Saturday 1 August 2009

AIR FORCE ONE ULINZI MKALI ANGANI

Ndege ya Rais wa Marekani ina ulinzi maalum wa ndege yake iwapo angani, Ndege inayoonekana pembeni ndio ndege ya ulinzi kwa Air Force One ila ulinzi huu si kila wakati,itategemea sababu za kiusalama na kila wanapotaka kuipa escort ndege ya Rais lazima wananchi wa nchi hiyo waarifiwa ili kutokupata mawazo tata.

2 comments:

  1. Asante kwa taswira njema.
    Ni kweli kuwa (inapohitajika) Air Force One huwa na "escort" lakini hiyo ni PALE INAPOHITAJIKA TU. Katika hali ya kawaida si kitu cha kawaida kuiona hiyo ndege ikiisindikiza na inapotokea kitu kama hicho kufanyika, wananchi watataarifiwa kuhusu sababu za kiusalama zinazofanya hilo litokee (hasa kue ambako ndege itapita) na kwa kutofanya hivyo huleta WASIWASI mkubwa kama ilivyotokea April 27 mwa mwaka huu ambapo walitaka kupiga picha ndege ya akiba ya Rais na kutumia hizo za jeshi kufanya hivyo na matokeo yake ikawa big issue kwa kuwa watu hawakujua usalama wa Rais na hawakuambiwa kuwa tukio hilo lingetokea na ikaleta mgongano wa mawazo kiasi cha IKULU ya marekani kuwaomba wananchi msamaha. Taswira 146 za tukio hilo la April 27 ndio zimetolewa jana July 31. Rejea habari na video hapa (UKIANGALIA VIDEO UTASIKIA HOFU YA WAKAZI ILIVYOKUWA) http://www.nypost.com/seven/04272009/news/regionalnews/obama_plane_photo_op_startles_new_yorker_166470.htm . Kwa hiyo katika hali ya kawaida hizo ndege haziongozani namna hiyo ila tukio hilo ni nadra na adimu na huwa lahusishwa saana na hali-tete ya usalama wa Rais.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Nashukuru mzee wa Changamoto kwa maelezo mazuri, nadhani na wadau watapenda taarifa hiyo pia.

    ReplyDelete

Maoni yako