Monday 30 November 2015

UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO KWA KUTUMIA PESA ZA SHEREHE UA UHURU 2-15

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
Tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo
Kujengwa kwa njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati huo huo, Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokonga nyoyo za Watanzania.
Kwa Upande wake Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.

30 Novemba,2015
Sehemu ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo.

PICHA NA IKULU

Mhe.RAIS MAGUFULI NA MHE.WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WAMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS MHE.SAIA SULUHU OFISSINI KWAKE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.

Saturday 28 November 2015

KATUNI ZA LEO: KUTUNDUA MAJIPU KAZI

HAPA KAZI TU

KAMISHNA MKUU TRA AFUTWA KAZI


Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemsimamisha kazi kuanzia jana tarehe 27 Nov. 2015, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kasimu Majaliwa mapema jana asubuhi Bandarini jijini Dar

Friday 27 November 2015

WAZIRI MKUU MHE.MAJALIWA AFANYA ZIARA BANDARI NA KUTOA MSIMAMO


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.

Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.

Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo

Thursday 26 November 2015

PAPA FRANCIS AITEMBELEA KENYA


Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na kumpokea Kiongozi wa kanisa la katoliki duniani Papa Francis muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya

Wednesday 25 November 2015

MILION 90 HAZITOSHI KUNUNUA GARI

Mbunge anayedai leo kuwa milioni 90 hazitoshi kununua gari ya maana kufanyia kazi zake za kibunge, basi, wapiga kura waliomchagua mbunge kama huyo wajihesabu wamekula hasara, ama kwa lugha ya mitaani ' Imekula kwao'.
Mbunge kama huyo atakuwa ameonyesha mawili na kwa wazi ; ama amekosa kabisa sifa ya ubunifu, kwamba hata pale wapiga kura wake wangemkabidhi milioni 50 aende Dar na arudi na gari la wagonjwa jimboni, mbunge kama huyo angewaangusha, au, ni mbunge aliyeingia bungeni kwa kujali zaidi maslahi yake binafsi kuliko kutambua hali halisi za wapiga kura wake. Inasikitisha.
Wakai hayo yakiendelea, picha juu yaonyesha moja ya Gari analotumia mmoja wa maraisi "simple" duniani. Je kwa Milioni 90 Rais huyu angenunua magari mangapi kama hilo pichani?

Monday 23 November 2015

KAZI IPO

Video hii yaonyesha maamuzi ya Mhe.Rais Kikwete kuhusu Sherehe za Uhuru wa Tanzania hapo dec.9 mwaka huu

Kwa mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike kwa kufanya kazi. Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu. Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.
Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.

Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo, sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.

Sunday 22 November 2015

HUYU NDIO RAIS JPM: "HAPA KAZI TU"

AGIZO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU MSAADA MUHIMBILI LAANZA KUTEKELEZWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wabunge na wageni waalikwa kwenye mchapalo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. Ni hapo alipoamuru kwamba zaidi ya shilingi milioni 200 zilizochangwa na wafadhili kwa ajili ya mchapalo huo zitumike kwa kununulia vitanda vya wagonja katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Saturday 21 November 2015

MARAIS WA TANZANIA WA AWAMU YA 2-5

FURAHA KWENDA MBELE. CCM MBELE KWA MBELE

Friday 20 November 2015

video: HOTUBA YA WAZIRI MKUU BUNGENI LEO


video:WABUNGE WA UKAWA WALIYOTENDA LEO BUNGENI WAKATI MHE RAIS MAGUFULI ALIPOINGIA KUHUTUBIA

WAZIRI MKUU MH.MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AAPISHWA RASMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akimuapisha Kassim Majaliwa Kassim kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni, hafla ya kiapo ilifanyika leo Ikulu ya Chamwino Mkoa wa Dodoma
Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa baada ya kumwapisha Waziri Mkuu kwenye ikulu ndogo ya Chamwinomjini Dodoma Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mhe.Waziri Mkuu akipongezwa
Picha zaidi za tukio
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mtoto Majaliwa mtoto wa Waziri Mkuu mpya kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akimpongezwa na mkewe baada ya kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini Dodoma, leo Nov 20, 2015
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim (watatu kushoto mstari wa nyuma) baada ya kuapishwa rasmi leo katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma,Picha na Ikulu.

MHE.RAIS MAGUFULI AZINDUA NA KUHUTUBIA BUNGE LA 11 LA TANZANIA


KATUNI YA LEO

Thursday 19 November 2015

MHE. DK.TULIA ACKSON MWANSASU ACHAGULIWA KUWA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA 11 LA TANZANIA


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mhe.Dkt. Tulia Akson kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Spika wa Bunge la 11 baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Magdalena Sakaya.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mhe. Dkt. Akson kushinda kwa kura 250 ambazo ni sawa na asilimia 71.2 za kula halali dhidi ya mpinzani wake Mhe. Sakaya aliyepata kura 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 ya kura halali.

MHE.KASSIM MAJALIWA APITISHWA KUWA WAZIRI MKUU WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA


WAZIRI Mkuu mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa amesema hakutegemea nafasi ya jina lake kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa wa nafasi hiyo kubwa katika Serikali.
Alisema Uteuzi huo ulioidhinishwa na Bunge, umedhihirisha imani ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyonayo kwake iliyomwongoza katika kuliwasilisha jina lake Bungeni.
Akizungumza mara baada ya zoezi la uthibitisho wa uteuzi wa jina lake Bungeni Mjini Dodoma (leo), Mhe. Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa alisema kilichopo mbele yake kwa sasa ni kuwatumia Watanzania pasipo kujali itikadi ya vyama vyao.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuanza kazi yake atahakikisha anazunguka katika mikoa mbalimbali nchini ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania na maendeleo yaliyofikiwa katika sehemu mbalimbali.
Aidha Mhe. Majaliwa aliwahakikishia Wabunge ushirikiano wa karibu zaidi katika kupokea ushirikiano ili kuweza kuwaletea maendeleo ya haraka Watanzania.
Awali akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na Wabunge wa Bunge kwa ajili ya kuidhinisha jina hilo, Msimamizi wa jina hilo ambaye ni Katibu wa Bunge, Thomas Kashilill ah alisema katika uchaguzi huo, Mhe. Majaliwa alipata kura za Ndiyo 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote.
Aidha Kashilillah alisema kura 91 sawa na asilimia 25% ya kura zote zilisema hapana wakati kura 2 sawa na asilimia 0.06% ya kura zote ziliharibika.
Wakizungumzia uteuzi huo, Wabunge mbalimbali Bunge la Jamhuri ya wamesifu uteuzi waMhe. Kassimu Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kusema ni kiongozi mwadilifu, mchapakazi na asiye na makundi.
Alikotoka ni mbali ni tangu enzi za "Masantula/Santana na Pekosi"

Tuesday 17 November 2015

MHE.JOB NDUGAI: SPIKA MPYA WA BUNGE LA 11 LA TANZANIA

MATOKEO:- 1. Job Ndugai CCM - kura 254 au 70% 2. Ole Medeyi Chadema kura 109 wengine wote wameishia kupata 0 au 0%, kwa hiyo Mh. Job Ndugai ndiye Spika mpya wa Bunge la Awamu ya Tano

MHE RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA KWANZA WA MBUNGE: NI Mhe. TULIA A. MWANSASU

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU AONGEA NA VIONGOZI WA DINI MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Mahusiano ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma Nov 16, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma, baada ya mkutano uliofanyika Nov 16, 2015 kwenye Ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma

Sunday 15 November 2015

DUNIA YALAANI TUKIO LA UGAIDI PARIS: RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA POLE

Rais John Magufuli amemtumia salamu za pole Rais wa Ufaransa François Hollande, kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyogharimu vifo vya watu 127. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rais Magufuli alisema Serikali yake inaungana na wapenda amani wote duniani kulaani tukio hilo lililogharimu maisha ya watu wengi.

Saturday 14 November 2015

KUMBE WALIKOTOKA PAMOJA NI MBALI.

Inaelekea kipindi chote walikuwa na lao moyoni.
Wakiwa CCM
Wakiwa UKAWA(CHADEMA)

Friday 13 November 2015

MHE.ANNA MAKINDA: SITAGOMBEA KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika siasa.
ALIYEKUWA Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda amejing'atua rasmi na kuachana na uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.

SASA OFISI YA RAIS NI YAKO RASMI


Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi rasmi Ofisi ya Rais. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue