Friday 30 September 2016

VIDEO: WAZIRI MKUU MHE KASSIM MAJALIWA AHAMIA DODOMA RASMI

CHADEMA WAHAIRISHA TENA "UKUTA"

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena.

Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani.

Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa.

UDAKU: UMUHIMU WA ELIMU

.....unaenda Sheraton Hotel unaona menu imeandikwa:
Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!
Price: TSH 22,000/=
Unaagiza!
Ukiletewa ndio unagundua kwamba: ni makande na parachichi.....😏
#hapo ndo unagundua shule sio utumwa#
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Thursday 29 September 2016

WAZIRI MKUU MHE KASSIM MAJALIWA KUHAMIA DODOMA KESHO

MHE RAIS MAGUFULI APOKEA HATI YA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI WA TANZANIA HAPA NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Sarah Catherine Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.

KULIKONI? CHAMA CHA WANANCHI CUF

Wednesday 28 September 2016

MHE RAIS MAGUFULI AZINDUA NDEGE 2 ZILIZONUNULIWA HIVI MAJUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016

Tuesday 27 September 2016

NDEGE YA PILIYA "AIR TANZANIA" ILONUNULIWA CANADA YAWASILI LEO

KWANINI TUMENUNUA BOMBARDIER?

Shirika letu la ndege lilikufa kwasababu ya kushindwa kujiendesha kutokana na gharama kubwa za uendeshaji pamoja na ufinyu wa abiria wanaotumia usafiri wa anga!

Mwanzo nilifikiri labda ni wizi unafanyika lakini baada ya kujua gharama chache za uendeshaji nikaona ni sawa kwa shirika hili kushindwa kujiendesha.

Naomba nianze na bei ya Boeing

Boeing inauzwa dola milioni mia mbili tisini na sita(US296millions) wakati Bombardier Q400 inauzwa dola milioni 35 tu(US35millions)

Kumbe badala ya kununua Boeing moja ni heri tuongezee dola milioni kumi na tisa(US19millions) tununue Bombardier tisa(Bombardier 9)

Hesabu yake:

Boeing price US296 millions
Bombardier Price US35 millions
(35×9=315)
315-296=19

Ambapo hizi Bombardier tisa zingetusaidia kwa upande wa shirika kujiendesha lenyewe na kutupatia faida kubwa kwa mara tisa kwa Taifa.

Kuhusu Speed ya Boeing ni kweli ni kubwa kuliko Bombardier kutokana na uchomaji wa mafuta, Speed yake ni 590mph wakati speed ya Bombardier ni 414mph au 667km/h

Kama kutoka Dar to Mwanza ni Km 1100 maana yake Bombardier itatumia saa moja na dakika arobaini (1 hr and 40mnts) wakati Boeing itatumia saa moja na dakika kumi na tano(1hr and 15 mnts) tofauti ni dakika 25 tu

Boeing inatumia dumu moja la mafuta la lita 4 kwa sekunde moja kwa hiyo kwa lisaa limoja inatumia lita elfu kumi na nne mia nne (14,400) (4l×60s×60m)

Kwa mfano:

Mafuta ya ndege kwa lita yakiuzwa shilingi 2000 maana yake ili tutie mafuta ya kuelekea safari ya Songea inayochukua takriban saa moja tu tunahitaji milioni 28,800,000(14,400×2000)
Na tunahitaji abiria 96 watakaolipa Tsh 300,000 ili kuweza kulipia gharama za mafuta tu.

Hapo hatujajumlisha gharama za service na wafanyakazi na wala hatujapata faida yoyote

Bombardier inatumia 1.187lita ya madumu ya mafuta kwa mile moja yaani ukikadiria inatumia lita moja ya mafuta kwa mile moja (1mile=1.6kms)
Songea to Dar Air Distance ni takribani kilometa 537=335.625miles

Kwahiyo itatumia lita 398.386875 ambazo ukizizidisha kwa gharama ya Tsh 2000 kwa lita unapata laki saba tisini na sita elfu mia saba sabini na tatu=796,773

Kiuchumi kugharamika 28,800,000 na kugharamika 797,000 bora kipi?

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na mwenye kutaka shirika hili kujiendesha kwa kibiashara ni lazima atumie Bombardier ili apate faida.

Pia kutokana na hali ya viwanja vyetu ndege hizi zinafaa kwa sababu zinaweza kutua katika viwanja vya kawaida ndio maana serikali ilizinunua ndege hizi mahususi kwa safari za ndani!

Hizi ndege Bombardier Q400 zinatumika Marekani na wanaendelea kununua Shirika la ndege la American Eagle wanazo Bombardier 35 Uingereza nao shirika la ndege la Flybe wamenunua 40.

Australian Air wamenunua 20
Ethiopia wamenunua 4 kufikisha idadi ya Bombardier 19.

Hatuwezi kutenga bajeti ya serikali iende ikahudumie shirika la ndege ambalo ukitumia akili ya kiuchumi hili shirika linaweza kujiendesha na likaliletea faida Taifa na kuliinua kiuchumi.

Hatupo kwa ajili ya kujishow off kutumia ndege za gharama kubwa na zisizo na faida ili watu watuone tuna ndege kubwa no!

Tupo kwa ajili ya kuliendeleza Taifa letu kwa faida liendelee mbele

Monday 26 September 2016

COUPLE YA WIKI HII: (USIKOSE NI KILA JUMATATU)

Diamond Platnumz na Zari (The Boss Lady)

TAMKO LA MHE:RAIS MAGUFULI BAADA YA KUTEMBELEA BANDARI YA DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Septemba, 2016 ametembelea Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kununua mashine nne za kukagulia mizigo bandarini (Scanning Mashine).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa kati ya mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo, ni mashine mbili tu ndizo zinafanya kazi na hazina uwezo wa kukagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini kupitia bandari hiyo hali inayosababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakika wa udanganyifu.

“Kwa hiyo nawaagiza TPA, na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Mbarawa na Mamlaka ya Mapato mpo hapa hakikiseni mnanunua mashine za kukagulia mizigo nne ndani ya miezi miwili, na ikifika miezi mitano muwe mmenunua mashine sita, ni lazima mizigo yote ikaguliwe kwa mashine” Amesema Rais Magufuli

Dkt. Magufuli ameiagiza (TPA) kwa kushirikiana na Wizara husika kuanza mazungumzo na kampuni ya kimataifa ya kuhudumia shehena ya makasha bandarini (TICTS) ambayo inapakia na kupakua mizigo katika gati namba nane hadi kumi na moja ili kurekebisha mkataba ambao Kampuni hiyo imeingia na Serikali kwa lengo la kuhakikisha nchi inapata manufaa yanayostahili.

Rais Magufuli aliyetembelea eneo la mita za kupimia mafuta yanayopakuliwa melini (Flow Meters) na kubaini kuwa mita hizo hazifanyi kazi, ameiagiza TPA kuharakisha mchakato wa kununua mita mpya na kuzifunga katika eneo hilo ili kudhibiti ukusanyaji wa mapato ya kodi ya mafuta.

Aidha, Dkt. Magufuli ameitaka TPA kujipanga kujenga bandari kavu (ICD) katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani ili kuachana na bandari kavu zilizoanzishwa na watu binafsi hapa Jijini Dar es Salaam na ambazo zimekuwa zikitumika kukwepa kodi.

Akizungumza na Wafanyakazi mara baada ya kumaliza kutembelea bandari, Rais Magufuli amewatoa shaka wafanyakazi hao na wafanyakazi wengine Serikalini, kuwa zoezi la kuhakiki vyeti linaloendelea nchi nzima halina lengo la kuwafukuza kazi wafanyakazi bali linafanywa kwa lengo la kukabiliana na tatizo kubwa la wafanyakazi hewa ambao wamefikia 17,500 na pia kuondoa tatizo la wafanyakazi wanaotumia vyeti vya kufoji.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Deodatus Mtesiwa ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula alikuwa Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

26 Septemba, 2016

Sunday 25 September 2016

Saturday 24 September 2016

RAIS MSTAAFU MHE JAKAYA KIKWETE APEWA TUZO

Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Tuzo ya Uongozi wa Kisiasa na Utetezi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Speak Up Afrika Bi Kate Campana, katika hafla iliyofanyika siku ya Alhamis New York Marekani. Tuzo hiyo ni kutambua jitihada na juhudi zake za kufikisha huduma za jamii hususani afya kwa kwa wanawake na watoto.

VIGOGO HALI TETE

Friday 23 September 2016

MHE RAIS MAGUFULI HAJAKATAA KUONANA NA VIONGOZI WA DINI

Tujitahidi kuwa wakweli katika utoaji habari

Na.Sheila Samba & Abushehe Nondo,Maelezo
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi hao ambao wamemuomba kukutana naye, kama inavyoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Akizungumza leo jijini, Dar es Salaam na waandishi wa habari Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum, amesema taarifa zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo na.4310 sio za kweli.

“Taarifa hizo sio za kweli, taarifa hizo zimelenga kumgombanisha Rais na Viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla na hilo halitafanikiwa,” alisema Sheikh Alhad

Aidha Viongozi hao wamesema uamuzi wao wa kumuomba Rais kuonana naye, haujatokana na kuagizwa na UKAWA, bali umetokana na maono waliyopewa na Mwenyezi Mungu.

Amefafanua kuwa Rais MAGUFULI anawaheshimu Viongozi wa dini na mara zote amekua akiwaomba wamuombee na kusema leo ni siku ya tano tangu wamuandikie barua ya kumuomba kukutana naye na wanaimani Rais atakutana na Viongozi hao.

Ameeleza kuwa Barua hiyo imeandikwa Septemba 19 na kupelekwa siku hiyo hiyo Ikulu, ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu wa Bakwata, Katibu Mkuu wa CCT na Katibu Mkuu wa TEC.

“Naomba watanzania wasisikilize maneno hayo kwasababu hayana nia njema kwa Taifa letu, naamini Mh Rais tutaonana nae na tutaongelea mustakbali wa nchi katika mambo mbalimbali,” alisistisa Sheikh Alhad

Akizungumzia utendaji wa Serikali ya Rais MAGUFULI, Sheikh ALHAD amesema Rais amerejesha nidhamu Serikalini, ukusanyaji mapato umeimarika na pia pengo kati ya wasionacho na walionacho linaanza kupungua.

Thursday 22 September 2016

UJENZI WA DARAJA JIPYA LA SALENDER JIJINI DAR KUANZA JUNI MWAKANI

Ujenzi wa Daraja la Salender litakalounganisha eneo la Coco Beach na eneo Agha Khan kupitia baharini Jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza Mwezi Juni Mwakani baada ya Serikali ya Tanzania kukamilisha mchakato wa upatikanaji wa fedha za ujenzi kutoka benki ya Exim ya Korea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 22 Septemba, 2016 muda mfupi baada ya kufanya Mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Song Geum-Young, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema ujenzi wa daraja hilo litakalokuwa na urefu wa kilometa 7 zikiwemo kilometa 1.4 zitakazopita baharini, unatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na daraja hilo litasaidia kupunguza adha ya msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

"Mchakato wa kulijenga hili daraja la Salender unaendelea vizuri kwa sababu hivi sasa kampuni ya Kikorea ambayo inafanya usanifu ipo kwenye hatua za mwisho na zabuni zinategemewa kutangazwa mwezi wa tatu Mwaka kesho na zitakwenda haraka, kwa hiyo mambo yakienda vizuri ujenzi unaweza kuanza mwezi wa sita, bahati nzuri fedha zote zipo na zimeshatolewa na Benki ya Exim ya Korea" Amesema Rais Magufuli.

CHEKA KIDOGO

Najiuliza tu lakini;
TRENI ya Mwakyembe ilivyoanza kazi siku za mwanzo, tulipanda BURE.

MABASI YA MWENDO KASI tulipanda BURE

DARAJA LA NYERERE(KIGAMBONI) tulipita BURE

Sijui na hii NDEGE MPYA YA ATCL tutasafiri BURE nijiandae?

UTOAJI ELIMU NCHINI BADO UNA CHANGAMOTO NYINGI

VIDEO:MADREVA WALIOTEKWA CONGO WAREJEA SALAMA

MHE RAIS MAGUFULI AIPONGEZA KILIMANJARO QUEENS KWA UBINGWA WA CECAFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewapongeza wachezaji wa Timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Queens) kwa kuandika historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza wa Michuano ya kugombea kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) iliyofanyika katika Mji wa Jinja nchini Uganda.


Kilimanjaro Queens imefanikiwa kutwaa Ubingwa huo baada ya kuibwaga Kenya (Harambee Starlets) kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika jana tarehe 20 Septemba, 2016.

Katika pongezi hizo alizozitoa kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, Rais Magufuli amesema Timu ya Kilimanjaro Queens imeandika historia ambayo inalipa heshima Taifa na inaamsha morali kwa wanamichezo kufanya vizuri katika mashindano.

“Mhe. Waziri Nape Nnauye naomba unifikishie pongezi nyingi kwa Wachezaji wa Kilimanjaro Queens, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walimu na Viongozi wa Timu pamoja na wadau wote waliochangia kuiandaa Timu yetu ya Taifa ya wanawake ambayo hatimaye imepata ubingwa katika michuano hii mikubwa.

“Nimefurahishwa sana na ubingwa huu na nawaomba wachezaji wa Kilimanjaro Queens na wanamichezo wengine hapa nchini kuuchukua ushindi huu kama changamoto ya kuongeza juhudi katika michezo yetu ili nchi isiishie kupata ubingwa wa Chalenji bali pia ipate ushindi katika michezo na michuano mingine mingi ambayo hushiriki” Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwaunga mkono wanamichezo na kuwatia moyo wachezaji kwa kuwa mafanikio yao yanaitangaza nchi na yana mchango mkubwa katika maendeleo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

21 Septemba, 2016

Tuesday 20 September 2016

NDEGE MPYA YA ATCL YAWASILI DAR IKITOKEA CANADA ILIKONUNULIWA


Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo.
Mwonekano wa ndani wa ndege hiyo

ALIYOYASEMA MBUNGE WA IRINGA MJINI MHE.PETER MSIGWA (MB)

Monday 19 September 2016

NDEGE MOJA KATI YA MBILI ALIZONUNUA MHE RAIS MAGUFLI KUTUA TANZANIA KESHO

Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), inatarajiwa kuingia nchini kesho ikitokea Canada.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana.

Itule alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya ReykjavΓ­k, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.

“Ndege ya pili inatarajiwa kukabidhiwa Septemba 22 na kuanza safari ya kuja Tanzania Septemba 23,’’ alibainisha.

DIAMOND PLATNUMZ AJA KI-BUKOBA NA WIMBO "SALOME"


Staa wa muziki nchini, Diamond Platnumz ameachia Wimbo ambao amemshirikisha msanii mwenzake ambaye yupo katika lebo yake ya WCB Wasafi, Rayvanny ambayo ameipa jina la Salome. Video ameshoot, Nicorux kutoka Afrika Kusini Aprili, 10 mwaka huu

Sunday 18 September 2016

Saturday 17 September 2016

MHE RAIS MAGUFULI AUSHUKURU UJIRANI MWEMA WA KENYA NA UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tetemeko hilo limetokea Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Kigoma.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na shs 437 milioni kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali

JE, WALIJUA JIWE LA MBUJI LILILOKO HUKO MBINGA-RUVUMA?

JIWE la Mbuji lililopo wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, ni miongoni mwa vivutio adimu na vya kipekee vilivyopo katika Bonde la Ziwa Nyasa ambalo linajumuisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Njombe.

Tayari Wizara ya Maliasili na Utalii imeliingiza Jiwe la Mbuji kwenye orodha ya vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Ruvuma ili hatimaye kazi ya kutangaza eneo hilo na vivutio vingine, iweze kufanyika kwa tija.

Neno Mbuji lina maana ya Kitu Kikubwa. Hivyo pengine, jiwe hilo kuitwa Mbuji, ilitokana na ukubwa wake usiokuwa wa kawaida. Jiwe hili lipo katika Kijiji cha Mbuji, Kata ya Mbuji. Kwa sasa limekuwa kivutio kwa wageni wa ndani na nje wanafika kutembelea wilaya ya Mbiga kwa shughuli zao mbalimbali, zikiwemo za kitalii.

Moja ya maajabu ya jiwe hili, ni ukubwa wake likilinganishwa na mawe yote yanayopatikana katika mkoa wa Ruvuma. Chini ya jiwe hili kuna vyanzo vingi vya maji. Ni vigumu kwa mtu yeyote kulipanda bila kwanza kuwaona wazee wa kimila wa eneo hili. Yeyote anayethubutu kulipanda bila kuwaona wazee hao, yanayomkuta anajua mwenyewe, lakini ukweli ni kwamba ni tayari juu yake. Ni vigumu kulizunguka jiwe hilo bila kufuata mila na desturi za Kabila la Wamatengo wanaoishi eneo hilo.

Kwa jamii ya Wamatengo, jiwe hili linaheshimika sana. Sehemu kubwa ya wananchi wanaoishi kuzunguka eneo lilipo jiwe hili hawajawahi kulipanda wala kulisogelea katika maisha yao yote kwa hofu ya kupoteza maisha.
Sixmund Ndunguru (90), ni mmoja wa wazee wa kimila wa Kabila la Wamatengo. Katika mazungumzo yake na FikraPevu anasema pamoja na mambo mengine kwamba ili kuweza kupanda jiwe hili, ni lazima mtu awe na mzee wa kimila wa kumwongoza, anayezifahamu vizuri mila na tamaduni za kabila hilo.

“Ninayafahamu maajabu ya jiwe la Mbuji tangu nikiwa na umri mdogo. Mandhari ya jiwe hili hayajabadilika wala kuharibiwa tangu nilipoanza kulifahamu,” Mzee Ndunguru anaanza masimulizi yake juu ya jiwe hili.

Anaendelea: “Mimea hii aina ya matete inayozunguka jiwe hili imekuwepo miaka mingi sana. Kwa mara ya kwanza, mimi mwenyewe nilipanda juu ya jiwe hili miaka ya 1940 nikiwa na baba yangu mzazi…kwa hiyo, mtu yeyote anaruhusiwa kupanda jiwe hili ilimradi azingatie maelekezo ya wazee wa kimila.”

Kwa kawaida, Wamatengo wanaamini kwamba katika jiwe hili lina viumbe vinavyoitwa Ibuuta ambavyo ni mfano wa binadamu. Viumbe hivyo vinaelezwa kuwa vifupi mno na vya ajabu. Inadaiwa kwamba wakati mwingine inapofika usiku viumbe hivyo huweza kuonekana. Hata hivyo, inaelezwa kwamba viumbe hivyo vifupi vinapatikana pia katika mataifa kadhaa duniani, lakini vikifahamika kwa majina tofauti.

BAADA YA KUPATWA KWA JUA, LEO NI KUPATWA KWA MWEZI

Thursday 15 September 2016

HUKUMU YA KESI YA ZOMBE NA WENZAKE

Mahakama ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, baada ya kumtia hatiani kwa kosa ka mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.

Wakati Bageni akihukumiwa kitanzi, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na maafisa wengine wawili wa Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa huru, baada ya mahakama kuwaona kuwa hawana hatia.

Bageni amehukumiwa adhabu hiyo leo baada ya mahakama ya Rufani kukubaliana na rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwaachia huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara hao.

Wafanyabiashara hao, Savings Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa Manzese, Juma Ndugu, waliuawa Januari 14,2006, kwa kupigwa risasi Mbezi Luis, Dar.

WAASI WA MAI MAI WATEKA MADREVA WA MALORI WA TZ NA KENYA

Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo nchini Tanzania (TATOA) kinaripoti kwamba, waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wamewateka nyara madereva wa Tanzania na kuchoma baadhi ya magari ya mizigo. Waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. Pia waasi hao wametoa siku ya mwisho (deadline) ya majeshi yanayolinda amani nchini humo kuondoka.

TATOA inasema imezungumza na mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics, Mzee Azim Dewji ambaye amethibitisha taarifa hizi na pia balozi wa Tanzania DRC pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje tayari serikali inashughulikia suala hili. Jumla ya magariyaliyotekwa ni 12 kati ya hayo magari 8 ya Tanzania na 4 ya Kenya. Magari 4 ya Tanzania yamechomwa moto na madereva wote walichukuliwa na waasi lakini bahati nzuri madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kuwatoroka. Tukio hilo limetokea sehemu inaitwa Kasebebena na Matete, wastani wa kilomita 30 kutoka mji wa Namoya.

TATOA inawashauri wanachama waliopakia mzigo kuelekea huko kuwasiliana na madereva wao ili wasitishe safari, kusubiri taarifa ya hali ya usalama kutolewa.

Mai Mai Kata ni kundi la waasi nchini DRC ambalo linadai kupigania uhuru wa jimbo la Katanga, na linaongozwa na GΓ©dΓ©on Kyungu Mutanga, ambaye aliunda kundi hilo mara tu alipotoroka kutoka gerezani mwaka 2011.

GAVANA: SABABU ZA FEDHA KUHADIMIKA MTAANI

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.

“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.

“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.

Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.

Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.

Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

BUSARA ZA BABA KWA BINTIYE

Msichana alinunua simu smartphone ambayo ni ghali mno. Baba yake alipoiona alimuuliza "Binti yangu uliponunua hiyo simu yako ya gharama cha kwanza kufanya kilikua ni nini?"

"Niliweka screen protector kuzuia michubuko ya kioo na nikanunua cover kwa ajili ya kuzuia ikianguka isichubuke" binti alijibu.

"kuna mtu alikusukuma kufanya hivyo?" baba alimuuliza bintie

"Hapana" binti alijibu

"Unafikiri huko si kuwatukana waliotengeneza simu kwamba hawakukamilisha kazi yao? Baba aliendelea kuuliza.

"Hapana baba" ni kwamba hata wanaotengeneza wanawakumbusha watu kuweka cover katika simu zao kuzuia kuharibika kwa urahisi"

"Je uliiwekea cover kwa vile simu ni bei rahisi na inamuonekano mbaya?" Baba aliendelea kusaili

"ukweli nimeiwekea cover sitaki iharibike mapema na ipoteze uthamani wake" binti aliendelea kumjibu baba yake.

"ulipoiwekea cover, imepunguza uzuri wa simu yako?"

"Hapana baba nafikiri ndio imeonekana nzuri zaidi tofauti na mwanzo, na imeipa simu yangu ulinzi ili isiharibike"

Baba akamwangalia binti yake kwa upendo na akamwambia, " Je kama nikikuomba ukave mwili wako ambao unathamani kubwa kuliko hata hiyo simu yako kwa nguo ndefu zisizo onyesha maungo yako kwa watu hovyo hovyo utafanya hivyo?"

Binti alibaki kimya!

Niambie! Wanaume waone maungo yenu wagundue nin?

Kwa unyenyekevu naomba niwe mkweli binti yangu, uvaaji wa nguo fupi na zisizo na staha ambazo zinaweka wazi maungo yenu obvious zinapunguza thamani yenu na heshima kwa jamii.

Watakaokutamani ni wanaume wakware tu wale wahuni wahuni! Ila mwanaume mwenye heshima zake hawezi akavutiwa nawe kwake atakuona kama msichana fulani wa kileo unayefaa kwa usiku mmoja tu na sio kwa maisha.

Cover your smartphone, cover your precious body for your husband only!