Wednesday 11 June 2014

WADAU HII IMEKAAJE?

Kawaida kazi ya Jeshi la Polisi ni USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO. Sasa tukio la leo huko Mkoani Pwani linaleta utata. Iweje sasa Raia wageuke na kupoteza uhai wa yule ambae amekuwa katika jopo la walinda usalama wao na mali zao?
Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH
NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi
30.
Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako