Wednesday 13 January 2016

FAST JET YAANZA SAFARI ZA DAR-NAIROBI

Mkurugenzi asiye mtendaji wa kampuni ya ndege ya Fastjet Balozi Ami Mpungwe, akizungumza na wasafiri wakati wa kuanzisha safari za ndege hiyo kwenda Nairobi kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam, kutoka kulia ni mkurugenzi asiye mtendaji Lawrence Masha, Meneja mkuu wa kampuni hiyo (Afrika Mashariki) Jimmy Kibati na Meneja wa mahusiano kati ya Fastjet na Serikali, Mhandisi August Kowero.
Ndege ya Shirika la Ndege la fastjet ilikiwasili kwenye uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwa mara ya kwanza baada ya kuanza safari zake kati ya Dar es Salaam na Nairobi nchini Kenya
Meneja mkuu wa kampuni hiyo (Afrika Mashariki) Jimmy Kibati juu pamoja na wafanyakazi wa Ndege hiyo wakishuka kwenye ndege mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya.
Kampuni ya ndege ya Kiafrika yenye gharama nafuu fastjet,imepanua mtandao wake wa safari barani Afrika kwa kuwa na safari za kimataifa za kila siku kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro kwenda Nairobi na hali kadhalika safari za ndani za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar.

Uzinduzi wa safari za anga za fastjet kutoka Dar es Salaam hadi Nairobi, Kilimanjaro hadi Nairobi na Dar e s Salaam kwenda Zanzibar zote zimefanyika Januari 11, 2016 na hivyo kufanya iwe ni hatua muhimu katika kujipanua katika safari zake kimataifa na kitaifa.

Safari za kila siku kwenda Zanzibar zinatarajiwa kuwarahisishia watanzania walio wengi pamoja na wageni wa kimataifa kuitembelea Zanzibar,kukuza utalii na biashara pamoja na kuchangia kwa kiwango kikubwa kwenye kukua kwa uchumi visiwani humo.

Kuzinduliwa kwa safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam kunaanzisha enzi mpya ya abiria ambao wamekuwa wakitaabika kwa tozo kubwa ya nauli kwa usafiri wa anga kati ya nchi mbili za Afrika Mashariki ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

Matokeo ya safari za fastjet nchini Kenya tayari yameshaanza kujadiliwa, yakikolezwa na ukweli kwamba nauli dhidi ya mashirika washindani yanayofanya safari kati ya nchi hizi mbili ambako ni kushuka kwa kasi hadi ya asilimia 40 siku ya kwanza tu tangu fastjet

ilipotangaza kuanzishwakwa safari zake kati ya Kenya na Tanzania.

Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania John Corse anasema, “ukweli ni kwamba ushindani ni mzuri kwa abiria. Unaleta nafasi kuchagua jinsi ya kusafiri na pia unasababisha nauli kushuka.”

Nauli za fastjet kimsingi ziko chini kuliko nauli zinazotozwa na mashirika mengineya ndege ambayo hivi sasa yanafanya safari kati ya Tanzania na Kenya ambapo nauli za fastjet kutoka

Kilimanjaro/Nairobi ni kuanzia dola 50 kw safari moja na ya kwenda Dar es Salaam/Nairobi

ni dola 80 kwa safari moja. Nauli hizo hazijumuishi kodi za serikali ambazo ni dola

49kwa kuondokea Tanzania na dola 40 kwa kuondokea Kenya na hivyo fastjet

kuwashauri abiria kukata tiketi zao mapema ili kuitumia fursa hiyo ya nauli ya bei

nafuu. fastjet inatarajia kuongeza safari moja zaidi kwenye niia yake mpya ya Kenya

kutokan ana mahitaji ya wateja kuongezeka kutokana na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati na tayari imeshaonesha kwamba inatarajia kuzindua safari kati ya

Zanzibar na Nairobi na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka huu 2016.

“Kama ambavyo imekuwa kwa njia zetu nyingine ambazo fastjen timezindua tunatarajia abiria wetu walio wengi kwenye njia yetu mpya Kenya kuwa abiria wa kwanza ambao huenda wasingemudu kusafiri kwa njia ya anga hapo awali,” anabainisha Corse.

Matarajio haya yanaungwa mkono na utafiti uliofanywa na fastjet ambao unaonesha

Kuwa zaidi ya theluthi moja ya abiria watakuwa wanasafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza na hali kadhalika kumudu usafiri huo kwa mara ya kwanza.

“Usafiri wa anga ambao abiria wanaumudu ni msingi wa kukua kwa uchumi barani Afrika kutokana na matokeo chanya yanayosababishwa na bei nafuu ya usafiri wa ndege kwa maisha ya wananchi na uchumi kwa jumla,”alisema Corse.

“Tunazishukuru wizara za usafirishaji na mamlaka za usafiri wa anga za Tanzania na Kenya kwa kufanya kazi pamoja kuwezesha fastjet kutambua dira yetu ya kuongezeka kwa idadi ya wateja ambao wanaweza kufikia usafiri wa anga wanaoumudu,” alihitimisha Corse.

Jambo ambalo lina umuhimu zaidi kwenye njia hii mpya ni njia mbadala ya kuibeba mizigo inayojulikana kama “freighty” ambayo inaruhusu abiria kusafiri na mzigo hadi kilo 80 kwenye mabegi kwa dola 80. Mbadala huu wa mzigo kimsingi unatarajiwa kuwa maarufu kwa wafanya biashara wanaosafiri na fastjet kununua bidhaa za jumla na kuzisafirisha kwa ajili ya kuuzakwenye masoko ya ndani. Ukataji tiketi unaweza kufanyika kupitia mtandao wa www.fastjet.com, kupitia wakala waliothibitishwa na fastjet au kwa njia ya mawasiliano ya simu: +255-784-108900. Malipo ya tiketi yanaweza kufanyika kwa fedha taslim, kwa njia ya mtandao au kupitia malipo kwa njia ya simu

No comments:

Post a Comment

Maoni yako