Saturday 2 January 2016

MACHINJIO YA VINGUNGUTI YATATULIWA KERO ZAKE


Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais John Pombe Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.

Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.

Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.

Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.

Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.

Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.

Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.

Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.

Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.

Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.

Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako