Tuesday 14 April 2015

MJUE MWANZILISHI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Sewa Hadji Paroo, mwana jamii ya Ismailia mzaliwa wa Zanzibar na mwanzilishi wa Hospitali ya Muhimbili mwaka 1891. Sewa Haji pia ndiye mwanzilishi wa Shule ya Msingi Mwambao Bagamoyo (Rais Jakaya Kikwete amesoma shule hii) na Hospitali ya Bagamoyo. Muhimbili ilibadilishwa jina toka Sewa Hadji kuwa Princess Magreth Hospital wakati wa utawala wa Uingereza. Hospitali ya Muhimbili (wakati huo Sewa Haji Hospital) ilifunguliwa rasmi Ijumaa Oktoba 1 1897, miezi 8 baada ya kifo cha Sewa Hadji.
Jengo la mwanzo kabisa la Hospitali ya Muhimbili wakati huo ikiitwa Sewa Hadji Hospital

JE WAJUA ASILI YA JINA MUHIMBILI????
Neno Muhimbili limetokana kwa kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza wazaramo walisema "hapo ndipo wanawake wanapoenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa nalo ladumu hadi leo.
Kibao kinachoelekeza Hospital ya Muhimbili.
Jengo la Hospital ya Muhimbili kitengo cha Moyo
Mojawapo ya majengo ya Muhimbili

No comments:

Post a Comment

Maoni yako