Monday 6 April 2015

CHARLES HILARY KUTOKA BBC SWAHILI KUELEKEA AZAM TV

Miongoni mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata kupitia Radio One pia.
Charles Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.
Azam Tv inazidi kupata watangazaji mahiri akiwemo Mkurugenzi wake Tido Mhando.

Charles Hillary akipewa zawadi ya jezi nyekundu yenye jina lake na mhariri wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Ali Saleh, (katikati), na mtangazaji mwenzake, Peter Musembi

No comments:

Post a Comment

Maoni yako