Thursday 7 January 2016

SERA YA ELIMU BURE YAANZA KUTEKELEZWA RASMI:FEDHA ZATUMWA MASHULENI


KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3 kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Dk.Mipango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mipango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Beno Nduru akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Likwelile.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako