Monday, 11 January 2016

MHE.RAIS MAGUFULI AIFARIJI FAMILIA YA MWL.NYERERE KUFUATIA KIFO CHA BI.LETICIA NYERERE

Bi Leticia Nyerere akiwa Bungeni Dodoma enzi za uhai wake
#################################################################################################
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.

Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.

Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama Nyerere

No comments:

Post a Comment

Maoni yako