Friday 15 January 2016

WIZARA YA AFYA YATOA MSIMAMO KWA WAGANGA TIBA MBADALA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa uamuzi wa Serikali kuhusu Serikali kuhusu Tiba Asili na TibaMbadala katika mkutano wa waandishi ulifanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.kushoto ni Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu, ambapo ameleza kwamba watoa huduma hao ni lazima wasajiliwe na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala wakiwemo wasaidizi wao, vifaa wanavyotumia na dawa. Pia imetoa muda wa miezi mitatu kwa mijini na vijijini miezi sita kutekeleza agizo hilo.

Katika nchi yoyote ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau. Huduma za tiba asili na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa. Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali. Kutokana na hali hiyo na kutokana na ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) kwa Tabibu Juma Mwaka Juma tarehe 14/12/2015 na kufuatia uchambuzi uliofanywa na Wizara baada ya ziara hii, Wizara imebaini changamoto zifuatazo:- 1. Huduma za tiba asili na au tiba mbadala zinatolewa na watoa huduma wasiosajiliwa na Mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria. 2. Uwepo wa vituo vinavyotoa huduma za Tiba Asili na au Tiba Mbadala bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria. 3. Kutolewa dawa kwa wagonjwa bila dawa hizo kusajiliwa na mamlaka husika. 4. Uingizaji na matumizi ya vifaa vya uchunguzi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka zinazohusika, na 5. Utoaji wa matangazo bila ya kufuatwa kwa matakwa ya sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. Aidha baadhi ya matangazo hayo yamekuwa na taarifa zinazoweza kuleta madhara na kupotosha Umma wa Watanzania.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako