Wednesday 30 December 2015

HONGERA SANA MASANJA MKANDAMIZAJI

Masanja Mkandamizaji:
"Macho ya kibinadamu yanaweza kusema sistahili lakini yupo Mungu ambaye hutustahilisha sote muda atakao na kwa haki".

BOMOA BOMOA BONDE LA JANGWANI DAR

Baadhi ya wananchi wakiwa wamesha bomoa nyumba zao zilizo katika Bonde la mto Msimbazi, mtaa wa Magomeni Sunna jijini Dar es salaam, kabla ya serikali kuanza kuzibomoa nyumba hizo ifikapo tarehe 5 januari 2016

Monday 28 December 2015

UDAKU; SMS INAYOPENDWA NA KINADADA WENGI

VIJANA KIPINDI CHA XMAS 'ENZI ZA MWALIMU'

MAWAZIRI WAPYA 4 NA NAIBU WAAPISHWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa Ikulu, ambapo amewapisha mawaziri watano kujaza nafasi za mawaziri zilizokuwa wazi katika wizara kadhaa za serikali ya awamu ya tano, Hafla ya kuwaapisha mawaziri hao imefanyika leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Gerson Lwenge kuongoza wizara hiyo ikulu leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango kuongoza wizara ya fedha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dk. Joyce Nderichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mawaziri walioapishwa katika picha wa pili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, wa pili kutoka kulia ni Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kulia ni Mh. George Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.

KIOTA MAARUFU MWANZA: JEMBE BEACH RESORT

Picha zote kwa hisani ya G.Sengo Blog

Sunday 27 December 2015

MHE RAIS WA ZANZIBAR DR.SHEIN AWAKILISHA TAARIFA YA HATUA YA MAZUNGUMZO KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO MHE.DK.MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam jana Desemba 26, 2015

Friday 25 December 2015

XMAS DAR ES SALAAM BILA KWENDA BEACH HAIONOGI

Basi sisi tumeamua kutengeneza swimming pool yetu

NAWATAKIA KRISMASI NJEMA


RAIS Dr John Magufuli ameweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa kisiasa kubusu mikono ya kiongozi wa dini hadharani ishara inayoashiria upendo kwa viongozi hao wa dini ambao hufanya kazi kubwa ya kuchunga kondoo.

Rais Magufuli alifanya tendo hilo leo katika misa takatikfu ya Krismasii katika kanisa kuu Mt Peter jijini Dar Es Salaam.

Thursday 24 December 2015

SHOPPInG YA XMAS YAPAMBA MOTO DAR

ZIKIWA zimebaki siku mbili waumini wa dini ya Kikristo duniani kusherehekea sikukuu ya Krismas ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, jana kwa wingi wao, wameonekana wakifanya manunuzi ya nguo na bidhaa mbalimbali za sikukuu katika mitaa ya Kariakoo.
Kamera yetu imefanikiwa kunasa baadhi ya picha zinazoonesha wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakiwa katika shamrashamra za manunuzi na kusababisha mitaa kutokupitika kwa urahisi kutokana na msongamano wa watu.

KATUNI YA LEO

Inaakisi tatizo kubwa lililopo katika jamii. Watendaji kuwa mbali na wananchi. Na wakati mwingine hata kwenye mazungumzo ya ana kwa ana. Ubwana na Ubibi shamba sio kazi za kwenda eneo la tukio na mavazi ya kuwafanya wakulima kujiona wako mbali na wanayetaka awasaidie.

DARAJA LA KIGAMBONI

Picha za Ujenzi wa Daraja la Kigamboni Ulipofikia Kwa Sasa....Siku si Nyingi Litaanza Kutumika Ambapo badala ya Kupanda Kivuko sasa unaweza kwenda kutoka kigamboni au kwenda kwa gari yako au miguu bila kupanda kivuko..

MHE.RAIS MAGUFULI AKAMILISHA BARAZA LA MAWAZIRI

KILIMANJARO XMAS Loading......................

Monday 21 December 2015

MHE.MAALIM SEIF AFANYA MAZUNGUMZO NA MHE RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif, leo Ikulu jijini Dar
Maalim Seif Sharif, Dkt. John Pombe Magufuli, (katikati) na Makamu wa rais, Mhe. Samia Suluhu wakiwa katika picha ya pamoja

KERO YA USAFIRI UBUNGO DAR KIPINDI CHA XMAS