Sunday 29 June 2014

NAWATAKIA JPILI NJEMA

Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu mahali fulani hapa nchini. Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole. Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia kanisani kusali. Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?
Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,
“Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”
Mwanaume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada
“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, Asante kwa ujumbe wa leo kutoka kwa mtumishi wako Mchungaji, Asante kwa miujiza ya uponyaji. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika, Kanisa woote tuseme Amen”
Baada ya kumaliza sala tu, alijikuta kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu kwani ibada ndo tu ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya kufunga ibada!
hii kali.
Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la.


No comments:

Post a Comment

Maoni yako