Friday 10 April 2015

MGOMO WA MADEREVA NCHINI LEO

Abiria wakisubiri Daladala katika eneo la Unungo Darajani Dar bila mafanikio kufuatia mgomo
Heka heka Kituo cha Mabasi Ubungo Dar

Kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii, redioni na TV ni ripoti ya story kubwa ya mgomo wa mabasi ya abiria, Kituo cha Mabasi Ubungo kumekuwa na Vurugu kubwa,kuchomwa matairi ya magari barabarani.Hakuna basi lolote la abiria kwenda mikoani lililokuwa limetoka wala hakuna daladala iliyokuwa ikipakia abiria katika eneo hilo.Baada ya kuanza vurugu Polisi waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya.
Maafisa wa Polisi wakijadiliana jambo katika Stendi ya Nyegezi Mwanza ambapo mgomo nao umefanyika/
Hata hivyo, Mgomo huo ulioanza rasmi leo asubuhi baada ya madereva kuwa na malalamiko, umeisha baada ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, kufuta Agizo la Madereva kusoma upya katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

No comments:

Post a Comment

Maoni yako