Monday, 4 January 2016

SERIKALI YAINUNULIA MUHIMBILI MASHINE YA CT SCAN MPYA


Naibu Waziri wa Afya , maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto Dokta Khamis Kigwangwala leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili -MNH- na kuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za kulipia kwa kiwango cha daraja la kwanza ili kuongeza mapato ya hospitali na pia mgonjwa aweze kuona thamani ya pesa yake.

Akizungumza mara baada ya kutembelea hospitali hiyo ikiwemo Idara ya magonjwa ya dharura na ajali pamoja na mashine za CT Scan na MRI , Dokta Kigwangala amesema watumishi wa MNH hawanabudi kuwa wabunifu ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zina kuwa bora zaidi na zenye faida .

“ Hospitali ya Taifa Muhimbili ina madaktari bingwa wengi na wenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma na wengine ni wataalam wa magonjwa mbalimbali ikiwemo moyo na figo hivyo naamini wanaweza kufanya mabadiliko makubwa “ amesema Kigwangala .

Awali Mkuu wa Idara ya Mionzi Dokta Florah Lwakatare amemueleza Naibu Waziri Kigwangala kwamba mashine ya mpya ya CT Scan ambayo imenunuliwa na serikali inaendelea na majaribio pamoja kuwapatia mafunzo watumishi wake kwakua kua mashine hiyo ni ya hali ya juu sana .

Amefafanua kuwa mashine hiyo ya kisasa inafanya kazi kwa haraka na kwamba tangu ianze majaribio hapo juzi mpaka leo tayari wagonjwa 26 wameshapimwa .

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Mseru amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa MNH itaendelea kutoa huduma bora za afya

1 comment:

  1. Picture is wrong. It is not of new CT scanner at Muhimbili. Reporter should visit and confirm.

    ReplyDelete

Maoni yako