Saturday 31 January 2015

MSONGAMANO WA MAGARI BARABARANI DAR

Hili sasa limekuwa tatizo kubwa. Watu siku hizi Dar wanatumia muda mwingi barabarani kuliko maofisini, kwenye biashara,shuleni na hata nyumbani. Msongamano umezidi. Serikali tupieni macho jambo hili pamoja na juhudi kbwa zinazoendelea hadi sasa.

RAIS ROBERT MUGABE MWENYEKITI MPYA WA AU

Umoja wa Nchi za Africa (AU) umemteua mhe. Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja huo katika kikao kinachoendelea huko Addis Ababa Ethiopia.
Na hapa ni Mhe.Rais Kikwete akiwa katika kikao hicho huko Addis Ababa Ethiopia

MHE. RAIS KIKWETE ZIARANI UFARANSA

Akikagua kwaride la heshima Ikulu ya Ufaransa, na pia akisalimia na Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande

Friday 30 January 2015

VITUKO VYA WADADA WA KAZI

Wazazi ni muhimu kuwa makini sana na hawa wasaidizi. Utakuwa unashangaa mwanao kila siku malaria na net ulinunua. Mwezio dada wa kazi ndo anaitumia
Halafu usishangae hali hii inaweza kupelekea mambo kama haya kutokea kwa watoto

NDOTO YAKO NI YAKO, USIKATISHWE TAMAA

TULIKOTOKA NI MBALI: WABUNGE ZAMANI HIZO

Thursday 29 January 2015

USAFIRI WA UHAKIKA NA WA RAHA

Mabasi ya Kampuni ya SHABIBY yameendelea kushika kasi kwa usafiri mzuri wa DAR/DODOMA/DAR

Wednesday 28 January 2015

NIMESHINDWA KUCHEKA NIMESHINDWA KULIA

Kitendawili cha maisha Bora kwa kila mtanzania kinapokosa majibu. Kwakweli bado tuna safari ndefu....

MWEZI JANUARI UNATISHA

Kutokana na matumizi mengi ya kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka 2014, na majukumu mengi ya mwanzo wa mwaka, wengi pochi zao zipo tupu, Tarehe zza mwezi hu zinavyosogea, ni kama vile wanatamani kuiuliza Google iwape majibu

DHARAU NYINGINE JAMANI UUUH......

TUJIFUNZE KUMUHESHIMU KILA MTU HATA KAMA UNA MALI NYINGI KIASI GANI IPO SIKU NA WEWE UTAKOSA -
Wadau tukumbuke hali ya maisha huweza kubadilika wakati wowote.
Leo waweza kuwa tajiri lakini kesho ukawa masikini.Endapo unaamini hayo yanaweza tokea wakati wowote, basi huna budi kumuheshimu yule asiye nacho,au aliye na kidogo kuliko wewe kwasababu wakati wowote unaweza ukawa katika hali aliyonayo mwenzako
(Picha maeneo fulani Kariakoo Dar)

MJUE MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI

Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali ya Tanzania mhe.George Masaju akila kiapo katika ukumbi wa Bunge hii leo baada ya Jaji Werema kujiuzulu
Spika wa Bunge mhe. Anna Makinda aiingia katika Ukumbi wa Bunge Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine alimwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Tuesday 27 January 2015

ZAMBIA YAPATA RAISI MPYA

Rais mpya wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akila kiapo kushika hatamu baada ya bnafasi ya urais kuachwa wazi kufuatia kifo cha Rais Sata.

YASEMAVYO MAGAZETI

Sunday 25 January 2015

MABADILIKO: UTEUZI WA MAWAZIRI NA MANAIBU

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu jana.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao jana, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais, Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa jana jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).

Friday 23 January 2015

ELIMU HAINA MWISHO

Bibi huyu mkazi wa Kenya kaamua kurudi shule ili kujifunza kusoma na kuandika. Hakuna kuchelewa katika kujifunza jambo jipya

Thursday 1 January 2015

KHERI YA MWAKA MPYA 2015

Napenda kuungaana na wadau wapendwa wa blog hii kumshukuru kwa kutuwezesha kuuona Mwaka Mpya 2015. Tunazidi kumwomba Mungu atuongoze kwa mwaka huu wote ili tuweze kutimiza majukumu na matarajio yetu kwa baraka zake.