Tuesday 31 May 2016

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU DAR-UDSM WAFANYA MGOMO

Wakati ambapo Wanafunzi wanaosomea kozi ya Ualimu wa Sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma kuamriwa waondoke Chuoni hapo, leo baadhi ya wanafunzi wa UDSM wamefanya mgomo kudai fedhha za kujikimu.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.

Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pesa hiyo haijaingizwa

Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.

Monday 30 May 2016

MWALIMU NYERERE KATIKA USAFIRI WA UNYENYEKEVU

Hapa kwetu Tanzania Julius Nyerere ni mfano wa viongozi walioishi maisha ya kadiri. Mwalimu aliishi kama alivyohubiri. Ni mfano wa kuigwa.

YALIYOJIRI BUNGENI LEO


MHE RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI

Mhe.Jaji Shaaban Ali Lila (Jaji Mahakama ya Rufani)
Mhe Mama Anna Makinda (NHIF)
Mhe Prof Apollinaria Elikana Pereka (DIT)

SERIKALI KUPIGA MARUFUKU MIFUKO YA PLASTIK NA POMBE ZA VIROBA

Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia mwakani.

Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.

Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba aliwaambia wanahabari jana sehemu kubwa ya mifuko hiyo inayotolewa bure imekuwa ikichangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa.

Wakati Makamba akiyasema hayo, Februari mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina aliondoa zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki akisema kuwa itaziweka rehani ajira za Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyo.

Pia, Mpina alisema itapunguza kasi ya uwekezaji wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo.

Akizungumza katika siku ya Mazingira Afrika, Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius Ningu alisema maamuzi hayo yamelenga kulinda viwanda vilivyoajiri mamia ya Watanzania, tofauti na nchi nyingine zinazotegemea wazalishaji wa nje ya nchi.

Makamba akizungumzia uamuzi mpya wa kuzuia mifuko ya plastiki, alisema matumizi ya mifuko inayofungashia vileo na inayotumika katika matumizi mengine husambaa na kuchafua mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa kuziba mifereji na kusababisha mafuriko na athari nyingine za mazingira.

“Leo (Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu mwingine utakaowekwa na Serikali,” alisema Makamba na kuongeza kuwa:

“Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo vya maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastiki.”

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.

Alifafanua kwamba Serikali itatoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha shughuli hizo na badala yake itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungashio mbadala.

“Kwa wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika soko la nje hatuna tatizo nao waendelee. Ila kwa soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio hili litakuwa la kisheria siyo kwa maneno,” alisisitiza Makamba.

Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008.

Waziri huyo alitoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko hiyo kujiandaa na zuio hilo na katika siku zijazo Serikali itatoa utaratibu na maelekezo ya tarehe ya kuanza zuio huku taratibu nyingine za kina zikifuata ili kuondoa mkanganyiko.

Katika hatua nyingine, Makamba alisema maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka hayatafanyika kitaifa badala yake wizara imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya maadhimisho katika maeneo yao.

“Tumewapa miongozo kuhusu utekezezaji wa shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga kutoa hamasa ya hifadhi ya mazingira hususan nyanzo ya maji amabayo ni muhimu kwa viumbe hai,” alisema Makamba.

Kwa mujibu wa Makamba, kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa juu ya maadhimisho hayo ni ‘ tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu’aliwashauri na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kupanda miti, kudhibiti uchomaji wa misitu

Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.

Alisema agizo la Waziri Makamba litawezekana, lakini linahitaji ushirikiano kutoka kwenye sekta zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya plastiki vipo Kenya.

"NEMC tayari tulishaanza mazungumzo na wazalishaji kuhusu mifuko ya plastiki,” alisema.

Sunday 29 May 2016

REAL MADRID MABINGWA CHAMPIONS LEAGUE KWA MARA YA !!

Real Madrid imetawazwa mabingwa wa Champions League baada ya kuitungua kwa Penati 5-3 timu ya Atletico Madrid

KATUNI ZA LEO

TAMASHA LA NYAMA CHOMA VIWANJA VYA LEADERS DAR

Mtaalamu wa kuchoma nyama kutoka mkoani Arusha, Jackson Isaya akionesha ufundi wa kuchoma nyama katika Tamasha la Nyama choma lililofanyika ,viwanja vya Learders Dar es Salaam jana

Friday 27 May 2016

VIDEO: KAULI YA MHE MAALIM SEIF YAMCHUKIZA MHE MREMA WA TLP

MARUFUKU KUVAA VIMINI NA KUTEMBEA NA WATOTO WADOGO USIKU KIJIJI SANYA HOE- KILIMANJARO

Moja ya matukio ambayo yanamake headlines katika Wilayani Siha Kilimanjaro ni pamoja na adhabu zinazotolewa kwa wale wanaovunja sheria, kingine ni kwamba kijiji cha Sanya Hoye kimepitisha adhabu ya faini ya Shilingi 50,000 pamoja na viboko 15 kwa atakayekutwa baa na mtoto mdogo au kuvaa nguo fupi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Sanya Hoye, Moses Mnuo ametoa ufafanuzi wa maazimio waliyokubaliana katika kikao cha kijiji cha Sanya Hoye………

‘Tumepitisha sheria kwa mtu yeyote anayevaa nguo fupi kwa watoto wa kike ni marufuku tangu siku ile ya kikao kile, wanawake hao wanapotembea hapa usiku wana ajenda walizonazo wanafanya machafu yao kwa hiyo tutawapiga faini na hizo hela watapewa risiti’ Sikiliza Hapa

DADA WA BILIONEA MSUYA AUAWA KINYAMA KIGAMBONI - DAR

Dada wa marehemu Erasto Msuya aliyetambulika kwa jina la Anathe Msuya ambaye alikuwa ni Mtumishi wa Wizara ya Fedha, ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana Dar es Salaam. Anathe aliuawa nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni, ambako inaelezwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Thursday 26 May 2016

ASKARI TRAFFIKI ANAYEONGOZA MAGARI KWA MAKINI NA MBWEMBWE DAR

YANAYOJIRI: TUZIDI KUMWOMBEA MEMA RAIS WETU MHE.MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’
Mwandishi wetu, Amani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’, huenda ndiye mtu anayeongoza kwa kupigwa juju kwa waganga wa kienyeji kuliko mtu yeyote nchini kwa sasa, Amani linakuja na ushuhuda.
Sangoma mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shark Abdullah ‘Kishapu’, akipiga simu kutoka jijini Tanga mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa katika miezi ya hivi karibuni, amekuwa akipata wateja, wakiwemo wafanyabiashara na watumishi wa umma wakimtaka kumpunguza kasi ya utendaji kiongozi huyo, wakisema inawaathiri.

Wednesday 25 May 2016

KATUNI YA LEO

RC WA DAR MHE PAUL MAKONDA AGOMEWA MKONO WA POLE NA BINTI WA MAREHEMU WILSON KABWE

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauti yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike

MHE MIZENGO PINDA (WAZIRI MKUU MSTAAFU) ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA

Tuesday 24 May 2016

MHE ZITTO KABWE ATAUKACHA UKAPERA MUDA SI MREFU

Picha ikimuonyesha Mhe Zitto Kabwe na Mchumba ake ambae alimvisha pete hivi karibuni

Sunday 22 May 2016

RAIS WA FIFA AWAPONGEZA YANGA (YOUNG AFRICANS SC)

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ameipongeza timu ya soka Young Africans ya Dar es Salaam, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.

Young Africans imetwaa ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo, lakini ikiwa ni mara ya 26 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara mwaka 1965.

Katika salamu zake, kupitia barua yake ya Mei 18, 2016 kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Infantino ameelezea ubingwa wa Young Africans kwamba umetokana na kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa timu hiyo, makocha, wachezaji pamoja na mashabiki.

“Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Young Africans na timu nzima isiyoshindika kwa mafanikio haya makubwa. Taji la Young Africans ni matokeo ya mshikamano ulioko ndani ya Young Africans,” amesema Infantino katika barua hiyo yenye kichwa cha habari kinachosema: Salamu za Pongezi kwa Young Africans.

Amesema pongezi zake ziende kwa uongozi wa klabu, makocha na benchi nzima la ufundi, wachezaji, madaktari pamoja na mashabiki wote wa Young Africans.

“Kwa niaba ya familia ya soka, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Young Africans na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa jinsi mnavyopeleka ujumbe chanya wa soka kwa jamii ya michezo,” alisema Infantino katika barua hiyo iliyotua TFF Mei 21, mwaka huu.

Tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikwisha kuipongeza Yanga ambayo imepewa Kombe na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji na kwa sasa wanasubiri zawadi ya fedha Sh 81,345,723.

SURA NNE ZA MHE.RAIS MAGUFULI

JAMII ya Watanzania imetakiwa kujifunza sura za Rais John Magufuli, kutokana na hatua yake ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.

Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu hatua hiyo ya Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, alisema Rais ametuma salamu kwa sura nne kupitia utenguzi huo.

Sura ya kwanza kwa mujibu wa Minja, alisema Rais amewakumbusha watumishi wote wa umma kwamba uadilifu ni jambo muhimu mahali pa kazi, na wanapaswa kuheshimu na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia muda na sio kutumia muda huo vibaya.

Pili, Minja alisema Rais ametuma salamu kwa walio karibu yake, kwamba uswahiba wao hauhusiani na kazi ya nchi, hivyo suala la kufahamiana si kigezo cha kiongozi avunjaye maadili kuachwa, bali wanapaswa kutambua nchi inaongozwa kwa Sheria na Katiba.

Akizungumzia sura ya tatu ya uamuzi huo, Minja alisema Rais amewakumbusha Watanzania kuwa haangalii muda gani amemteua kiongozi au muda gani ametumikia nafasi aliyopewa, bali kinachoangaliwa ni utendaji kazi wake kwa Taifa.

Aidha sura ya nne, imeelezwa kwamba Rais ameonesha kuwa haendeshwi kwa siasa za vyama kwa kuangalia wanasiasa watasema nini, hasa wakati huu wa uwepo wa Sakata la Kampuni ya Lugumi, na kusema alichoangalia ni kosa limetendeka muda gani.

“Kwa kweli Rais kaonesha ukomavu wake, ameonesha ni Rais mwenye msimamo, bila kusita amefanya uamuzi sahihi, hakuangalia vyama vya siasa vinasema nini, bali aliangalia maadili ya utumishi wa umma yanasema nini na kuchukua hatua,” alisema Minja.

UNAPORUDI NYUMBANI UMELEWA, JIANDAE KWA HILI

Mwanaume mwenye familia unatoka nyumbani ukidai huna hela , huachi hata mia kisha jioni unarudi nyumbani umelewa chakari., Jiandae kukutana na hili mezani,. Wanawake wa sasa hawataki mchezo. Familia kazi tu

Saturday 21 May 2016

KUMBUKUMBU YA MIAKA 21 YA KUZAMA MELI YA MV BUKOBA

ALICHOKISEMA MHE ZITTO KABWE BAADA YA WAZIRI KITWANGA KUSIMAMISHWA

Habari kubwa iliyoteka vyombo mbalimbali vya habari jana usiku ni habari ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo .

“Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “
Zitto Kabwe
14 hours ago
Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja - hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake.
Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ' no nonsense '

Thursday 19 May 2016

MUONEKANO WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR KATIKA MOJA YA VIKAO VYAKE

NDEGE YA MISRI (EGYPT AIR) YAPOTEA IKIWA NA ABIRIA 59

Ndege moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imepotea kutoka kwenye mitambo ya rada.

Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.
Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri.
Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.

BAADHI YA WAKUU WA MIKOA WAFANYA UTALII WA NDANI HIFADHI YA TARANGIRE

Wakuu wa Mikoa wakiwemo wakuu wa wilaya waliowakilisha mikoa yao wakiwa katika ofisi za Shirika za Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kimafunzo katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire

KIWANDA CHA SARUJI MBEYA CHAZINDUA NEMBO YA SARUJI "TEMBO FUNDI"

Tuesday 17 May 2016

ZITTO KABWE: TV NA REDIO TANZANIA ZIPIGE NYIMBO ZA WATANZANIA KWA ASILIMIA 80

May 13 2016 ilikuwa ni siku ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 .

Hotuba hiyo iliyosomwa na Waziri, Nape Nnauye ambapo kiwango kilichoombwa kilikuwa ni shilingi 20,326,176,000.

Wabunge mbalimbali walichangia bajeti hiyo huku Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe yeye alikuwa na haya ya kusema katika uchangiaji wake wa Wizara hiyo kuhusu muziki wa nyumbani:

“Leo hii ukifungua Redio au TV za hapa nyumbani zote asilimia nyingi utakuta wanapiga nyimbo za nje tu. Leo hii ukienda nchi za watu kuna limit mfano ukienda Lagos,Nigeria ukisikia nyimbo ya msanii wa huku kwetu basi ujue lazima atakuwa amefanya na msanii wao yaani wana promote wasanii wao, sasa sisi sijui ni ulimbukeni wa ukoloni wa miaka hamsini bado haujatutoka. Nape hili lipo kwako kama unataka kuwatetea wasanii hili wala halihiitaji kubadilisha sheria na kanuni za kontenti zipo chini ya waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki kuwa asilimia 80 ya nyimbo zitakazopigwa kwenye redio na TV zetu ziwe za wasanii wetu wa Tanzania basi,” alisema Zitto.

KIJIPU UPELE BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI

Barabara hii ilitengw akwa ajili ya haya mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi, lakini wananchi wengine bado wamekuwa wakaidi kutii amri ya kutotumia barabara hii kama wanavyoonekana katika picha

Monday 16 May 2016

VIDEO: MASANJA MKANDAMIZAJI AKIONGEA KUHUSU MHE RAIS MAGUFULI

MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI DAR BAADHI YA MASHINE YA KUTA TIKETI MBOVU TAYARI

Baadhi ya Abiria wakisubiri kununua tiketi ambapo wameambiwa mashine hizo kwa leo zina hitilafu maeneo ya Posta ya Zamani