Wednesday 20 March 2013

Sunday 17 March 2013

TAFAKARI YA LEO

MAMBO 30 YANAYOKUONYESHA KUWA SASA UMRI UMEKUTUPA
MKONO....ushakuwa mtu mzima...:

1. Huna muda wa kushinda na
mpenzi wako kutwa nzima mkipiga
stori za mapenzi
2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali
unakokufikiria ni kitandani
3. Unaanza kujaza friji lako kwa
vyakula zaidi kuliko pombe
4. Muziki unaoupenda unausikia
ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari
lako ukienda na kutoka kazini
5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda
unaoamka, na siyo muda tena
unaorudi kulala
6. Unatazama taarifa ya habari hadi
utabiri wa hali ya hewa
7. Rafiki zako wanakualika zaidi
kwenye vikao vya harusi kuliko
mtoko wa kwenda Maisha Club
8. Ukienda dukani kununua kitu
unakuwa na juhudi sana ya kuomba
upunguziwe bei
9. Idadi ya tisheti na jinsi inapungua
kwa kasi kwenye kabati lako la nguo
10.Wewe ndiyo unayekumbuka
kuwapigia simu polisi endapo
mtaani kwenu kuna vijana wavuta
bangi wanaowasumbua
11. Ndugu zako watu wazima
wanajisikia kawaida tu kufanya utani
wa kiutu uzima mbele yako
12. Hukumbuki tena Azam Ice
Cream na Samaki Samaki wanafunga
saa ngapi
13. Timu yako ya mpira ikifungwa
hutaki tena kutaniwa na watu
14. Wanyama uwapendao kama
mbwa na paka unawaandalia chakula
kwa kanuni za kisayansi badala ya
kuwapa mabaki uliyotoka nayo
Subway ama Steers
15. Ukilala kwenye kochi unaamka
mgongo unakuuma sana
16. Unaithamini sana ratiba yako ya
kulala
17. Ukiwa nyumbani unaanza
kutumia muda wako wa ziada
kulima lima bustani ya maua ama
mbogamboga badala ya kutazama
filamu na kuzurura
18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani
jambo la kwanza unalouliza,
"Umenunua sh' ngapi?"
19. Unakwenda duka la madawa
kununua Ibuprofen na Antacid, siyo
kondomu tena wala kipima mimba
20. Unaanza kununua magazeti ya
Mwananchi, The Express, Citizen na
Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa,
Kiu na Amani
21. Unapata kifungua kinywa kwa
wakati
22. Ukiwa baa unanunua bia
unazohitaji wewe badala ya kusema
"zungusha kama tulivyo"
23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia
kwenye kompyuta yako unautumia
kufanya kazi badala ya kuchati
24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi
unaanza kunywea nyumbani ili
kupunguza gharama kabla hujaenda
baa
25. Ukimwona rafiki yako yu
mjamzito unampongeza sana badala
ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"
26. Ukienda kutembea mahali
unaulizia bei za viwanja
27. Hupendi tena kuwaazimisha
marafiki zako magari yako
28. Ukiwa na rafiki zako unapenda
kujadiliana nao kuhusiana na
mfumuko wa bei na mfumo mbovu
wa utawala
29. Ukiwa unakula chakula unakuwa
mkali ikitokea chakula kimewekwa
mafuta mengi ama chumvi nyingi
30. Ukimaliza kusoma kanuni hizo
29 hapo juu unaanza kuhesabu
ambazo unaingia wewe.
Ukiona una nusu ya sifa hizi 30 basi
huhitaji kupigiwa kengele
kukumbushwa kuwa umri
ushayoyooooooooooooooooooo

JE WAJUA????

Ukiwa Dar es Salaam maduka ya mchele huwa yanajinadi kwa mbwembwe MCHELE SAFI KUTOKA MBEYA

Ukishafika Mbeya unakutana na maduka ya mchele yakijinadi
PATA MCHELE SAFI KUTOKA KYELA

Ukifika zako hapo mjini Kyela unakutana na maduka ya mchele nayo yakijinadi
TUNAUZA MCHELE SUPER KUTOKA IPINDA

Unakufahamu Ipinda wewe? Ukishafika unakwenda zako duka la mchele. Mwuzaji anakwambia
HUU NI MCHELE SUPER KABISA KUTOKA BONDE LA TENENDE

Halafu ikitokea ukazurura hadi Tenende wenyeji wanakwambia MCHELE SUPER NI ULE WA SHAMBA LA MZEE MWAKIPESILE.

Unashangaa? Kila kizuri kina kizuri zaidi yake.

WEEKEND NJEMA


Thursday 14 March 2013

Ubunifu mwingine bhana!!!!!


HATIMAYE: POPE FRANCIS 1



Baada ya kupiga kura za siri kwa siku mbili huku wakiongozwa na Roho mtakatifu, makardinali wa kanisa katoliki wamemchagua Jorge Mario Bergoglio kutoka Argentina kuwa Baba Mtakatifu. Amechagua kuitwa Papa Francis 1.

Tuesday 12 March 2013

KANISA KATOLIKI-UCHAGUZI WA PAPA MPYA

Leo Makardinali zaidi ya 112 baada ya sala katika kanisa la St.Peter's Basilica huko Vatican Rome, wameingia kwenye chumba cha siri cha mikutano kinachojulikana kama @CONCLAVE@ kwa ajili ya kusali na kupiga kura za siri sana ili kumchagua Papa atakayechukua nafasi ya Papa Benedict XVI ambaye alijiuzulu 28 Februari  kwa sababu za uzee na kiafya. Papa atakayechaguliwa ni wa 266.

Thursday 7 March 2013

NDOTO NJEMA

Mtu utakavyokuwa baadae huanza tangu mtoto. Pengine wewe mwenyewe kama mtoto waweze kuanza kuonyesha viashiria hivyo au wanaokuzunguka wanaweza kukusaidia kukutambulisha utakavyokuwa baaadae. Ni muhimu hapa kulea vipaji vyetu ili kitimiza ndoto zetu.
 Yaonekana atakuwa kiongozi mzuri
 Yawezekana akawa Mtendaji mzuri wa shughuli za kijamii
Yawezekana akawa mwindaji mzuri sana

Wednesday 6 March 2013

ELIMU HAINA MWISHO.

Tuige mfano wa mzee huyu pengine matokeo mabaya katika mitihani yangepungua.

MCHANA MWEMA

Leo mchana twaenda Mbeya zaidi kukutana na "Ndookani/Ndoofwani"

MAMBO YA OLD TRAFFORD


RIP HUGHO CHAVEZ


Tuesday 5 March 2013

DANGANYA TOTO

Wakati bado tunajiuliza kulikoni kuhusu matokeo mabaya ya Kidato cha nne 2012, hili nalo ni la kutupia macho, lisibaki kichekesho tu

UJUMBE WA LEO


Katika harakati hizi za kujikwamua kimaisha, ujumbe huu watukumbusha jambo fulani. Si vibaya kwa wale walioguswa kuzingatia undani wa ujumbe huu. Tafadhali usiusome ujumbe huu kwa papara na kukimbilia kulalamika au kukosoa.

MOTO-LEO

Moto umetokea tena leo na kuunguza baadhi ya ghala katika eneo la Uwekezaji la Shekilango Jijini DAR. Bado haijajulikana vizuri moto huo ulianzia wapi, ila mpaka picha hii inapigwa bado moto huo ulikuwa haujaweza kuzimwa kutokana na moshi mweusi kutanda juu ya eneo hilo na kusababisha usumbufu wa wahusika wa zima moto. Ikumbukwe kuwa moto huu unatokea baada ya tukio kama hili kutokea huko Mbezi- Kiwanda cha Chemi and Cotex, Mwenge madukani kwenye kituo cha Daladala na juzi tu huko Tegeta.

INATIA HURUMA

Wakati kila mmoja anajaribu kupambana kutafuta unafuu wa maisha, tunapaswa kwa wakati huo kuangalia wale ambao bado hawajiwezi kujitafutia wenyewe kama watoto hawa. nani anasikia kilio chao. Kilio hiki kinatokana na mambo mengi ya kimaisha, pengine ni ukosefu wa lishe, makazi, vita, ugomvi baina ya wazazi na mengine kama hayo. Ni wakati ambapo Serikali na watu husika waangalie hili maana inatia huruma.

Monday 4 March 2013

MVUA KIDOGO DAR LEO

Dar es Salaam , leo Mungu alitujalia baraka ya mvua lakini adha yake anaijua mwenyewe aliyeileta

BENKI ZA TANZANIA MPOOOOO