Wednesday 30 April 2014

UJUMBE WA LEO

Hii ni baada ya mchezaji wa Barcelona Dani Alves kutupiwa ndizi akiwa uwanjani kisha akaamua kuiokota kuimenya na kuila kama anavyoonekana pichani

AIRTEL YATANGAZA WHATSAPP,FACEBOOK NA TWITTER BUREEEEEE

Kwa maelezo zaidi soma vipeperushi.......

ALIYETUNGA JINA LA TAIFA "TANZANIA"

Ndg. Mohammed Iqbal Dar (Picha na maelezo kwa hisani ya DjSeki Blog)

Nimeona niwafahamishe hili huenda likatusaidia hasa kwa hivi sasa wakati tukisherekea miaka 50 Muungano, najua wengi wetu hatujui historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar maana tuliwakuta waasisi wetu wameishafanya zoezi hilo , tusilijadili sana kwa kuwa lengo lao lilikuwa zuri.
Lakini je unamjua huyu Bwana aliyetunga jina la Tanzania pata historia ya namnaalivyofanikiwa kupata jina la T A N Z A N I A.
Sherehe za Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huwa tunasherekea kila Mwaka Tarehe 26/04/ lakini Tangu mimi binafsi nipate ufahamu na kuanza kushuhudia sherehe za Muungano nimekuwa nikisikia kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibar na Raia wengine wa nje lakini sikuwahi kukutana na huyo ambae alibuni jina hili tamu la Tanzania .
Imekuwa kama Bahati nimekutana na Mtu huyu aliyebuni jina la Tanzania Mkoani Mtwara, sehemu ambayo tayari naiweka kwenye Historia yangu hata kesho nikiondokaMtwara nitaikumbuka Radio yangu Safari Radio.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Muhindi na Dini yake ni AHMADIYA MUSLIM JAMAAT TANZANIA majina yake ni MOHAMMED IQBAL DAR.
Mohammed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944, Baba mzazi wa Mohammed alikuwa Daktari huko mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dr. T A DAR alikuwa Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya Msingi Mkoani Morogoro shule ya Msingi H H D AGHAKHAN kwa sasa ni Shule ya Serikali na baada ya hapo alikuja baadae kujiunga na Chuo cha Mzumbe akasoma Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina la Muungano kati Tanganyika na Zanzibar ?
Mohammed anasema alikuwa Maktaba akijisoma gazeti la Tanganyika Standard, siku hizi Daily News, akaona Tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana kwa hiyo Wananchi wote wakaombwa Washiriki kwenye shindano la Kupendekeza jina moja litakalo zitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuingia kwenye Shindano na hivi ndivyo alianza Safari ya Kubuni Jina la Muungano.
Kwanza anasema alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na Imani yake na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika baada ya hapo akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal halafu akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya baada ya Hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika. Baada ya hapo Mohammed Iqbal Dar alichukua herufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua Herufi tatu za Mwanzo ZAN ukiunganisha unapataTANZAN alivyoona hivyo akachukua I herufi ya kwanza katika jina lake la Iqbal na akachukuaA kutoka jina la dini yake yaani Ahmadiyya kwa maana hiyo ukiongeza herufi hizi mbili I na Akwenye TANZAN unapata jina kamili TANZANIA akalisoma jina akaliona ni zuri lakini akajiridhisha pia kwamba akiongeza herufi hizo za I na A kwenye TANZAN italeta maana kwakuwa nchi nyingi za Afrika zinaishia na IA, mfano EthiopIA, ZambIA ,NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA alivyoona hivyo akaamua apendekeze kuwa jina TANZANIA ndio litumike kuwakilisha nnchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka majina manne majina hayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.
Mohammed Iqbal Dar baada ya kupata jina hilo akalituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu Shindano. Baada ya Muda mwingi kupita baba yake na Mohammed Iqbal Dar alipokea barua nzito kutoka Serikalini ikiwa inasomeka kama ifuatavyo…

REPRESENTED BY THE
MINISTRY OF INFORMATION AND TOURISM , TANZANIA
TO
MOHAMED IQBAL DAR
IN RECOGNATION OF THE ACHIEVEMENT OF CHOOSING THE NEW NAME FOR THE
UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR NAMELY
“ REPUBLIC OF TANZANIA ”
DURING THE NATIONAL COMPETITION DAY IN 19TH NOVEMBER 1964
I A WAKAL
MINISTER FOR INFORMATION AND TOURISM

Barua hiyo pia ilisema...
Utakumbuka kuwa miezi michache iliyopita ulituandikia kutupa ushauri kuhusu jina jipya la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na wewe pamoja na wananchi wenzio 16 ulishauri nnchi yetu iitwe Tanzania . Nafurahi kukuarifu kuwa mshirikiane ile Zawadi ya sh. 200 iliyoahidiwa na leo nakuletea check ya sh. 12/50 ikiwa ni hisa yako katika zile sh.200. Nashukuru sana kwa jitihada ya kufikiri jina la Jamuhuri yetu.
Barua ikasainiwa na Idrisa Abdul Wakil Waziri wa Habari na utalii kipindi hicho.
Sasa kwa nini Mohamedi Iqbal Dar anadai yeye kuwa mshindi pekee wakati barua ilikuwa inaonyesha kulikuwa na washindi wengine 15 ambao nao walishinda?
Jibu ni kuwa wakati wa kutolewa kwa Zawadi hizo hakuna aliyejitokeza zaidi ya Bwana Mohammed Iqbal Dar na Bwana Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya kumpongeza kuwa ameshinda kwa madai kuwa Barua ameipoteza, hivyo Wizara ya Habari na Utalii iliamua kumtangaza bwana Mohammed Iqbal Dar kuwa Mshindi na kumpatia zawadi yote ya sh.200/; pamoja na Ngao.
Bwana Mohammedi Iqbal Dar anasema anachosikitika ni kuwa mchango wake bado Watanzania hawathamini mchango wake lakini yeye anaipenda Tanzania na anajivunia kuwa Mtanzania japo anadhani dini yake ya Uislamu ndiyo tatizo hawataki kutambua mchango wake ila anaamini kuwa siku moja ukweli utajulikana.
Hayo ni maelezo ya Mohammed Iqbal Dar ambaye kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alipata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK , Dar– es-Salaam House, 18 TURNHOUSE ROAD , PHONE 44 121-747-9822
Nimeona niwatumie hii wadau wangu ili tuweze kuongeza ufahamu na kama ulikuwa unalijua hili basi nimekukumbusha pia mambo yalivyokuwa miaka ya 1964

Tuesday 29 April 2014

JITAMBUE: WASEMAVYO WATAFITI

FAHARI ZA TANZANIA

Nawatakia wadau mwanzo mwema wa wiki na pia kila la kheri kwa wiki nzima

Sunday 27 April 2014

KANISA KATOLIKI LAPATA WATAKATIFU WAPYA WAWILI LEO

Papa John Paul II aliwahi kutembelea Tanzania mwaka 1990

NUKUU YA LEO_JUMAPILI NJEMA

MWEMBE WA MUUNGANO NAO WATIMIZA MIAKA 50

Wakati wa Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili 1964, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Zanzibar Abeid Amaan Karume ambao sasa wote ni marehemu, walipanda katika shimo moja miembe miwili mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka Tanganyika. Miembe hiyo imekuwa na kustawi pamoja na kufanya shina moja 'through grafting' .Leo hii mti huo wa mwembe umestawi vyema katika bustani ya Ikulu, Dar es Salaam, kama unavyoonekana leo Aprili 26, 2014 ambayo ni Siku ya miaka 50 ya Muungano.
(Picha na maelezo kwa hisani ya CCM Blog)

Saturday 26 April 2014

TWAJIVUNIA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
Taswira ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 1964

CHANGAMOTO KUELEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO

Licha ya watoto hawa kuishi maisha duni lakini nyuso zina tabasamu na matumaini. Ni vizuri tukawatimizia hayo

Friday 25 April 2014

UBUNIFU TANZANIA

Viatu na pochi (wanawake)

Ubunifu huu mkubwa unafanywa na KIM FASHION DESIGN ambao wanapatikana NAFASI ARTSPACE karibu na ITV Mikocheni. Kama wahitaji kupata viatu au mikoba hii wasiliana nao hapa +255 714 76 83 98
viatu mwanana vya kiume

UJENZI WA TERMINAL 3 UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM KUZINDULIWA

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akitazama ramani ya utakaokuwa Terminal 3 ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa JN Dar es Salaam katika uzinduzi wa ujenzi wake ulofanyiika jana. Uwanja huo unajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uholanzi na watarajiwa kukamilika mwaka huu.
Kukata utepe katika uzinduzi wa ujenzi huo

Thursday 24 April 2014

MAMBO YA BUNGE MAALUM LA KATIBA

MUUNDO WA SERIKALI ULIOPENDEKEZWA NA TUME
MUUNDO WA SERIKALI ULIOPO HIVI SASA

Wednesday 23 April 2014

BUNGE LA KATIBA=TAZAMENI HAWA MNAPOJADILI KATIBA MPYA

Wananchi wakiwa wavumilivu kuwasikiliza mjapo kutoa sera zenu. Hapa wanadiriki kujificha mvua kwa viti ambavyo hata hivyo inawalowanisha tu. Je, mnawatimizia matakwa yao huko Bungeni?
Mzee huyu miaka nenda rudi anatafuta hela kukidhi mahitaji yake walau hata kiatu cha kusitiri mguu wake. Kodi yake mnaitumiaje huko Bungeni?

Saturday 19 April 2014

HUJAFA HUJAUMBIKA

Gwiji la muziki wa dansi nchini Marehemu Muhdin Gurumo enzi za uhai wake akitazama mwembe, mti ambao tawi lake lilimdondokea akiwa mdogo na kumpofua jicho moja. Inaemekana alikuwa amelazwa hapo chini ya mwembe huku mama yake akiendelea na shughuli nyingine ndipo tawi hilo lilipomdondokea na kumuumiza jicho. Mungu amrehemu.

Mtoto akimlisha mama yake. Alipokuwa mchanga mtoto huyu alikuwa akilelewa na kulishwa na mama yake ila baadae kaona mama yake anavyoteseka majukumu yakageuka.

MAANDALIZI YA KITOWEO CHA PASAKA

Friday 18 April 2014

NAWATAKIA IJUMAA KUU NJEMA

KWA MWENDO HUU KWELI KATIBA TUTAIPATA?

WAJUMBE karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza. Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba. Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko. Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu…

Sunday 13 April 2014

JUMAPILI NJEMA ILA MVUA YA WIKI HII TUNAIPA SHIKAMOO


Eneo la Jangwani Dar es Salaam. Kwa mbali linaonekana jengo la Yanga
Hata kwa mtumbwi hapafai
Kwa wingu hilo lilivyotanda uuuh
Uhai kwanza, gari tutanunua jinginge

Dar es Salaam yageuka kisiwa baada ya eneo la Ruvu kufurika.

Thursday 10 April 2014

FAHARI YA ZIWA TANGANYIKA

Hii ndio Mv.Liemba ambayo inatimiza miaka 100 ya huduma za usafiri katika Ziwa Tanganyika. Meli hiyo ilianza safari zake mwaka 1914.

Tuesday 8 April 2014

POSTA DAR ES SALAAM HAPAPITIKI LEO

HAPO ZAMANI ZA KALE..........................

Haya ndio yalikuwa mafuta maarufu ya kupikia
Huu ndio ulikuwa usafiri wa viongozi wa kitaifa
Huu ndio ulikuwa usafiri wa mabasi ya Abiria (KAMATA na TANGANYIKA BUS)
Baadhi ya vitabu mashuleni vilikuwa hivi