Friday 28 February 2014

Wednesday 26 February 2014

UJUMBE WA LEO

Heri "kutabasamu" kwenye BODABODA.......................

Kuliko "kununa" kwenye RANGE ROVER.

Monday 24 February 2014

KATUNI YA LEO

Kwa hisani ya Michuzi/Mpangala

Sunday 23 February 2014

ASIYEFANYA KAZI NA ASILE

Inapendeza sana kuona namna mama huyu anajitahidi kuwajibika kwa ajili yake na familia yake. Mama Mwafrika halisi.

Saturday 22 February 2014

YA KWELI HAYA?

Kucheki mpira na wanawake ni stress tupu kwa maswali yao:

Mwanamke: Baby yule jamaa ni Chris Brown?
Jamaa: Hapana anaitwa Theo Walcott.
Mwanamke: Hee.. Ile kadi ya njano ni ya nini?
Jamaa: Ni onyo tu kwamba kafanya kitendo kibaya, akipewa nyekundu anatoka!
Mwanamke: Na ya kijani je?
Jamaa: Hamna kitu kama hicho! Hamna za kijani!
Mwanamke: Nataka Arsenal washinde Kombe la Dunia.
Jamaa: (kimya)
Binti: Yule mzee ni nani?
Jamaa: Arsene Wenger.
Binti: Okay! Kwa hiyo na yule mwingine ni Manchester Wenger?!

Friday 21 February 2014

VIMINI HAVINA SOKO TENA UGANDA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini Mswada wa kuzuia wanawake kuvaa nguo fupi zijulikanazo kama vimini ama nguo zozote za nusu uchi. Kuanzia sasa mtu yoyote atakaye kutwa amevaa hivyo atachukuliwa sheria ikiwemo adhabu ya kufungwa jela miaka 10 mpaka 15 ...Je unaonaje na kwetu Tz ikiletwa Adhabu Hii 

Wednesday 19 February 2014

MILA NYINGINE DUH!

Hii ni moja ya michoro mwilini inayofanywa na kabila la Surma huko Ethiopia. Michoro hii hufanyika kwa kudonolewa donolewa na mwiba bila ganzi.

HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA

Nimewapa pichaa hii wadau wangu kuwatia moyo kujitahidi katika kujiendeleza. Pia kuwataadharisha kwamba kama kuna kasoro yoyote ifanyiwe kazi na kuondolewa mara moja kabla ya kukua na kuleta madhara.

Sunday 16 February 2014

USIJARIBU HII BONGO

Mkulima mmoja nchini China aliwatembeza bata wake wanaokadiriwa 50,000 akisema anawapa zoezi maana wanakaa ndani muda mrefu. Magari yalisubirishwa muda mrefu bata hao walipokuwa wanavuka njia.

JUMAPILI NJEMA WADAU

Friday 14 February 2014

HERI YA SIKUKUU YA WAPENDANAO

Nawapenda sana wadau wangu za Blog hii. Karibuni nyumbani
Ila pamoja na kuenjoy siku hii, muhimu kuwa makini.....

Thursday 13 February 2014

Wednesday 12 February 2014

UDEREVA WATAKA MOYO HAPA

Barabara hii ipo katika mazingira hatari ya miinuko mirefu na mabonde ya kina lakini hakuna jinsi lazima watu wasafiri

Tuesday 11 February 2014

UDA YAZIDI KUJIIMARISHA

Shirika la Usafiri Dar(UDA) jana limeongeza mabasi 175 kufikia mabasi 288 kwa ajili ya usafiri jijini dar

Monday 10 February 2014

UHABA WA NISHATI WAWAUMIZA KINAMAMA

Wakati Tanzania ikipigania kuvuna Gesi asilia kutoka mikoa ya kusini,bado kumekuwa na uhaba mkubwa wa nishati. Maeneo mengi hasa ya kijijini bado wananchi wanategemea kuni kupikia. Hii imepelekea kuvuna misitu asilia hovyo. Akinamama ambao ndio tegemezi.katika kuhudumia familia katika masuala ya chakula wamekuwa wakipata adha kubwa kutafuta kuni. Pengine ni umbali au uhaba. Hii imeenda mbali zaidi hata kufikia hatua ya kudhuru wanafunzi ambao hupoteza muda mwingi kwenda maporini kutafuta kuni za kupikia shuleni.

Sunday 9 February 2014

UCHAMBUZI WA MAKABILA:WACHAGGA

Wachagga ni kabila
 la watu wenye asili ya Kibantu
 wanaoishi kaskazini mwa Tanzania
 chini ya mlima
Kilimanjaro
, mkoani Kilimanjaro
. Shughuli kubwa ya Wachagga nibiashara
 na kilimo
.Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.*Vikundi vya Wachagga*Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea
, Rombo
hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha
,Machame
. Makabila ya Kichagga niWa-Rombo
, Wa-Marangu
,Wa-Kilema
, Wa-Old Moshi
, Wa-Kibosho
, na Wa-Machame
. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo
, Wa-Uru
, na Wa-Siha
.

*Lugha ya Kichagga*Lugha ya Kichagga
, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea
 mpaka unapofika Siha
 magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katikaKirombo
, Kimarangu
, Ki-Old Moshi
,Kikibosho
, Kimachame
,Kikirua
 na Kisiha
. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha
, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.*Historia ya elimu kati ya Wachagga*Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari
 waKikristo
 walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu.*Kilimo na chakula*Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi
, maharagwe
,viazi,ndizi
, ulezi
 na mboga mbalimbali. Mazao ya biashara kama vilekahawa
, nyanya
 na vitunguu
.

*Ndizi za Wachagga*Ingawa wachaga wa leo wanakula vyakula mbali mbali kama vile ugali
,wali
 na viazi
, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi
. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko,kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege
. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.*Wachagga na muhogo*Inasemekana kuwa "mchagga halisi, hali muhogo
 - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi
 ndani yao; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.*Ulaji kiti-moto*Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".*Majina ya Kichagga*Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi,Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Kavishe,Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.Ukoo wa akina Teri wako Mamba Kiria na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi
, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini yaUkristo
 kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.*Utawala wa jadi ya Wachagga*Watawala wa kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" nadhariainawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa kichagga.*Ardhi*Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya wachaga mikoani mbali mbali.*Maoni juu ya Wachagga*Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi
 na Kibosho
 ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.pia wachaga wamekua na desturi ya kuwaenzi wazee wao walio tangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanapo rudi nyumbani ifikapo mwezi desemba. hili limekua ni swala la kawaida sana na halipingiki. wengi wao huwa wanarudi na magari ndio sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi desemba kila mwaka foleni za magari zimekua zikiongezeka kutokana na wachaga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. wengi wao wamekua wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi,
(Kwa hisani ya Dj Seki Blog)

Saturday 8 February 2014

BAADHI YA TASWIRA ZA MAENEO YA KILIMANJARO

Taswira ya mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutokea maeneo ya Sanya Juu-Moshi Biashara ya Parachichi katika soko la Kwasadala-Hai Msikiti mzuri karibu na kituo cha mabasi cha Moshi Mjini Round about ukiwa unaingia mjini moshi karibu na KNCU na jengo la Posta

Friday 7 February 2014

UAMINIFU NA UMAKINI

Taswira ya mfuko wa saruji

Katika harakati za kupambana na maisha,mengi hujitokeza. Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na utapeli wa aina nyingi. Mfano ni kama picha hiyo ambapo mfuko huo uliopaswa kuwa na saruji ndani lakini badala yake kukuta udongo. Blog hii inawaomba wafanyabiashara kuwa waaminifu na makini kwa bidhaa zao. Pia wateja wanakumbushwa kuwa makini kuhakikisha bidhaa wanazonunua ili kuepuka utapeli kama huyo.

WABUNGE WA BARAZA LA KATIBA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Florence Turuka akitangaza majina ya wabunge hao jijini Dar es salaam TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA UTANGULIZI 1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (*The Constitutional Review Act, Cap 83*). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika. 2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:- (i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; (ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na  (iii) Wajumbe *201* kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika. 3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:- (i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20) (ii) Taasisi za Kidini (20) (iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42); (iv) Taasisi za Elimu (20); (v) Watu wenye Ulemavu (20); (vi) Vyama vya Wafanyakazi (19); (vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10); (viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10); (ix) Vyama vya Wakulima (20); na (x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

Thursday 6 February 2014

HII IMEKAAJE?

Sheria za Usalama barabarani zimekuwa zikivunjwa kila siku hasa na madereva na abiria wa pikipiki au maarufu Bodaboda jijini Dar es Salaam na hata mikoani. Pichani ni raia wa kigeni wakiwa wamepakiwa kwa staili ya mshikaki katika bodaboda huku wakiwa hawana kofia ngumu za kuwakinga na ajali. Hii ilikuwa Posta mtaa wa Ohio.  (Habari picha kwa hisani ya Father Kidevu)

Wednesday 5 February 2014

MTANDAO WA FACEBOOK WATIMIZA MIAKA 10

Mark Zuckerman mwanzilushi wa facebook Facebook ni mtandao wa Kijamii, ambao unatokana na jina la colloquial name for the book ulianzishwa nchini marekani kwa ajili ya wanafunzi ili uweze kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kuwasiliana na kutambuana kila mmoja. It was founded in February 2004 by Mark Zuckerberg with his college roommates and fellow Harvard University students Eduardo Saverin, Andrew McCollum, Dustin Moskovitz and Chris Hughes.

Tuesday 4 February 2014

ALIKOTOKA NI MBALI

Mhe Rais Jakaya Kikwete akivuka mto huku ameshika viatu mkononi. Picha hii ni ya miaka ya 1990 (kwa hisani ya dj seki blog)

Monday 3 February 2014

MIAKA 37 YA UHAI WA CCM

Mwenyekiti wa CCM Taifa mhe. Jakaya Kikwete;Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia katika maadhimisho ya miaka 37 ya CCM huko Mkoani Mbeya.

Saturday 1 February 2014

CHANGAMOTO

Mwezi wa kwanza(Januari) ndo umeisha na sasa tumeingia Februari. Pengine si vibaya kuangalia ni kwa namna gani mikakati yetu ya mwaka huu imeanza kupata mafanikio au kukwama.

Haitoshi tu kuvaa na kupendeza. Ila pia muhimu kujua chakula malazi na mahitaji mengine yanapewa kipaumbele katika utafutaji. Kazi ni kazi kwa mtu yeyote,nsmna yoyote,na mazingira yoyote ili mradi inakuletea kipato na hauvunji sheria za nchi au za kibinadamu.