Saturday 31 May 2014

NYOTA NJAMA HUONEKANA ASUBUHI

Watoto hawa japo wanaanza katika mazingira magumu lakini wakikuza vipaji vyao watakuwa wasanii wazuri sana baadae. Tuwape moyo na panapowezekana tuwasaidie kufanikisha ndoto yao.

FANYENI KAZI BILA KUCHOKA

Pamoja na kwamba weekend imefika, bado ni muda wa kupambana na maisha maana kila siku mpya maisha yanazidi kuwa magumu hasa kwa wenye kipato kidogo

TUJIKUMBUSHE MAKABILA YA WATANZANIA

Tanzania ina zaidi ya Makabila 120 katika mikoa yake. Ila Tumshkuru Mwl.Nyerere kwa kutuunganisha Watanzania kwa kutumia na kueneza lugha ya kiswahili. Sasa twaishi kwa amani na maelewano

Friday 30 May 2014

WABUNGE WETU WATOKA NJE TENA

Ukumbi wetu wa Bunge umekuwa sehemu ya kususiwa kila mara. Leo tena katika vikao vya Bunge la Bajeti baadi ya wabunje wa Kambi ya Upinzani wasusia mjadala wa Uwasilisjwaji wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na kutoka nje.

DAR ES SALAAM KABLA YA MWAKA 1900 NA ILIVYO SASA

Na hapa chini ni Dar ilivyo miaka ya karibuni. Bado vikwangua anga vingi vinaendelea kujengwa

KITUO CHA DALADALA MWENYE KUFUNGWA RASMI

TUDUMISHE MILA 1

Akina mama na wasichana wa huko Babati Mkoani Manyara wakiwa katika mavazi yao asilia

Thursday 29 May 2014

WASICHANA ASILIA HUKO WILAYANI HANANG MKOANI MANYARA

Tudumishe mila zetu hasa zile zilizo sahihi na zisizo na upotoshaji wowote kiuchumi na kijamii.

Monday 26 May 2014

KUMEKUCHA TUKAWAJIBIKE

Kwa wafugaji wa kuku tuwahi kwenye mabanda ya kuku wetu
Chukua usafiri wowote uliopo na kama hamna tembea kwa miguu
Kwa wakulima mashambani, mungu katupatia ardhi nzuri yenye rutuba twendeni tukawajibike.
Wachuuzi wa bidhaa mbalimbali mfano dagaa wa Kigoma kama wanavyoonekana hapa

Sunday 25 May 2014

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Hawa sijui wanaelekea kanisani kweli au!? Na hii ndo staili mpya ya Mshikaki katika Bodaboda. Hatari kweli kweli.

REAL MADRID MABINGWA UEFA 2014

Timu ya Real Madrid imefanikiwa kuchukua Kombe la UEFA 2014 usiku huu baada ya kuwacha Atletico Madrid kwa Mabao 4 - 1 huko Lisbon,Portugal.Bado la mwisho ambalo lilifungwa katika kipindi cha dakika 3o za nyongeza kwa njia ya Penati na Cristian Ronaldo, ndilo lililofunga kikapu cha magoli hayo. Hongereni Real Madrid.
Kufurahia ushindi

Saturday 24 May 2014

RAIS MTEULE WA AFRIKA KUSINI MHE.JACOB ZUMA KUAPISHWA LEO

Mhe.Rais Jakaya Kikwete aliwasili nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe za kuapihwa kwa Raisi Jacob Zuma.
Rais mteule wa Afrika Kusini Jacob Zuma anaeapishwa leo kuwa rais kwa kipindi kingine cha uongozi kupitia chama cha ANC

KUTOKUJIAMINI

Wakati mwingine tunakuwa watumwa wa mali zetu wenyewe na hata kuwa wachoyo kimatumizi na hivyo kujikuta tunachelewesha maendeleo. Unapokuwa nacho tumia ipasavyo japo kwa uangalifu lakini sio kuwa mchoyo na kutojiamini hivi. Kujiamini kunaanza kwako na pia kunaelekea kwa wengine. Kukosekana kwa uaminifu ni kero kubwa kwa jamii na huanza hivi hivi kwa mambo madogo kama haya. Simu tu unaiwekea kofuli,ingekuwa bastola....

Friday 23 May 2014

KIONGOZI NI MFANO NA UNYENYEKEVU

IJUMAA NJEMA WADAU

KAZI NI KAZI BORA MKONO KINYWANI

Katika nchi ya wajisiriamali kama yetu, suala hili sio geni kwani kuwajibika katika kutafuta maisha bora ni kwa kila njia ili mradi ni halali

KUJISIFU KWINGINE JAMANI UUH

Thursday 22 May 2014

SAFARI KUELEKEA ELIMU BORA KATIKA MAZINGIRA MAZURI BADO NDEFU

Hawa ni wanafunzi wa shule mojawapo Mkoani Singida ambayo wanajifunza katika darasa lililoezuliwa paa kama wanavyoonekana
Kwa mtindo huu, hii katuni inaleta taswira
(katuni kwa hisani ya Nathan Mpangala)

Wednesday 21 May 2014

MV BUKOBA-TUTAWAKUMBUKA DAIMA

Tanzania tutakumbuka daima ajali mbaya ya Meli ya MV.Bukoba iliyotokea 21.05.1996 kilomita chache kutoka Bandari ya Mwanza. Meli hiyo ilikuwa inatoka Bukoba kuelekea Mwanza. Watu wengi walipoteza maisha yao akiwemo Mjomba angu Mpendwa. Mjomba na wote waliofariki mpumzike kwa amani. Amina

Tuesday 20 May 2014

KIJEMBE KWA WACHEPUKAJI

PUMZIKA KWA AMANI ADAM KUAMBIANA

Mtayarishaji na Mwongozaji mahiri wa filamu hapa Bongo,Adam Kuambiana anaagwa leo katika Viwanja vya Leaders jijini Dar na baadae kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni. Mungu ailaze pema roho yake.Amen

Monday 19 May 2014

CHANGAMOTO YA ELIMU YETU

Pamoja na ugumu wa kimazingira, bado wanafunzi hawa wana kiu ya kupata elimu.

KUMEKUCHA JKT

Wahitimu wa Kidato cah Sita 2014 wanatarajia kujiunga na JKT kuanzia Juni 1 hadi Sept 4 kufuatia utaratibu huo ulorudishwa na Serikali miaka ya hivi karibuni

Friday 16 May 2014

USIKOSE HII MAANA UNAAMBIWA NI KALI TOKA KWA JOTI

Ufafanuzi wa ile kauli "Uzee mwisho Chalinze,Mjini wote Baby" unapatikana humu.
Penda nchi yako na wasanii wake kwa kununua kilicho cha kitanzania

Sasa nimeamini ule msemo: "MAMBO YA NGOSWE MWACHIE NGOSWE"

Wakati mwingine akipiga usingizi tena kazini na silaha imekaa kihatari, wengine wanaendelea kujituma vilivyo. Mungu abariki juhudi za kila anayejitahidi na wewe unayelala usingizi katika eneo la kazi tambua familia na jamii inakuhitaji. Wajibika!

Thursday 15 May 2014

USHAURI WA BURE

USALAMA WA MAISHA YAKO.

* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua.
Hiyo ni hatari kwani hujui huyo
jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi
ya wizi au mauaji. Inawezekana
simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige
sehemu yoyote.
* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake
kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina
sh ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa,
unapoiweka simuni mwako, simu yako
inahusishwa na tukio hilo.
* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha
unaichana. Unapoitupa, watu
wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya
vocha ile na kuweka sehemu ya
tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na
wewe kuhusishwa.
* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina
lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya
matukio hayo yakitokea na namba yako
kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa
namba moja. Wengi wamepewa kesi
za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini,
wanapoona vidhibiti wanakuchukua
kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni
makini ili usije kuingia matatizoni,
simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi
kama uzembe, utaishia pabaya.
MPE ONYO NA MWENZAKO.

Wednesday 14 May 2014

KWELI BIASHARA KUJITUMA

Pamoja na kwamba usalama wa mama huyu upo hatarini lakini anajituma hivyo hivyo ili walau mwisho wa siku apate chochote cha kujikimu
Mjasiriamali huyu wa asili ya Kimasaai anaonekana akiuza sarafu za zamani ambazo kwa sasa hazitumiki kama pesa halali. Kadiri ya mfanyabiashara huyo,pesa hico zinaweza tumika kama dawa ya kichwa tumbo na hata kuzuia mimba kuharibika. Haya yote ni katika kujiwajibisha ili kujikimu kimaisha.

HOMA YA DENGUE YAWA TISHIO DAR ES SALAAM