Monday 13 April 2015

MHE RAIS KIKWETE AONGEA NA MAASKOFU -SHINYANGA.

Mhe Rais Kikwete alikuwa miongoni mwa Waumini na watu wenye mapenzi mema waliojumuika katika Ibada ya kumsimika/kumtia wakfu Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu iliyofanyika katika Parokia ya Ngokolo,mjini Shinyanga hapo jana. Askofu Sangu anachukua nafsi iliyoachwa wazi Jimboni Shinyanga tangu Novemba 2012 kufuatia kifo cha aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga Marehemu Askofu Aloysius Balina.
Mhe. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kutoa wito wake. Soma hapa chini.
"'eh nchi yetu hii haina dini....mkiona tunaliamua jambo kama CCM ama kama serikali mjue tumeliamua kwa haki kabisa,,,nyie viongozi wa dini wasameheni wale wengine wanaowatusi ,,,
nyie ndio mnaotufundisha kuwa tusamehe saba mara sabini,
,,na mshukuru sana baba Kardinal Pengo kwa kusamehe...
anafundisha pakubwa sana hasa sisi tulio na nafasi kubwa hizi serikalini katika hilo...kwa hiyo jambo tulilo liamua baada ya kulifanyia uchunguzi wakina tutalitetea tu atakama baadhi ya watu litawakera,,,eh,,,serikali tunatambua sana umuhimu wenu viongozi wa dini katika kutuombea na mchango wenu katika jamii ...
na ndio mana tunasema kama kunamambo muhimu ambayo zipo baadhi ya sheria zinatatiza ama hazitambui ni wajibu wetu kuwasaidia katika hilo madhali zinafaida na jamii husika na wala kwa kufanya hilo hatuwezi kuwa wadini hata kidogo,,,oneni mimi mwuislamu leo nipo katikati yenu TUNAJENGA NCHI YETU...
Rais Kikwete akimpongeza Askofu Mpya Mhashamu Liberatus Sangu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako