Sunday 28 February 2016

MIZIKI YA KALE ILIVYOKUWA INASAIDIA SERIKALI KIUSHAURI NA KIMATANGAZO

JAMANI NISAIDIENI MWENZENU NIMESHINDWA KUONA TOFAUTI ZA WATU HAWA WAWILI

MHE:RAIS MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUHUDHURIA MKUTANO WA !/ WA WAKUU WA EAC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.

Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Kabla ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tarehe 03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha – Holili – Taveta – Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.

Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

Dar es salaam

Saturday 27 February 2016

MSIBA: MMILIKI WA MABASI YA NGORIKA "MBERESERO" AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati akizungumza na simu.

Kamanda wa polisi wa MKOA wa Tanga Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo ilitokea juzi SAA 2;30 usiku katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya himo mjini Korogwe.

Alisema Mberesero ambae mabasi yake hufanya safari Kati ya mikoa ya Arusha,tanga,Daresalaam na singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya kituo cha mafuta cha Lake oil na kugongwa na gari hilo.

Mfanyakazi wa kampuni hiyo ,Adam Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe kuangalia Kiwanja kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta.

Kama unavyojua bosi wetu pamoja na kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam na Arusha,hivyo alipokuja Tanga alituambia anakwenda Korogwe kuangalia Kiwanja cha kujenga kituo kipya cha mafuta,alisema Adam.

Alisema bosi wake huyo alikuwa ameliweka gari lake katika kituo cha mafuta cha Lake oil na kwamba alishuka kwajili yakuelekea katika Kiwanja hicho.

Wengi waliokuwepo eneo la ajali hawakujua kama ni yeye hadi tulipokwenda kuchukua mwili wake ndipo wakashtuka,Alisema.

Kamanda Mihayo alisema wanamsaka Dereva aliyesababisha ajali hiyo kwa uzembe na kusababisha kifo.

SIJUI TUNAELEKEA WAPI......?

"Even satan wasn't Gay, he chose to approach naked Eve instead of naked Adam." - President Mugabe

Friday 26 February 2016

FIFA YAPATA RAIS MPYA: NI MHE. GIANNI INFANTINO

FIFA imemchagua Mhe. Gianni Infantino kutoka Uswisi kuwa Rais Mpya wa FIFA kuchukua nafasi ya Sepp Blatter aliyeachia ngazi kwa kashfa mbalimbali. Mhe Gianni alikuwa Katibu wa UEFA alipata kura 115 dhidi ya mpinzani wake Shekh Salman al Khalifa. Rais huyu mpya ameahidi kurudisha heshima ya FIFA.

"BANGI HAIONJWI"

WAJAWAZITO MMELIONA TANGAZO/ANGALISHO HILI?

MSIBA: MWANAMUZIKI MKONGWE MZEE KASSIM MAPILI AFARIKI DUNIA

Nimepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Muziki Tanzania na mwimbaji wa muziki wa injili Ado November ambazo zinasema nanukuu ” Nimepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa za Kifo cha Mzee wetu Mzee Mapili”…
Breaking News…. Tanzia…. Mwanamuziki Mkongwe Kassim Mapili amefariki leo jioni baada ya kuonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu…. Ndipo mlango ukavunjwa nyumbani kwake Tabata Matumbi… Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha Napenda Nipate Lau Nafasi na Rangi Ya Chungwa…Taarifa zaidi zitawajia…!! Plz call 0744150000 Kama una swali… Nawaomba wanamuziki wote Tujitoe kwa wingi kumpa heshima Mzee wetu Mapili….!! Addo November Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!
Mwanamuziki mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band

MSAADA WA VIFAA-TIBA KUTOKA AZAM,PEPSI NA COCA COLA

Umoja wa Wazalishaji Vinywaji laini umetoa msaada wa vifaatiba vyenye thamani ya Sh Bilioni Kumi vilivyopokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Vifaatiba vilivyopokelewa jana ni pamoja na mashine za aina mbalimbali kama utra sound, mashine za kustulia moyo, vitanda vya watoto njiti, vitanda vya kujifungulia, vitanda 80 vya kawaida na magodoro yake, ambavyo viliwekwa kwenye makontena 20.

“Haijapata kutokea msaada mkubwa kama huu,” alisema Majaliwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ghala la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) iliyoko Mabibo, Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Natoa wito kwa makampuni mengine binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali.”

Msaada huo wa vifaa tiba unawalenga zaidi watoto na wajawazito, ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha huduma za afya.

PICHA: GUESS WHO?

Thursday 25 February 2016

TANZANIA KUWA TAJIRI WA GESI ASILIA

Tanzania imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.

Ugunduzi huo wa gesi asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta katika Mkoa wa Pwani.

Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani bilioni sita sawa na Sh trilioni 12.

Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.

Kwa upande wake, Profesa Muhongo alithibitisha kugundulika kwa gesi hiyo tangu Julai mwaka jana, lakini akaeleza kuwa Serikali imechelewa kutangaza ugunduzi huo kama inavyoagizwa na Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kutokana na shughuli za uchaguzi.

“Sheria mpya inatutaka kabla ya waziri mwenye dhamana ya gesi kutangaza ugunduzi mpya wa gesi na mafuta ni lazima athibitishiwe na mamlaka ya udhibiti wa bidhaa za Petroli na Gesi (PURA).

“Wizara yangu itawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kupata ushauri wa kisheria kuhusu jambo hilo na bahati nzuri tayari PURA imeshaanza kushughulikia jambo hilo na naamini kuwa nitatangaza ugunduzi huo mpya hivi karibuni,” alifafanua Profesa Muhongo.

Licha ya ugunduzi huo mpya tayari gesi imegundulika katika maeneo ya kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na eneo la Mnazi Bay huko Mtwara na katika Wilaya ya Mkuranga, Pwani pia kumegundulika kiasi kikubwa cha gesi.

Wednesday 24 February 2016

VURUGU ZASABABISHA CHUO KIKUU (ARUSHA CAMPUS) KUFUNGWA

Uongozi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph tawi la Arusha umekifunga chuo hicho kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kufanya vurugu chuoni hapo.

Inaelezwa kuwa, wanafunzi wa chuo hicho wamekuwa katika hali ya wasiwasi wakihofia chuo chao kufungwa na serikali kama kilivyofungwa St. Joseph tawi la Songea

Wanafunzi wote wameamriwa kuondoka chuoni na wametakiwa kusoma magazeti au kutembelea tovuti ya chuo hicho ili kujua hatima yao.

UDAKU: NYUMBA YA WATU ZINA MAMBO

HESHIMA NA UNYENYEKEVU WA MWANAMKE WA KIAFRIKA

Balozi wa Zambia nchini Mhe Judith Kangoma-Kapijimpanga akimsalimia kwa unyenyekevu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne February 23, 2016

Tuesday 23 February 2016

HAPPY BIRTHDAY H.E PRESIDENT MUGABE

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza umri wa miaka 92 huku chama chake kikisema atawania tena urais 2018.
Mnadhimu wake mkuu alisema kiongozi huyo ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 1980, bado ana uwezo kamili wa kuongoza Serikali licha ya tetesi kwamba hawezi kuongoza kutokana na umri.
Akizungumza na gazeti la Serikali Sunday Mail, Katibu Mkuu wa Rais Misheck Sibanda alisema tetesi hizo si za kweli na hazina msingi kwani Rais Mugabe ana ratiba ya wiki nzima kutekeleza kazi za Serikali na chama

Monday 22 February 2016

USAFIRI WA KWENDA NYUMBANI

JIJI LA MWANZA LAZIDI KUNOGA

Baada ya Serikali kukamilisha Ujenzi wa Darala la juu la Watembea kwa Miguu katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza na kupunguza wingi wa ajali pamoja na msongamano wa magari katika eneo hilo, Sasa juhudi zimehamia katika eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia linajengwa Daraja la juu la Watembea kwa Miguu ili kukabiliana na foleni katika eneo hilo ambalo limejengwa pia Kitega Uchumi cha Kisasa cha Rock City Mall ambayo ni Mall (Soko) Kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

YAMOTO BAND - MAMA

Saturday 20 February 2016

MHE YOWERI MUSEVENI ATANGAZWA MSHINDI WA KITI CHA URAISI UGANDA

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi. Rais Museveni amepata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu. Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye amepata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.

YANGA KIDEDEA

Leo Februari 20 ndio siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka la Tanzania, kwani ndio siku ambayo mashabiki wa soka la Tanzania wamepata nafasi ya kushuhudia mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu, baada ya mchezo wa mzunguuko wa kwanza kumalizika kwa Yanga kuifunga Simba goli 2-0.

Dk 90+ 3: Mpira umemalizika, Yanga SC inaifunga Simba SC 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Donald Ngoma kipindi cha kwanza na Amissi Tambwe kipindi cha pili
Dk 90+ 1: Yanga wanapata kona ya kwanza, lakini haina faida
Dk 87: Simba SC wanapata kona tena inazua kizaazaa langoni mwa Yanga kabla ya kuondoshwa kwenye hatari
Dk 82: Mashabiki wa Simba SC wanaanza kuachia siti zao Uwanja wa Taifa
Dk 80: Brian Majwega anakwedna kuchukua nafasi ya Ibrahim Hajib
Dk 72: Tambwe anaifungia Yanga bao la pili kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Godfrey Mwashiuya kutoka kushoto

Dk 45: Hassan Kessy anapiga mpira wa adhabu unapotea
Dk 44: Simba wanapata kona ya saba wanapoteza pia
Dk 44: Simba wanapata kona ya sita wanapoteza
Dk 39: Ngoma anaifungia Yanga bao la kwanza. Hassan Kessy alimrudishia pasi fupi kipa Vincent Angban, Ngoma akainasa akampga chenga kipa huyo na kufunga
Dk 35: Simba SC wanapata kona nyingine dakika ya 35, lakini inaokolewa
Dk 25: Abdi Banda anaonyeshwa kadi ya njano ya pili na kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu tena Ngoma

Friday 19 February 2016

UDAKU:BAADA YA RAY KIGOSI KUSEMA ANAKUNYWA MAJI NDO YAMEMFANYA MWEUPE.........

DARAJA LA KIGAMBONI LAKAMILIKA KWA ASILIMIA 99.5

daraja hilo la Kigamboni Jijini Dar es Salaam linatarajiwa kuwa limekamilika hivi karibuni baara ya njia ya kuingia na kutoka katika Daraja hilo kukamilika ujenyi wake. Linasubiriwa kwa hamu sana maana ni kiungo kizuri kati ya sehemu hizi mbili za Jiji la Dar ambapo kwasasa wanahudumiwa zaidi na Ferry/Kivuko

WAJUE WANAFUNZI WALOSHIKA NAMBA 1 na 2 KITAIFA KIDATO CHA NNE 2015

Huyu ndiye mwanafunzi bora wa kwanza Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha Nne 2015, Butogwa Charles Shija kutoka Canossa Sekondari ya Wasichana
"Mtanzania" Congcong Wang, mwenye asili ya China; ameshika Nafasi ya PILI KITAIFA, huku akipata Divisheni 1.7 yenye 'B' ya Kiswahili!
Amemaliza Kidato cha Nne FEZA GIRLS - 2015

IGP ATANGAZA OPERESHENI KWA BODABODA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amewataka Makamanda wa Polisi kote nchini kuendesha oparesheni kali ya kuwachukulia hatua kali za kisheria waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu pamoja na kutovaa kofia ngumu
(Taarifa hii kwa hisani ya Frank Geofray wa Jeshi la Polisi.)

Thursday 18 February 2016

VIONGOZI WA JUU WA KITAIFA WAYASHUKURU MAKUNDI WALOSHIRIKI NAO KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU "=!%

Mhe Rais John Magufuli akitoa shukrani
Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu akitoa shukrani
Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Kassim akitoa shukrani
Wananchi waliohudhuria halfa hiyo ya shukrani

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAMETOKA

Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80. Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu

http://tanzania.go.tz/matokeo_2015/CSEE2015/indexfiles/index_m.htm

http://tanzania.go.tz/matokeo_2015/CSEE2015/indexfiles/index_m.htm

Wednesday 17 February 2016

KARIBUNI MGAHAWA "MASANJA WALI NYAMA"

Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji siku ya jana amezindua Mgahawa wake wa Kisasa unao fahamika (Masanja Wali Nyama) Maeneo Ya Tabata Magengeni Karibu na CRDB BANK. Shughuli hiyo iliyo anza saa mbili usiku na kumalizika saa tano usiku, ilipambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa Gospel akiwemo Miriam Jackson,Emmanuel Mbasha,Faraja Ntaboba,Mc Makondeko,Stella Joel pamoja na Wachungaji,Mitume na Manabii.
Sura ya Mgahawa huo
Mmiliki wa Mgahawa huo Masanja Mkandamiyaji katika taswira mbalimbali na Wadau
Baadhi ya Watendaji/Wahudumu katika Mgahawa wa "Wali Nyama"