Monday 27 April 2015

TETEMEKO LA ARDHI HUKO NEPAL LAUA ZAIDI YA 4,000

watu wanaokadiriwa 4,000wamefariki dunia kufuatia tetemeko la ardhi huko nchini Nepal.Maeneno mbalimbali ya Makumbusho katika Mji wa Kathmandu yameharibiwa kabisa

SHEREHE ZA MUUNGANO ZAFANA

Rais Jakaya Kikwete hapojana aliongoza sherehe za miaka 51 ya Muungano waTanganyika na Zanzibar. Hii nisherehe yake ya mwisho kama rais wa Tanzania maana baada ya Uchaguzi wa Oktoba tutakuwa na Raismwingine. Rais Kikwete alitumia muda huokuwaaga wananchi

Friday 24 April 2015

JIJI LA DAR ES SALAAM LAZIDI KUCHANUA


Taswira kutokea maeneo ya Posta Dar
Mawasiliano Tower pembeni ya Mandela Road (Ubungo/Mwenge)
Twin Towers (Magorofa Pacha) ya Benki Kuu ya Tanzania
Jengo la Kuongoza Meli lililopo maeneo ya Ferry Dar
Uhuru Heights karibu na Hotel ya Movenpick-Dar
Kuanzia maeneo ya Posta hadi Kigamboni

Thursday 23 April 2015

KUSINI MWA TANZANIA KUANZA KUNEEMEKA NA MIRADI YA DANGOTE


Msafara kutoka kijiji cha Mgao atakako jenga Bandari
Ndege ya Alhaji Dangote katika Uwanja wa Ndege Mtwara baada ya kutua alipokuwa naenda kutembelea eneo la fukwe atakakojenga Bandari.
Kiwanda cha Saruji cha Dangote kinachoendelea kujengwa

Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MKUU WA WILAYA WA KINONDONI AONYESHA KUTHAMINI VIPAJI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Makonda na Kampeni ya vipaji inaitwa "Kipaji chako Ajira yako" fomu za kushiriki kwa Vijana zimeshaanza kutolewa kwenye ofisi za Kata za Serikali ya mitaa za Wilaya ya Kinondoni

Wednesday 22 April 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU: MNAOWANIA UONGOZI JIANDAENI KUTULETEA UWIANO WA HUDUMA MUHIMU NA MAENDELEO ZAIDI

1. MICHEZO YA WATOTO
Watoto wanahitaji maeneo ya kuchezea. Sehemu nyingi zilizokuwa wazi zimetengwa kwa ajili hiyo zimeingilia na kutumika vinginevyo.
Wakati hao wa mazingira magumu wanacheza peku kwenye mawe, wengine waliojaaliwa wanafurahia mazingira mazuri.
2. USAFIRI
Hili nimekuwa tatizo kila kukicha. Mfano kwa Jiji la Dar, msongamano wa magari na usafiri kutokidhi kunawapa watu wengi adha. Hali hii imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo sana.
Lakini hatuachi kushukuru kwa juhudi za serikali kuboresha hili.
3. MAKAZI
Bado wananchi wengi wanaishi katika mazingira magumu kimakazi. Tunaomba hili litupiwe macho
Hata hivyo juhudi za serikali na watu binafsi kuboresha maisha zinaonekana. Ni bidii iongezwe tu
4. MAJI
Wananchi wanateseka kwa adha hii
Hata hivyo juhudi katika baadhi ya maeneo zimefanyika na wananchi wanapata maji safi na salama. Ila sio wote. Tanzania ilivyojaliwa mito na maziwa inawezekana tatizo la maji likawa historia

UKITAKA KUITWA "BABY" JIANDAE KWA HAYA

WAALIMU KWA ADHABU HIZI MNATUULIA WATOTO

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui wilayani Kiteto, amefariki dunia darasani baada ya kudaiwa kuchapwa viboko na walimu watatu wa shule hiyo, kwa kile kilichodaiwa kufeli mtihani wa Kiswahili.

Polisi wilayani na mkoani Manyara, wanamshikilia mwalimu mmoja baada ya wenzake kukimbia baada ya tukio.

Akizungumza jana, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samwel Nzoka alimtaja mwanafunzi huyo aliyepoteza maisha kuwa ni Noel Bichima (15).

Kanali Nzoka alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi wakiwa darasani, wakati mwalimu huyo anayeshikiliwa na polisi alipokuwa akiwafundisha. Inadaiwa mwanafunzi huyo alichapwa viboko vinane. Haikuelezwa kama alichapwa kiganjani ama sehemu nyingine.

Nzoka alidai kuwa mwalimu huyo alimchapa marehemu baada ya kupata alama 40 katika mtihani wa somo la Kiswahili kwani walipeana mkakati wa kutofeli na kwamba mwanafunzi atakayepata chini ya alama 40 atachapwa fimbo 12.

WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU: MECHI ZA LEO JTANO

WATAMBUE WATUHUMIWA SUGU WA KUPORA WAGENI NA WANAWAKE MIKOBA/POCHI

Watuhumiwa wanne wamekamatwa jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena baada ya kumpora raia wa kigeni wakiwa na gari dogo rangi ya kijivu yenye nambari za usajili T787 DBU Toyota Cienta.

Hivi karibuni kumeibuka wimbi la wahalifu kuwapora pesa na vitu vya thamani kama mikufu, bangili, hereni pia pete na vitu mbalimbali vya thamani raia wa kigeni na akina mama ambao hupenda kutembea na pochi. Wahalifu hawa hutumia gari dogo ambalo mara kwa mara hubadilishwa namba zake za usajili na wakati mwingine gari hili wanalitumia kama Tax bubu.

Leo tarehe 21/04/2015 majira ya saa 09:00 asubuhi katika eneo la Posta Mpya watuhumiwa hawa walimdangavya bwana CEES S/O JAN CONIJN, Miaka 27, raia wa Uholanzi aliyetaka kufika Klabu ya Leaders kwamba wangempeleka eneo hilo kwa kutumia gari tajwa hapo juu. Baada ya kuondoka na dereva kila baada ya mita 200 dereva huyo alikuwa anasimamisha gari na kuongeza mtu mwingine kama abiria hadi walipotimia wote wane.

Walimpeleka hadi maeneo ya Kinondoni kwa Manyanya na walipofika eneo hilo walimweleza wazi kuwa wao ni wahalifu na walimtaka awapatie pesa vinginevyo wangemuua. Aliwapatia pesa zote alizokuwa nazo Tshs 75,000/= lakini hawakuridhika ndipo walipomtaka awapatie kadi ya benki (ATM CARD) na nambari za siri (Pass Word).

Baada ya tukio hilo wakamtupa karibu na Hospitali ya Mwananyamala na wao wakageuza gari kurudi katikati ya mji. Wakati tukio hilo linatokea raia wema walishuhudia na kutoa taarifa kwa Polisi. Polisi walifuatilia haraka na kuweka mtego uliowanasa watuhumiwa wote katika eneo la makutano ya barabara ya Bibi Titi na Ohio karibu na Hotel ya Serena.

Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni:

1. SALUM S/O SAID MTUMWA @ MARO, Miaka 25, Mkazi wa Chang’ombe Bora.
2. ALEX S/O INNOCENT MANGUKA @ MAKA, Miaka 30, Mkazi wa Kimara Temboni.
3. MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, Miaka 27, Mkazi wa Mwananyamala.
4. STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, Miaka 32, Mkazi wa Mwananyamala.

Walipopekuliwa watuhumiwa hawa walikutwa na simu mbalimbali za mkononi zipatazo 11 ambazo zinachunguzwa kuhusiana na mbinu ya uhalifu wanaoutumia. Pia ilikamatwa ATM CARD iliyochukuliwa kwa mlalamikaji kabla watuhumiwa hao hawajaitumia. Aidha gari namba T787 DBU Toyota Cienta linashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa, wawili ambao ni MOHAMED S/O ALLY ABDALLA @ MEDY, na STEPHANO S/O ALBERT KIKINDI @ KING, tayari wanazo kesi nyingine mahakamani na wako nje kwa dhamana.

Sambamba na tukio hili oparesheni ya kuwakamata wahalifu wengine wenye mtindo huu wa kuwapora wageni au wakina mama wenye mikoba inaendelea na tunawaomba wananchi waonyeshe ushirikiano wa kutosha ili kutokomeza vitendo hivyo viovu. Aidha hakuna silaha yoyote iliyotumika au kukamatwa kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

Tuesday 21 April 2015

TRENI YA MWENDO KASI KULIKO ZOTE DUNIANI HUKO JAPAN

Treni ya Japan ya Shirika la Central Japan Railway iendayo kasi, imevunja rekodi yake duniani kwa kufikia mwendo wa kilomita 603 kwa saa, sawa na maili 374 kwa saa katika majaribio yake karibu na Mlima Fuji.
Treni hiyo imevunja rekodi yake ya mwendo wa kilomita 590 kwa saa iliyoweka wiki iliyopita katika jaribio lingine.

Monday 20 April 2015

SIFA ZA MGOMBEA URAISI KWA TIKETI YA CCM ZAAINISHWA

1. Anapaswa kuwa na uwezo wa kuliongoza Taifa kwa kuzingatia uzoefu alionaokatika uongozi wa shughuli za Serikali, umma na taasisi.
2. Awe mwadilifu, mwenye hekima na busara.
3. Awe na elimu ya kiwango cha Chuo Kikuu au inayolingana na hiyo.
4. Awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza Muungano wetu, umoja, amani na utulivu wetu pamoja na mshikamano wa kitaifa.
5. Awe mtu wa kuona mbali, asiyeyumbishwa, mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala nyeti na muhimu ya Taifa kwa wakati unaofaa.
6. Awe na upeo mkubwa usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifaili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na Dunia yote kwa jumla.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya udikteka au ufashisti bali aheshimu na kuilinda Katiba ya nchi, sheria, utawala bora, kanuni na taratibu za utawala bora.
8. Awe mtetezi wa wanyonge, kusimamia haki za binadamu, mzingatiaji makini wa maendeleo ya raia wote na asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wake binafsi.
9. Awe mstari wa mbele kuzifahamu, kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza Sera za CCM na Ilani ya CCM ya Uchaguzi.
10. Awe mpenda haki na jasiri wa kupambana na dhuluma,maovu yote nchini.
11. Asitumie nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali.
12. Awe ni mtu anayekubalika na wananchi.
13. Awe makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa uongozi, watendaji, asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu ili kuinua nidhamu ya kazi, tija na ufanisi.

WATEJA WA TIGO PESA KUFAIDIKA NA MGAO WA BILIONI 3.3

Tigo Tanzania imetangaza mgao mwingine wa malipo kutoka kwenye mfuko wa fedha wa Tigo Pesa wenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 (US $ 1.8) kwa wateja wake. Mgao huu wa fedha ndio wa kwanza katika robo wa mwaka huu.

Malipo haya ni ongezeko la asilimia 6 ukilinganisha na mgao uliopita wa bilioni 3.1 uliotolewa katika robo ya mwaka iliyopita 2014. Ongezeko hili linaashiria ukuaji wa umaarufu wa huduma hii pamoja na ongezeko la idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa, kwa mujibu wa maelezo ya Kaimu Meneja Mkuu, Cecile Tiano.

“Tunayofuraha kubwa sana tena kutangaza ugawaji wa faida hii kwa watumiaji wetu wa Tigo Pesa. Malipo haya yanadhihirisha moyo wetu wa kushiriki katika kuboresha hali za maisha wateja wetu pamoja na nchi zima kwa ujumla,” alisema Tiano.

Alisema kwamba malipo haya ya robo mwaka yatalipwa kwa watumiaji wote wa huduma ya Tigo Pesa ikiwemo mawakala wakuu, mawakala wa reja reja na mteja mmoja mmoja.

“Tunaamini ya kwamba faida hii ya robo ya kwanza ya mwaka 2015 itatoa nafuu ya kifedha kwa mamilioni ya wateja wa Tigo kutokana na mahitaji na matumizi yao waliyonayo,” alisema.

Meneja Mkuu alielezea, kama ilivyokuwa awali ya kwamba wastani ya kiwango amabacho mteja atajipatia itatokana na kiwango ambacho atakuwa alikuwa anakihifadhi katika akaunti yake ya Tigo Pesa.

Tigo Pesa ilikuwa huduma ya kwanza ya kifedha ya simu ya mkononi duniani kulipa mgao wa faida kwa wateja wake pale mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ulipozinduliwa kutoa migao yake ya fedha rasmi mwezi Julai 2014. Mgao unaofuata war obo mwaka wa fedha wa mwezi Aprili mpaka Juni 2015 utalipwa mwezi Julai mwaka huu, kutoka na maelezo ya Meneja Mkuu.

Mgao wa faida kutoka mfuko wa fedha wa Tigo Pesa inaenda sambamba na tangazo la Benki Kuu lilitolewa mwezi Februari 2014. Mpaka sasa kampuni imekwisha lipa kiasi cha shilingi bilioni 23.9 kwa watumiaji wa Tigo Pesa katika migao minne tofauti ya robo mwaka tangu kuzinduliwa kwa huduma hii Julai 2014.

WAZIRI MEMBE: HAKUNA MTANZANIA ALIYEFARIKI KATIKA MAPIGANO AFRIKA KUSINI

Watanzania 23 waishio Afrika Kusini wamewekwa kwenye kambi maalumu ya Isipingo nchini humo ili kupewa ulinzi wa maisha yao yaliyo hatarini kufuatia mashambulizi yanayofanywa na wazawa dhidi ya wageni.

Watu hao ambao ndiyo idadi ya Watanzania waliotambulika kuwa hatarini nchini humo, wanatarajia kuwasili nchini muda wowote baada ya Serikali ya Afrika Kusini kuridhia.

Watakaorejea nchini ni Watanzania 21, wengine wawili wameomba kuendelea kubaki huko.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema hakuna Mtanzania aliyepoteza maisha katika vurugu zilizosababishwa na chuki dhidi ya wageni, lakini wapo Watanzania watatu waliokufa nchini humo kwa sababu nyinginezo

Goodwill Zwelithini, Mfalame wa Zulu ambae inasemekana matamshi yake ndo yalopelekea mapigano haya huko Africa Kusini, japo leo kajitokeza akiwaasa wananchi hao waache fujo

MAGAZETINI

Sunday 19 April 2015

TULIKOTOKA NI MBALI

Soda zetu ambapo miaka ya 80 zilizkuwa zinauzwa kati ya sh.12 na 20 kwa chupa
Usafiri wetu ambapo kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam mnalala njiani hata siku 2 kwa baadhi ya mabasi hayo
Stempu zetu ambapo wakati huo salamu zilikuwa zatumwa kwa barua. Ukiandika barua leo ukisema naumwa inamfikia mlendwa ukiwa tayari ushapona au labda haupo tena. Tofauti na sasa mambo ya simu, whatsapp,ujumbe mfupi nk

FASTJET YAZINDUA SAFARI KILIMANJARO-ENTEBBE

Meneja Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki Mhe. Jimmy Kibati akikata keki kuashiria uzinduzi wa Safari za ndege ya Fastjet katiya Kilimanjaro (KIA) na Entebbe Uganda. Uzinduzi huu ulifanyika wiki ilopita katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe nchini Uganda. Hii ni katika kukuza huduma za anga Afrika Mashariki.

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA

Ni jumapili siku nyingine ya mapumziko na kwa wakristo siku ya Ibada, nawatakia nyote mapumziko mema ya mwisho wa Juma.
Nae mnyama huyu katika moja ya Mbuga zatu za wanyama akiwa amepiga pozi lake la Ki-weekend.