na Sisimba.

Mapendekezo hayo yanataka Jimbo la Iyunga liundwe na kata zote 21 za Tarafa ya Iyunga ambayo ina jumla ya wakazi wapatao 327,122.

Jimbo la Sisimba, litakuwa na kata 15 zilizopo Tarafa ya Sisimba yenye wakazi wanaokadiriwa kuwa 106,264.

Pamoja na idadi ya watu, vigezo vingine vilivyotumika kuyagawa majimbo hayo ni pamoja na jiografia ya tarafa hizo kwa kuwa Tarafa ya Sisimba imezungukwa na milima na mabonde.

Kwa upande wa Halmashauri ya Mbeya, mapendekezo yaliyopo ni kugawa Jimbo la Mbeya Vijijini linaloongozwa na Mchungaji Lacksoni Mwanjale (CCM).

Mapendekezo yaliyopo yanataka jimbo hilo ligawanywe ili lipatikane Jimbo la Mbeya na Jimbo la Isangati.

Jimbo la Mbeya, litaundwa na kata 11 za Tembela, Inyala, Itewe, Njombe, Maendeleo, Igoma, Ilungu, Ihango, Lwanjilo, Ulenje na Swaya zenye wakazi 107,349.

Jimbo la Isangati litakuwa na kata 15 za Masoko, Ilembo, Izyira, Iwiji, Isuto, Bonde la Songwe, Iwindi, Igale, Santiliya, Iyunga Mapinduzi, Itawa, Utengule Usongwe na Nsalala zenye wakazi 221,480.

Akizungumza baada ya kufungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa, alisema mgawanyo wa majimbo hayo umepita katika vikao mbalimbali vya kisheria.

MHE. RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAALIMU TANZANIA (UWT)

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Chama Cha Waalimu TANZANIA( CWT) uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto nje kidogo ya mji wa Arusha jana.Wakati wa mkutano huo wanachama wa CWT ulitarajia kuwachagua viongozi wapya wa chama Hicho.Akizungumza katika mkutano huo Rais Kikwete ameahidi kutatua changamoto moto mbalimbali zinazowakabili waalimu nchini(picha na Freddy Maro

TUZO ZA BBC: MCHEZAJI BORA WA KIKE WA MPIRA WA MIGUU


Mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Wanawake ya Liverpool, Asisat Oshoala ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa mwaka.
Oshoala, mwenye umri wa miaka 20 ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo mpya kutoka BBC World Service,kwa kura zilizopigwa na wapenzi wa kandanda duniani.
Mwanadada huyu amemuangusha Veronica Boquete wa Uhispania na Nadine Kessler wa Ujerumani,Scot Kim Little na Marta wa Brazil.
"ninapenda kutoa shukrani zangu kwa BBC,mashabiki wangu duniani na kila mmoja aliyepiga kura" alisema.
Tuzo hii ni ya kwanza kufanyika na Shirika la utangazaji la kimataifa.
Oshoala, ambaye ni mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kati ya wapinzani wake, alikuwa mfungaji bora na alipigiwa kura wakati wa michuano ya kombe la dunia la wachezaji wa umri wa chini ya miaka 20 nchini Canada kipindi cha majira ya joto kilichopita.
Jitihada zake ziliifikisha Nigeria katika hatua ya Fainali ambapo ilikutana na Ujerumani, ambapo Ujerumani ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Nigeria.
Pia alitoa mchango mkubwa katika timu ya wanawake ya Nigeria katika kutwaa ushindi wa kombe la mabingwa Afrika kwa wanawake mwezi Oktoba.
Hatua hiyo imeiwezesha Nigeria kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa wanawake nchini Canada inayoanza tarehe 6 mwezi Juni

Tuesday 26 May 2015

WALIKOTOKA NI MBALI MHE.RAIS KIKWETE NA MHE KINANA

Ndugu Jakaya Kikwete na Abdulrahman Kinana, siku ya kuhitimisha na kustaafu utumishi wao kwa JWTZ, Oktoba 1992. Hii ilikuwa ni miezi mitatu tangu kutangazwa kuanza rasmi kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania, Jumatano Julai 1, 1992

MAGAZETINI LEO

CHELSEA MABINGWA BARCLAYS PREMIER LEAGUE 2014/15

Monday 25 May 2015

RAIS AFANYA UHAMISHO WA WAKUU WA WILAYA

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.
Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu, 2015.
Wakuu wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Dkt. Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma, Agnes Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.
Wengine ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro John Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam

CCM YATANGAZA MASHARTI KWA WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI KWA UCHAGUZI UJAO

*Mbwembwe,sherehe marufuku
*Idadi ya wadhamini, mikoa sasa yaongezwa
*Wajumbe NEC, marufuku kudhamini wagombea
Chama cha Mapinduzi(CCM), kimetangaza rasmi ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya urais, huku kikitoa masharti magumu kwa wanaotaka kuwania urais kupitia chama hicho.
Chama hicho kimetoa msimamo wake kuwa wagombea wanatakia kuheshimu kanuni na misingi ya chama hicho na ni marufuku kwa wagombea kufanya mbwembwe, madoido na kukodi watu kwa ajili ya kukushangilia wakati wa kuchukua fomu au kurudisha ni marufuku.
Akitangaza uamuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu(NEC) ya chama hicho, leo mjini Dodoma,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema fomu ya kugombea urais itaanza kutolewa Juni 3 mwaka huu na kuzirudisha Julai 2 mwaka huu saa 10 jioni.
Amesema kuanzia Juni 3 wanaruhusiwa kuanza kuchukua fomu na kuzirudisha Julai 2 mwaka huu. Wakishachukua fomu watafanya kazi ya kutafuta wadhamini mikoani.
Amesema mwaka huu idadi ya wadhamini imeongezeka kutoka wadhamini 250 hadi wadhamini 450 huku idadi ya mikoa nayo ikiongezeka kutoka 10 hadi 15.
Nape amesema kuongeza kwa wadhamini hao ni kutokana na idadi ya wanachama wao kuongezeka na wakati huo huo mikoa nayo imeongezeka.Hivyo lazima wagombea waende kwenye mikoa hiyo ambapo mikoa 12 kwa Tanzania Bara na mikoa mitatu Zanzibar na moja ya mkoa uwe Pemba au Unguja.
Amesema moja ya sharti ni kuhakikisha wadhamini wa mgombea mmoja wa ngazi ya urais hawatakiwi kuwa wadhamini wa mgombe mwingine .Hivyo kila mdhamini mmoja anatakiwa kumdhamini mgombea mmoja na si zaidi.
“Tumekubaliana kwenye NEC mwanachama mmoja anatakiwa kumdhaminni mgombea mmoja tu.Haitaruhusiwa mwachama mmoja kuwadhamini wagombea wawili.
Pia amesema wakati wa kuchukua fomu na kurejesha ni marufuku mgombea kufanya mbwembwe za aina yoyote huku akifafanua ni muhimu wagomba kusoma kanuni na kuzielewa mapema.
Kwa mujibu wa Nape ni kwamba vikao vya uchuchaji ni kwamba Kamati ya Maadili na Usalama itachuja majina ya wagombea urais Julai 8 mwaka huu, Kamati Kuu(CCM) itachuja majina Julai 9 mwaka huu na Halmashauri Kuu nayo itapitisha jina la mgombea Urais Zanzibar.
Wakati kwa jina la mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jina litapitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu Julai 11 mwaka huu mjini hapa.
Alisisitiza wagombea urais wanatakiwa kuheshimu kanuni za chama hicho katika mchakato mzima wa kuchukua fomu, kurudisha na hata wakati wa kutafuta wadhamini na mwaka huu masharti yameongezeka kidogo likiwemo la idadi ya wadhamini na wagombea kuhakikisha hawakiuki kanuni za maadili.
“Sharti ambalo limetolewa na NEC ni kwamba marufuku wajumbe wa NEC na Kamati kuu kuwadhamini wagombea urais kwani wao ndio watakaopitisha jina la mgombe, hivyo hawatakiwi kua sehemu ya wadhamini.
Kuhusu kuchukua fomu ya udiwani, ubunge na uwakilishi, Nape amesema fomu zitaanza kutotolea Julai 15 mwaka huu na kurudishwa Julai 19 mwaka huu wakati mikutano ya kempeni itaanza Julai 20 hadi Julai 31 mwaka huu.
Nape alisema kura ya maoni itafanyika Agosti 1 mwaka huu wakati wabunge wa viti maalumu nayo itakuwa Julai 15 mwaka huu na kurudisha fomu Julai 19 na kufafanua uchujaji wa majina utafanywa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake(UWT), Taifa licha ya kwamba mchakato wake utapita Baraza la Vijana.
Kwa upande wa gharama za fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chama hicho,Nape alisema fomu ya kugombea urais itakuwa sh.milioni moja, wakati fomu ya kugombea ubunge ni sh.100,000 na fomu ya udiwani sh.50,000

MHE.MWIGULU NCHEMBA AJIUZULU WADHIFA WA NAIBU KATIBU MKUU CCM

Sunday 24 May 2015

RAIS KIKWETE ATOA ANGALISHO CCM UCHAGUZI MKUU OKTOBA


Wajumbe wa NEC wakiwa katika kikao Mjini Dodoma