Sunday 12 April 2015

SOKOINE; TUTAKUKUMBUKA DAIMA

Tarehe kama ya leo 12.04.1984, Taifa la Tanzania lilimpoteza kiongozi wake shupavu, aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine, kufuatia ajali ya gari eneo la WAMI-DAKAWA Kilomita 35 nje kidogo ya mji wa Morogoro. Waziri Mkuu huyu alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam baada ya kufunga Kikao cha Bunge mjini Dodoma.
Baada ya kuagwa kiserikali Jijini Dar, marehemu Sokoine alisafirishwa kwenda Monduli Juu Arusha kwa mazishi.
Atakumbukwa kama kiongozi shupavu na ambaye alikuwa hacheleweshi utekel;ezaji wa jambo pale linapoonekana linatakiwa utekelezaji wa haraka na madhubuti. Alipigana kupunguza rushwa na ufujaji wa mali, pia ulimimbikizaji wa mali mikononi mwa wachache (Ufisadi)
BAADHI YA KAULI ZA SOKOINE

"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983

"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983

No comments:

Post a Comment

Maoni yako