Sunday 9 November 2014

WEE BODABODA, YAKWELI HAYO???

MISS TANZANIA 2014 MPYA

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzulu kwake na kumvua taji.Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam jana.

Na huyu ndiye anayechukua nafasi ya Redds Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima,aliyekuwa mshindi namba 2

DILI KWA RAIS MASKINI ZAIDI DUNIANI

Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen.
Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake ,alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu katika eneo la uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake kwa watu masikini.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen
Busqueda liliripoti kwamba ombi la gari hilo lilifanywa katika mkutano wa kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.
''Nilishangaa mara ya kwanza ,lakini nikapuuzilia mbali.Ila baadaye ombi jengine lilikuja na hivyo basi nikaanza kulichukulia kuwa swala la umuhimu'',. Alisema Mujika.

Friday 7 November 2014

KAZI NI KAZI BORA MKONO KINYWANI

Haijalishi ni kutoka wapi au rangi gani, linapofikia suala la kutafuta kipato kila mmoja ana namna zake. We kaa tu nyumbani na vyeti vyako ukisubiri uajiriwe ofisini. Wenzio wamekuja na sasa mahindi wanachoma, baadae utatafuta hata hizi kazi za kuchoma mahindi ukose.

KWA WATUMIAJI WA WHATSAPP

Whatsapp imefanya mabadiliko kidogo katika upande wa ujumbe mfupi ili kuweka mambo wazi zaidi. Kuanzia sasa:
1. Unapotuma ujumbe utaona tick moja ya kijivu kuonyesha message imeenda
2. Kisha utaona tick mbili za kijibu kuonyesha ujumbe umemfikia mlengwa
3. Baadae utaona tick mbili za Bluu kuonyesha ujumbe ulotumwa umesomwa na mlengwa.

Hii yote ni kuondoa ile kwa sijapata message yako na visingizio kama hivyo.

TAMBUA UTEUZI NA UHAMISHO WA WAKUU WA MIKOA ULOFANYA NA MH.RAIS KIKWETE HIVI KARIBUNI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.

Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014

KITENDAWILI CHA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA KINAPOKOSA MAJIBU....

Kwakweli makazi ya baadhi ya ndugu zetu hayaakisi hata kidogo msemo wa "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania"
Kivuko hiki cha MV.KILOMBERO kilikwama jana kwa takribani saa 6 huku abiria wasijue la kufanya. Katika nchi zilizoendelea na kujali sana watu kwa uwiano, tayari ungekuta kuna boti ndo za kusaidia watu hawa na mizigo. Pengine tuvute subira, wakati mwafaka bado haujawadia.
Na wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Kawanzige huko Mpanda, ndivyo wanavyosoma wakiwa wamekaa sakafuni darasani. Wewe kama mkuu wa kitengo kinachohusika na elimu unapokalia sofa unajisikiaje uonapo watoto hawa???

YASEMAVYO MAGAZETI

Tuesday 4 November 2014

ABIRIA WA DALADALA KUWENI MACHO:LISEMWALO LIPO

KWA WAPENZI WA SOKA KIMATAIFA: MECHI ZA LEO NA KESHO

MHE RAIS KIKWETE AONGEA NA WAZEE WA DODOMA

Mhe. Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia baadhi ya wazee waliokusanyika kuzungumza nao mambo mbalimbali ya kimaendeleo
Umati wa baadhi ya wazee wakimsikiliza mhe.Rais

NANI KAMA MAMA!

Mama huyu anawajibika ili familia yake iweze kupata mahitaji yake ya kila siku. Ni kazi ngumu lakini mama huyu anajituma ipasavyo. Hongereni kinamama mnaowajibika hivi. Mungu atawajalia kadiri ya jasho lenu. (Picha hii imepigwa Morogoro kwa hisani ya Mjengwa Blog)

KWAKO NI CHAKULA, KWA MWENZIO NI KITENDEA KAZI

Imefahamika kuwa, walimu wa shule moja huko Biharamulo,Kagera wanatumia mihongo kuandikia ubaoni kufuatia uhaba wa chaki katika shule hiyo. Shule hiyo ambayo ipo katika maeneo ya jamii ya wafugaji inasemekani ilianzishwa kinyemela bila kusajiliwa. Lakini tunachojiuliza, kama watu wamejitolea kuanzisha shule kwa lengo la kufuta ujinga, kwanini serikali nayo isiwaangalie na kuwasaidia pale panapopungua???

PICHA HII YAANZA KUGUSA WATU

Picha hii imekuwa mitandaoni kwa muda sasa. Amejitokeza msamaria mwema anayetaka kuwasaidia zaidi watoto hawa. Kama unajua wanakopatikana, tafadhali wasiliana na imblessd22@gmail.com

Saturday 1 November 2014

FANYA MAZINGIRA YA CHUMBANI KUVUTIA

PATA SETI HII IFUATAYO KWA TSH 67,000 TUU NI SETI YA FORONYA 4, SHUKA KUBWA , NA KAVA MOJA NZITO YA KUFUNIKIA BLANKETI NA VITU KIBAO. NI RAHISI PIGA SIMU NAMBA 0654221465 AU 0683167574

FURAHA YA MV.MAFANIKIO MKOANI MTWARA

Kwa muda mrefu wananchi wa mwambao wa Mtwara kuunganisha MsangaMkuu na Mtwara Mnjini walikuwa wakipata adha ya usafiri. Mitumbwi ndio ilokuwa yatumika kuvusha watu na mizigo.
Ila serikali imetimiza ahadi yake wa kuwaletea wananchi kivuko kipya na hivi karibuni kivuko hicho kimewasili. Furaha kwa wana Mtwara.
Ila kwa wengine sehemu nyingine za nchi usafiri wao ni huu.

VITUKO VYA TEKNOLOJIA

Wakati binadamu wanajitahidi kwenda na wakati kwa kubuni vifaa vinavyorahisisha kazi, kwa wengine bado ni tabu tupu. Ni muhimu kujitahidi kujifunza mambo mengi yanayoletwa na maendeleo ya ubunifu ila kwenda sambamba. Angalisho: " Mwelekeze namna ya kutumia vifaa hivi na sio kumcheka, sio asili yake"
Ila kikikamilika na kuletwa mezani mate yanakutoka, hujui alipata tabu kiasi gani huko jikoni.

AFRIKA: KILA KITU ASILIA

UMUHIMU WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Tunapokata miti ili kuchoma mkaa ambao husaidia katika matumizi mengi, tusisahau pia kuwa miti ni muhimu kwa mazingira yetu. Hivyo ni vizuri kujitahidi kuotesha miti sawia na ukataji miti kwa ajili ya mkaa.