Friday, 8 January 2016

PICHA RASMI YA MHE.RAIS DKT.JOHN MAGUFULI


IDARA ya Habari Maelezo imetangaza rasmi upatikanaji wa picha ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa matumizi ya maofisini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Msaidizi wa idara hiyo, Zamaradi Kawawa, alisema kila nakala ya picha hiyo bila fremu itauzwa kwa Sh 15,000 pamoja na picha ya Baba wa Taifa itauzwa Sh 5000 katika ofisi hizo.

Alisema picha ya Rauis na ile ya Baba wa Taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Tasisi za umma, Mashirika na ofisi binafsi.

“Serikali inatoa onyo kwa wale wote waliokuwa wakitundika picha ya Rais isiyo rasmi, wanatakiwa wazitoe haraka na waje katika ofisi zetu wanunue picha rasmi,” alisema Kawawa.

Aidha alisema picha hizo zitauzwa katika ofisi za Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), ambazo zimesambaa nchi nzima, hivyo watu wa mikoani watazipata katika Ofisi hizo.

Alipoulizwa kuhusu picha hiyo kucheleweshwa Kawawa alisema ilichelewa kutokana na picha iliyotolewa mwanzo kutokuwa na bora na kuwalazimu kurudia kutengeneza nyingine ambayo kimsingi inaubora wa kuridhisha.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako