Friday 8 January 2016

MMBWANA SAMATTA MCHEZAJI BORA ANAYECHEZEA AFRIKA

Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika, wakati tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja nchini Nigeria. Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.

Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye amempongeza mchezaji wa mpira wa miguu wa Taifa Star Mbwana Samatta baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka Afrika 2016 kwa wachezaji wanaocheza soka Barani Afrika.iliyotolewa nchini Nigeria.
Nnauye ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na watumishi wa Wizara wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo leo jijini Dar es salaam.
Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.
Nnauye amewataka wachezaji wengine kufuata nyayo za mchezaji huyo kwa kuongeza juhudi, nidhamu katika michezo na watambue kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.
Akifafanua zaidi Nnauye alibainisha kuwa kilichomfikisha Samatta hapo ni kujitambua na kujituma katika ajira yake.
Samatta ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Barani Afrika kwa kupata alama 127 dhidi ya Robert Kidiaba aliyepata alama 88 na Baghdad Bounedjah alama 63.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako