Wednesday, 6 January 2016

MHE RAIS OBAMA ATOA MACHOZI AKITETEA WANANCHI WAKE


Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa Risasi nchini humo. Obama aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatetea ni kwa manufaa yao wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na wala hana mpango wa kugombea.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako