Sunday 31 August 2014

UDAKU: LULU KATUPIA VAZI LA HESHIMA ,HONGERA ZAKE

Wakati mwingine unajiuliza kulikoni? katika ndio binadamu tulivyo. Kubadilika ni kawaida ila mabadiliko kutoka kubaya kwenda kuzuri ndo yatakiwayo...

KUTOKA MAGAZETINI

SUALA LA VIGODORO LIPUKIWE MACHO DHIDI YA MAADILI

Pamoja na kuendelea kufurahia weekend, lakini tunaiomba serikali ielekeze nguvu katika suala zima la maadili dhidi ya Kundi linalojihusisha na burudani zijulikanazo kama Vigodoro.

Saturday 30 August 2014

JE WAJUA?..........

Kama unataka kujua zaidi ---> Mwezi huu una Ijumaa 5, Jumamosi 5 na Jumapili 5. Hii hutokea mara moja tu kila baada ya miaka 823. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1191. Baada ya hii ya mwaka huu wa 2014 mara nyingine tena itakuwa mwaka 2837

MAUSIA MAZURI YA BABA KWA MANAE WA KIUME

1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama mama kwako, mama kwa wanao na mama kwa familia, tafadhali mwanangu usimuache huyo!

2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!

3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!

4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo awe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi, lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa umeishiwa!

5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!

6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke na mume!

7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!

8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza kufanya nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio vinginevyo!

9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.

10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.

11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na hajakufafanisha na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio maana aliamua kuwa na wewe.

12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na mwambie atimize nusu iliyobaki.

13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikra) na nilikuwa naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.

14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga kama wazee wengi wa hapa kijiji wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga huu, kwani kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu kama enzi zetu. Ukijaliwa watoto wape elimu.

15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!

16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na ukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.

17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.

18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika. Pamoja na kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.

19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!

20.NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU….NAKUPENDA!

Friday 29 August 2014

KATUNI YA LEO

MSUMENO UNAKATA KOTEKOTE

KWA WALE WALIOANZA WKEND,NAWATAKIA WKEND NJEMA

Tujitahidi kila kitu kwa kiasi, kisheria na umakini

UBUNIFU

Wakati wengine wakigundua umaarufu wa kutengeneza Hoteli katika Meli zilizoegeshwa Pwani ambayo hazitumiki tena, Huko Ghana wajanja wamejenga Hoteli nzuri ndani ya ndege.

Thursday 28 August 2014

RONALDO WANASOKA BORA WA ULAYA

Cristiano Ronaldo anachukua ubingwa wa Mwanasoka bora wa Ulaya akiwapiku washindani wenzake Manuel Neuer (Golikipa wa Ujerumani)na Robben wa Uholanzi. Amekabidhiwa ushindi huu jana huko Monaco Ufaransa

HUYU NDIYE ALIYEGUNDUA MADINI YA TANZANITE

Mzee Jumanne Ngoma wa Makanya Samer, Kilimanjaro ndiye anayesadikiwa kugundua madini hayo mwaka 1967

YALIYOJIRI LEO MAGAZETINI

Wednesday 27 August 2014

UNAPOINGILIA ANGA ZA WENGINE.....

Picha hizi zaonyesha wanyama wanavyojihami hasa wale wasio wa eneo hilo wanapoingilia anga zao

SHERIA KWA WOTE

Hapa anaonekana Askari wa Usalama Barabarani akikagua gari walilokuwa wanaendesha watoto hawa. Ama kweli sheria inabana wote sawasawa kadiri ya matumizi

VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO

Tuesday 26 August 2014

USINGIZI HAUNA PENYEWE

Hata kama ni kuchoka lakini usalama pia uzingatiwe unapohitaji kupata usingizi

ZANZIBAR KUPATA UWANJA MPYA WA KISASA WA NDEGE

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanza mchakato wa Ujenzi wa Uwanja mpya wa Kimataifa wa ndege ambao utaendana na hadhi za kimataisha na kukidhi haja ya wasafiri kwa sasa
Mwonekano wa uwanja huo baada ya kukamilika

UJIRANI MWEMA

Mjane wa Rais Mkongwe wa Afrika Kusini Mama Graca Machela akilasilimiana na Mama Salma Kikwete alipotembelea Ofisi za WAMA hapo jana jijini Dar es Salaam.
Mgeni akipokea zawadi

Monday 25 August 2014

MICHEZONI: BALOTELLI AHAMIA LIVERPOOL

Mchezaji wa zamani wa Man City ambaye mpaka siku za karibuni alikuwa akichezea AC MILAN ya Italy amehamia rasmi timu ya Liverpool ya Uingereza

Sunday 24 August 2014

UDAKU_NDOA YA DIAMOND NA WEMA MBIONI

Msanii anayependwa sana kwa sasa Bongo Diamond Platnumz amegusia kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenz wake wa muda mrefu Wema Sepetu. Anasema kwakuwa ana washabiki wengi inawezekana hata akapanga kufunga ndoa hiyo Uwanja wa Taifa ili mashabiki wake wengi waweze kuhudhuria. Tunamuombea heri

KUTOKA MAGAZETINI LEO

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Pengine wapo mbio kwenda Kanisani kusali. Hiki ni kipaji kikikuzwa kitaleta manufaa. Hawa ndo wabunifu wa baadae

Saturday 23 August 2014

KAZI; KAMA SEHEMU MBILI ZA SHILINGI VILE

Wakati mwingine anawajibika sana kimajukumu, mwingine wakati wa kazi kajistarehesha anavyojua.

UONGOZI WAHITAJI FADHILA NYINGI MOJAWAPO UNYENYEKEVU

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akipanda Treni ya Tazara kuelekea Kisaki Morogoro katika moja ya ziara zake hivi Karibuni.
Waziri Mkuu wa Uingereza mhe.David Cameroon akiwa anasafiri katika moja ya viunga vya London alipanda treni.Hata hivyo hakupata nafasi ya kukaa.Hakuona tabu kusimama pembeni huku akijisomea gazeti lake badala ya kuwabughudhi wananchi wampishe akae au kutumia gari na ving'ora kupisha njia
Pope Francis 1 akiwa kwenye bus katika moja ya viunga vya Vatican City

Monday 18 August 2014

HILI HALIKUBALIKI

Nafasi ya upendo kwa binadamu haipaswi kulinganishwa na ya mnyama mwingine.

Sunday 17 August 2014

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Nawaomba kwa kimya cha muda kidogo.Kulikuwa na mambo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu kunifanya nishindwe kupost habari. Ila sasa karibuni tena nyumbani.

Saturday 9 August 2014

NCHI MASKINI AMBAYO ARDHI YAKE IMEBARIKIWA

Waziri Mkuu mhe.Mizengo Pinda akitazama ndizi katika Maonyesho ya NaneNane huko Mwanza.

ALI KIBA KWENYE KANDANDA NAE YUMO EEE

Katika Tamasha la matumaini,mchezaji Ali Kiba wa Bongo Fleva akimtoka mchezaji Issa Musa Cloud 112 wa Bongo Movie. Katika mchezo huo Bongo Fleva walishinda 1-0

KATUNI YA LEO-MICHEPUKO SIO DILI

MAGAZETINI

Monday 4 August 2014

JEURI YA PESA-RANGE ROVER YA DHAHABU

TUJIHADHARI NA HAWA TRAFIKI FEKI.....

Mheshimiwa Kamishna Kova akionyesha kidole kwa Askari feki aliyenaswa huko Chamazi Mbagala-Dar

WAKATI MWINGINE HUWA NAJIULIZA..............

Hivi mtoto kama huyu aliyezaliwa kwenye nchi nzuri yenye sifa nyingi nzuri duniani, asubuhi ameamka na kuwahi shuleni kwa miguu, kisha mchana anaporudi inabidi ahangaike kujitengenezea chakula chake duni mwenyewe,hivi kweli kuna siku atakaa auelewe huu msemo "Maisha bora kwa kila Mtanzania"????

Sunday 3 August 2014

"WANAUME WA AFRIKA,WAWEZESHENI WANAWAKE KUTOKA KIMAISHA"MHE MICHELLE OBAMA

Michelle Obama, mke wa rais wa Marekani amewataka wanaume wa Afrika kuwasaidia wanawake katika vita vya kuleta usawa wa jinsia kote duniani.
Akizungumza katika kikao cha kufunga mkutano mkuu wa kwanza wa mradi wa Mandela kwa ajili ya Viongozi Vijana wa Afrika - YALI mjini Washington, Bi. Obama akishangiriwa na vijana 500 kutoka zaidi ya mataifa 50 ya Afrika, aliwapongeza viongozi hao kwa kazi wanaofanya na kuweza kufika mahala walipo hii leo.
Mke wa rais wa Marekani alisema akiwa Marekani mwenye asili ya kiafrika na kuolewa na Marekani mwenye asili ya Kenya, anafahamu fika safari ndefu wanawake wanapita kuweza kufanikiwa, na kusema "nimefika mahala nilipo kutokana na msaada wa kaka zangu na wanaume katika familia yangu. " alisema Bi. Obama.
Akizungumza kutoka moyoni alisema badala ya watu kuzungumzia rasilmali zinazohitajika kuwezesha ufanisi wa elimu ya wasichana, jambo ambalo bila shaka ni muhimu, lakini amesema inabidi kwanza, watu kuanza kuzungumzia wazi haja ya kubadili tabia, maadili na imani ya jinsi kina baba na kina mama wanavyo wachukulia wasichana wao, kwa kuuliza ikiwa wanastahiki kupata elimu au kuolewa wakiwa wagdogo.

Kutokana na hayo Michelle Obama amewataka vijana walohudhuria wiki sita za masomo na kupata ujuzi hapa Marekani kurudi nyumbani na kuanza kampeni ya kuomngoza miradi ya kuleta mabadiliko bila ya kuwasuiri viongozi wao au serikali zao kuwafanyikia mambo yao.

Vijana wote wameeleza kuridhika na ziara yao na kusema wamepata motisha wa kutosha na wanarudi na nguvu kuweza kuleta mabadiliko barani Afrika. (Habari kwa mujibu wa VOA)

MICHEPUKO INAANZAGA HIVI HIVI....KUWA MAKINI

LISIMWALO LIPO,KAMA HALIPO LINAKUJA