Friday 31 July 2009

MKOMBOZI WA KINAMAMA



Hatimaye Benki ya Wanawake nchini imefungua milango yake rasmi leo yapata saa 2:30 asubuhi, na kama uonavyo pichani wateja si wanawake tu bali na kinababa pia. Hii ipo mtaa wa Mkwepu.Hii inakuja huku kukiwa na wimbi la wizi wa mamilioni ya watu yaliyohifadhiwa benki (Rejea NMB Temeke)

MAMILIONI YAKOMBWA NMB TEMEKE

Hii sasa kazi maana tunatafuta kwa jasho na kula nako kwa wizi wizi.Maisha bora haya jamani sijui yatatufikisha wapi?Askari wakiweka doria sehemu ya tukio
Majambazi yaliyo na Silaha na mabomu ya kurusha kwa mkono leo asubuhi majina ya saa 5:20 walivamia Benki ya NMB tawi la Temeke na kupora kiasi kikubwa cha fedha. Pia yaliua mlinzi mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi na kujeruhi wengine 13 wakiwamo askari Polisi wawili.

MISS TEMEKE 2009

Wote wanaonekana kuwa na vigezo, tumchague nani? Majaji kazi kwenu.

Thursday 30 July 2009

KUNA KAUWIANO FULANI KAMBALI

jiji la Larnaka
Jiji la Dar-es-salaam

JAMANI MAISHA HAYA!

Kweli maisha Bongo yanagonga si utani. Ni mchana wa jua kali, mzee huyu ameamua kujilaza hapa.Pengine ni kwasababu ya uchovu wa kazi, pengine ni njaa, pegine ni kukosa sehemu ya kupumzika. Haya yote yanatokea nyumbani Tanzania huku msisitizo ukiwa ule ule wa kuwapatia raia "Maisha bora", lakini kama hali ndio hii tunajiuliza "maisha bora kwa kila mtanzania" yapi?

Wednesday 29 July 2009

JIJI LA MWANZA LAZIDI KUPENDEZA

Mandhari ya jiji la Mwanza inazidi kupendeza hasa baada ya mwanza kuwa Jiji. Ni eneo lililokaa sehemu nzuri ukingoni mwa Ziwa Victoria na hivyo kuipa Mwanza mandhari murua ya kubarizi na maisha kwa ujumla. Tuzidi kuboresha na kutunza mazingira hayo.

MAMBO HUANZA HIVI


Ajali nyingi huanza hivi

Monday 27 July 2009

AJALI TENA



Zaidi ya watu 28 wamepoteza maisha
Kwa bahati mbaya wiki inaanza kwa taarifa kuwa kuna ajali mbaya imetokea usiku huu huko Korogwe na kuhusisha basi la abiria la Mohamed Trans na Lori lamizigo. Inahofiwa takriban watu 20 wamepoteza maisha. Bado blog yako inafuatilia na itakuletea nyepesinyepesi mara zikipatikana. Poleni jamani.

Sunday 26 July 2009

NAWATAKIA WIKI NJEMA WADAU

Huu ni kama mlango wa kwenda kusaka maisha ndani ya jiji la Dar.Mtelemko kuelekea Ubungo Maji

MWEUSI WA KWANZA KUWA MISS ENGLAND 2009

Her ambition is to follow in her uncle's speedy footsteps and win Olympic gold.
For Rachel Christie, that dream is still at least three years away. In the meantime, however, the 20- year-old niece of Linford Christie has just won another title – becoming the first ever black Miss England.
The professional track and field athlete swapped her running gear for high heels and a glamorous dress to win the contest on Monday night.
It means 5ft 10in Miss Christie will have to juggle her training schedule again as she prepares to face another hurdle – a bid for the Miss World crown in South Africa later this year.

USISHANGAE NI "WIVU WA MAPENZI" HUU

JUMAPILI NJEMA

Nawatakieni wadau Jumapili njema na mapumziko mema ya mwisho wa wiki.Msisahau kesho kuwahi tena kazini kusukuma gurudumu la maisha

MKUTANO MAALUM WA CCM READING

WANACCM NA WATANZANIA TOKA MIJI MBALIMBALI WAANZA KUWASILI READING KWA AJILI YA MKUTANO WA CCM - UK, UTAOFANYIKA JUMAPILI LEO TAREHE 26/07/2009, THE WAREHOUSE, READING, RG1 3LB.NYOTEMNAKARIBISHWA
www.ccmlondonuk.org
Susan Mzee
KATIBU CCM TAWI-UK

Wednesday 22 July 2009

KUHADIMIKA KWA "KARIBU NYUMBANI"

Kumradhi wapendwa sana wadau wa Blog hii kwa kutokuweza kuwaletea habari kwa wiki moja hivi. Natambua mchango wenu na nasikitika kwa kuwaacha gizani kwa muda. Nimerudi tena na karibuni sana wadau.

Tuesday 14 July 2009

UJUMBE WA LEO

TUFUNGUE MACHO AU?

Badala ya kukaa na kujilaumu kwamba maisha magumu, pengine tunaweza kufanya ubunifu kama huu wa hawa wenzetu. Lakini kuna maswali mengi; gari hili litapita wapi na barabara zetu hizi?, na hayo mabehewa vipi? Ni changamoto tu ya nini kifanyike kuboresha maisha yetu.

TUTATOKA LINI HUKU?

UFUGAJI WA KUIGWA

Pichani ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda(Kushoto)akiwaonyesha sungura watoto wa Kijiji cha Matumaini cha Dodoma kinacholea watoto yatima ambao aliwaalika nyumbani kwake Mjini Dodoma,Julai 12, 2009
Picha na maelezo kwa hisani ya Haki Ngowi

Monday 13 July 2009

WIKI YAANZA NA ADHA YA USAFIRI

Hapa ni katika kituo kidogo cha Bom Bom Kiwalani. Bado tatizo la usafiri lipo na hivyo kupelekea wat kugombania magari kwa vurugu sana. Hapa uhandsome na ubishoo pembeni.Pamoja na hayo yote NAWATAKIENI WADAU WIKI NJEMA YENYE MAFANIKIO

Sunday 12 July 2009

IRENE UWOYA SASA MKE WA MTU

Tangu jana Irene Uwoya amechukuliwa jumla na kihalali na Mchezaji maarufu wa kimataifa Bw.Ndikumana.(Pichani)Mr. & Mrs Ndikumana wakivishana pete za ndoa katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar-es-salaam jana, Picha zaidi baadae kwa ruhusa ya wandoa hao
Hakuna cha Benzi wala Limmousinne, usafiri simple tu
Mwendo kwa Ngamia, mke mbele, bwana nyuma juu ya ngamia.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

BEI YA NYAMA YAPANDA

Athumani Shabani ambaye ni mfanyabiashara ya nyama katika soko la Buguruni akikata nyama kwa ajili ya kumhudumia mteja wake. Hivi sasa vyama imepanda bei kiasi cha kuwafanya walaji kushindwa kumudu, kilo moja ya ni 3800 hadi 4000. Athumani amelalamikia mamlaka husika kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei.

"Sasa kama bei ya nyama imepanda na mie nilivyo kibonge hivi si ndo nitakwisha kabisa,maana ukibonge wangu wategemea sana nyama hasa 'beef'"

AMANI MUHIMU

Katika mazingira anayoishi mtoto huyu amani imetoweka. Ni mtoto mdogo sana lakini analazimika kushika mtutu wa bunduki kujilinda au kutetea amani. Si sahihi, viongozi wanapaswa kuwa makini kwa hili maana halitoi mwelekeo mzuri
Tanzania tunajivunia kuwa na amani. Hii ni tunu ambayo tunatakiwa kuilinda. Watoto hawa japo mazingira yaonekana kama ya tabu kidogo lakini wana amani. Tuiendeleze amani iliyopo.
Niitazamapo picha hii pia napata ujumbe kuwa wapo katika mazingira yenye amani ndio maana wapo katika hali hiyo, lakini pia ni muhimu Kujiuliza;hapo wameenda kufanya nini? na je wanakifuatilia? Sidhani kama kwa namna hii tunaweza kuendeleza Amani tuliyonayo maana haioneshi kama kuna ushirikiano katika kujadili au kufuatilia yanayotukabili katika kuimarisha maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha amani.CHANGAMOTO!!!

JUMAPILI NJEMA WADAU

Ni bora hata ungeenda kanisani kuliko kucheza na Beberu, Wewe sio mbuzi,inakuwaje wataka kupigana nae vichwa, akikupasua hicho kichwa je?

Wapendanao haooooooooooo, nao waelekea Kanisani wewe je?

Au jana ilikuwa hivi nini?

RAIS BARAKA OBAMA NCHINI GHANA

Rais Obama na Familia yake wakishuka toka kwenye ndege yao AIR FORCE ONE katika siku ya kwanza ya ziara yake Kusini mwa jangwa la Sahara nchini Ghana jana.Akibadilishana mawili matatu na Rais wa Ghana

Akihutubia Wabunge na waalikwa katika Ukumbi wa Bunge Ghana

Saturday 11 July 2009

Mhe. RAIS OBAMA AMPONGEZA JK

JK akiwa katika mazungumzo White House jijini Washington DC na Rais wa
Marekani Barack Obama na Secretary of the State Hillary Clinton Mei 20 mwaka huu


Rais Barack Obama wa Marekani amemsifia Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, akimwelezea kama kiongozi wa mfano ambaye amefanya kazi nzuri ya kupeleka huduma za waziwazi kwa wananchi wake.

Rais Obama amesema kuwa Rais Kikwete ni mmoja wa viongozi wa Afrika walioonyesha uongozi thabiti ambao uko tayari kusonga mbele katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Rais Obama amemwaga sifa hizo kwa Rais Kikwete katika mahojiano na taasisi ya mawasiliano kwa njia ya inteneti ya AllAfrica.Com wakati akijiandaa kufanya ziara yake ya kwanza katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara, kwa kutembelea Ghana.

Rais Obama aliwasili Ghana usiku wa kuamkia leo (Ijumaa, Julai 10, 2009) kuanza ziara ya siku mbili ya kwanza katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Rais Obama anatarajiwa kuondoka Ghana leo kurejea kwao Marekani.

Kabla ya kutembelea Ghana, Rais Obama tayari alikwishakutembelea Bara la Afrika kwa kuzuru nchi ya Misri, iliyoko Afrika Kaskazini katika wiki za karibuni.

Rais Obama ambaye aliwasili Ghana akitokea katika Mkutano wa Nchi Zenye Viwanda Vingi Zaidi Duniani wa G8 nchini Italia, aliiambia taasisi ya AllAfrica.Com katika mahojiano yaliyofanyika Ikulu ya Marekani kabla ya kuondoka kuelekea Russia, Italia na Ghana:

“Lazima kukumbuka kuwa pamoja na kwamba nitaitembelea Ghana kwa ziara hii, tayari nimemkaribisha Tsvangirai wa Zimbabwe katika Ofisi ya Rais wa Marekani. Tulikuwa na Rais Kikwete wa Tanzania kabla ya hapo katika Ofisi hii hii, na katika kila mkutano najaribu kuelezea ujumbe huo huo.”

Aliongeza Rais Obama: “Tumeona kazi nzuri sana inayofanywa na uongozi katika Tanzania ukielekeza nguvu zake katika kutoa huduma za wazi wazi na dhahiri kwa wananchi wake, na kila mahali ambako watu wanataka kujisaidia, na sisi tunataka kuwapo kama washirika wa uongozi.”

Rais Obama alimwalika Rais Kikwete kuwa kiongozi wa kwanza kabisa wa Bara la Afrika kukutana naye katika Ofisi ya Rais wa Marekani tokea kuapishwa kuwa kiongozi wa Marekani Januari 20, mwaka huu.

Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Obama katika Ikulu ya Marekani mwezi Mei mwaka huu, 2009.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa Bara la Afrika na uongozi wa Rais Kikwete na Afrika kwa jumla, Rais Obama alisema: “Nadhani Bara lote ni muhimu. Na nadhani kuwa tunao uongozi imara katika Bara la Afrika ambao uko tayari kusonga mbele na tunataka kusonga mbele nao.”

Rais Obama pia alisisitiza kuwa Afrika inahitaji kuendelea na juhudi zake za kuimarisha utawala bora, ili kuzidi kuvutia uwekezaji kutoka Marekani.

“Jambo la kwanza ni kwamba itakuwa vigumu kuvutia uwekezaji kutoka nje bila kuwako na utawala bora. Uwekezaji wa namna inayoboresha maisha ya kila siku ya wananchi wa Afrika. Kama maofisa wa Serikali wanataka binafsi kulipwa asilimia 10, ama 15, ama 25 juu ya kiasi cha uwekezaji, hakuna mwekezaji ambaye atakwenda kuwekeza kule. Hilo ni jambo la kwanza.”

Aliongeza kiongozi huyo: “Jambo la pili, nadhani wakati baba yangu aliposafiri kutoka Kenya kuja Marekani na akarudi nyumbani kwenye miaka ya 1960, pato la taifa la Kenya na Korea Kusini lilikuwa sawa...kwa hakika la Kenya lilikuwa kubwa zaidi. Nini sasa kimetokea katika miaka 50 tokea wakati huo hadi sasa?”

Alisisitiza: “Tulichoshuhudia ni Korea kuchanganya uwekezaji kutoka nje, kujishikamanisha na uchumi wa dunia pamoja na mkakati mkali wa aina ya viwanda ambavyo vililenga katika kuzalisha kwa ajili ya kuuza nje, msisitiko mkubwa kwenye elimu ya nguvukazi yenye ujuzi, ikisisitiza kuwa uwekezaji wa nje unakwenda sambamba na upatikanaji wa teknolojia, ili kuweza kuvijenga na kuviendeleza viwanda vya ndani.”

Rais Obama amesema kuwa kwa maana hiyo Afrika inayo mifano ya kuiga. “Hivyo, tunayo mifano. Tunajua kiasi cha kazi na nguvu na juhudi kinachotakiwa. Jambo ambalo hatujaliona ni matumizi endelevu, yasiyoyumba ya mifano hiyo katika Afrika kwa miaka yote hii, na nadhani wakati sasa umefika wa kuanza.”

Ziara ya Rais Obama inafuatia ile nyingine ya kiongozi aliyemtagulia wa Marekani, Rais George W Bush iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka jana, akitembelea nchi nne za Afrika, na kukaa muda mrefu zaidi, siku nne, katika Tanzania akiwa mgeni wa Rais Kikwete.

WADAU WEEKEND IMESHAFIKA, WAPI SASA? AU NI ...........


Picha hii inanikumbusha sana "enzi za Mwalimu" ambapo wadau wa wakati ule walikuwa wakijimwagamwaga sehemu hizo maarufu. "Mwafrika Bar" ilikuwepo kila eneo la nchi. Siku hizi mmmmm utaambiwa twaenda "Mango Garden, Coco Beach, Msasani Club, Friends Corner tukawaone Twanga Pepeta n.k. Zile Mwafrika Bar na kina Masantula wao ziko wapi tena?

WAPI NA WAPI AU NDO KUBADILISHANA ?

Binadamu
Sokwe

JK AFUNGUA HOTELI YA KITALII

JK na mmiliki wa hoteli ya kitalii ya Bilila Lodge Kempinski Bw. Ali Al Bwardy wakifungua kitambaa kuashiria kuzinduliwa kwa hotelui hiyo jana asubuhi. Hoteli hiyo ya nyota tano ina vyumba 80
Mandhari ya hoteli mpya ya kitalii ya Bilila Lodge Kempinski iliyofunguliwa na JK katika mbuga ya Serengeti leo asubuhi

BAISKELI ZETU

Watoto wa nyumbani wakiwa tayari kuikabili miteremko Iringa

Watoto wakijiandaa kwa mashindano ya baiskeli Canada

Baba na wana Srilanka/Thailand/India

Baba na mwana Ujerumani

Mama na mwana Uholanzi