Monday 20 April 2015

SIFA ZA MGOMBEA URAISI KWA TIKETI YA CCM ZAAINISHWA

1. Anapaswa kuwa na uwezo wa kuliongoza Taifa kwa kuzingatia uzoefu alionaokatika uongozi wa shughuli za Serikali, umma na taasisi.
2. Awe mwadilifu, mwenye hekima na busara.
3. Awe na elimu ya kiwango cha Chuo Kikuu au inayolingana na hiyo.
4. Awe mwenye upeo na uwezo mkubwa wa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza Muungano wetu, umoja, amani na utulivu wetu pamoja na mshikamano wa kitaifa.
5. Awe mtu wa kuona mbali, asiyeyumbishwa, mwenye uwezo wa kufanya uamuzi wa busara kuhusu masuala nyeti na muhimu ya Taifa kwa wakati unaofaa.
6. Awe na upeo mkubwa usiotiliwa shaka kuhusu masuala ya kimataifaili aweze kuwa kiungo imara kati ya nchi yetu na Dunia yote kwa jumla.
7. Asiwe mtu mwenye hulka ya udikteka au ufashisti bali aheshimu na kuilinda Katiba ya nchi, sheria, utawala bora, kanuni na taratibu za utawala bora.
8. Awe mtetezi wa wanyonge, kusimamia haki za binadamu, mzingatiaji makini wa maendeleo ya raia wote na asiwe na tamaa ya kujitafutia umaarufu wake binafsi.
9. Awe mstari wa mbele kuzifahamu, kuzieleza, kuzitetea na kuzitekeleza Sera za CCM na Ilani ya CCM ya Uchaguzi.
10. Awe mpenda haki na jasiri wa kupambana na dhuluma,maovu yote nchini.
11. Asitumie nafasi yake ya uongozi kujilimbikizia mali.
12. Awe ni mtu anayekubalika na wananchi.
13. Awe makini katika kuzingatia masuala ya uwajibikaji wa uongozi, watendaji, asiyevumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu ili kuinua nidhamu ya kazi, tija na ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako